FAIDA ZA KUNYWA MAJI MENGI MWILINI
➡️ Ombeni Mkumbwa
Maji ya Kunywa Yana Faida nyingi sana ambazo huenda ikawa nyingi huzifahamu kabsa. Licha ya Msemo wa "MAJI NI UHAI" lakini watu wengi hawaelewi siri iliyopo katika Msemo huu, na kuchukulia tu kama utani...!! Je wafahamu kweli kwamba Maji ni Uhai? Na kama unafahamu,kwanini tunasema Maji ni Uhai na Sio Soda?. Leo tuangalie makala hii ambayo inahusu Umuhimu wa unywaji wa Maji mengi mfano Lita 2.5 Kwa siku katika Mwili wa Binadamu na hata viumbe wengine...!!!
🔺Faida za Kunywa Maji mengi Mwilini Mfano;Wastani wa lita 2.5 kwa siku
- Kunywa Maji mengi hutibu tatizo la Kukosa Choo,pamoja na tatizo la kupata Choo kigumu
- Kunywa maji mengi husaidia kusafisha mwili na Kuondoa Sumu mwilini,hasa kwa Njia ya kukojoa
- Kunywa maji mengi husaidia kutibu magonjwa kama UTI(Urinary Track Infection) au kwa lugha ya Kiswahili ni maambukizi katika Njia ya Mkojo,ambapo tafiti zinaonyesha Unywaji wa maji Wastani wa lita 2.5 kwa siku,hupunguza uwezekano wa kupata UTI za mara kwa mara kwa zaidi ya asilimia 50%
- Unywaji wa maji mengi husaidia pia kutibu matatizo kama Kuumwa na KICHWA
- Kunywa maji mengi husaidia Ngozi ya mwili kunawiri kila wakati
- Unywaji Maji mengi husaidia kuzuia mtu kupatwa na Magonjwa Ya Moyo,Mfano; Utafiti uliofanyika Nchini Marekani kwa kipindi cha Miaka sita,husema kwamba unywaji waji Wastani wa Glasi 5 kila siku,husaidia kumkinga Mtu na magonjwa ya moyo kwa Wastani wa asilimi 41% zaidi ya wale wanaokunywa Glasi 2 au Chini ya hapa kwa siku
- Unywaji wa Maji mengi husaidia Kuupa Mwili Nguvu na kuondoa Uchovu kabsa.
- Kunywa Maji mengi husaidia kumkinga Mtu na Saratani ya Utumbo,kwani chakula na Usagaji wake utaenda vizuri kama Unakunywa Maji ya kutosha.
🔺Madhara ya Kutokunywa Maji mengi Mwilini
👉 Kupata Choo kigumu sana hivo kukupelekea kupata maumivu makali wakati wa kujisaidia,na hata michubuko pia sehemu ya Haja kubwa, Lakini pia kukosa Choo kabsa
👉 Kupatwa na Maumivu makali ya Kichwa
👉 Kuwa katika hatari ya kupatwa na Saratani ya Utumbo
👉 Kupatwa na Uchovu sana mwilini
👉 Kupatwa na UTI za mara kwa mara
👉 Kupatwa na matatizo ya Ini,kutokana na mwili kushindwa kutoa vizuri sumu mwilini
SUMMARY
Katika makala hii,tumegusia kuhusu Umuhim wa kunywa maji mengi mwilini,ambapo tumetaja baadhi ya Faida za Kunywa maji mengi mwilini,tukatolea Mfano wa wastani wa lita 2.5 Za Maji kwa siku
➖ KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584 PIGA SIMU AU TUMA UJUMBE,UTASIKILIZWA NA KUHUDUMIWA POPOTE ULIPO
#afya #Ushindi #Mtaji
afya
afyaclass
afyatips
magonjwa
magonjwa ya wanaume
magonjwa ya wanawake
magonjwa ya watoto
makala
muhimu
new
post
uzazi
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!