DALILI ZA UGONJWA WA PUMU YA NGOZI
➡️ afyayangoziyako
• • • • • •
CR: @Afyayangoziyako
Maradhi haya ni ya muda mrefu, kwa hiyo mtu huweza kukaa nayo kwa muda mrefu ingawa siyo muda wote ngozi itaonyesha dalili za maradhi. Zifuatazo ni baadhi ya dalili za ugonjwa huu:
-Muwasho wa ngozi usio wa kawaida na kupelekea ngozi kupata vipele kisha kuwa kavu na ngumu
-Kuvimba kwa ngozi -Sehemu ya ngozi iliyoathirika huwa inatutumka
-Ngozi huwa inakuwa na mipasuko inayoweza kuruhusu vimelea vya maradhi kushambulia sehemu ya ndani ya ngozi
-Maeneo ya ngozi yaliyoathirika huweza pia kuwa na malengelenge na hata kutoa maji
-Bila matibabu ya haraka ngozi inaweza fanya vidonda
-Ingawa maeneo yenye kuathirika huweza kutokea sehemu yoyote ya mwili lakini pumu ya ngozi hupenda kushambulia sehemu za mikono hususani eneo baada ya kiwiko kwenda chini, miguu, viganja vya mikono, eneo la nyuma ya magoti (mkunjo wa mguu kwenye eneo la goti), maungio ya mkono kwenye kiwiko, shingo, sehemu ya juu ya kifua, wagonjwa wengune hupata maambukizi kwenye maeneo yanayozunguka macho, watoto wengi hupata pumu ya ngozi kwenye uso.
Kwa wenye pumu ya ngozi mbaya kabisa sehemu kubwa zaidi ya mwili hututumka na vidonda pamoja na kutokwa na majimaji kwenye maeneo yenye vidonda. Wakati maradhi haya yanapoanza hunyesha dalili za muwasho ambao husababisha mgonjwa kujikuna na kumsababishia mikwaruzo kwenye ngozi ambayo nayo husababisha vimelea vya maradhi kuweza kupenya na kusababisha vidonda vikubwa zaidi kutokea kwenye eneo la ngozi. Vidonda vinapotokea hasa kwa mtoto huweza kumsababishia msongo wa mawazo, kama hali hii ikimtokea kwa mtoto wa shule basi hata mahudhurio yake shuleni yatakuwa mabovu au hata kufeli mitihani
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!