KUOTA KINYAMA UKENI-MASUNDOSUNDO/GENITAL WARTS

  KUOTA KINYAMA UKENI-MASUNDOSUNDO/GENITAL WARTS

➡️ Ombeni Mkumbwa

SUMMARY

Katika Makala Ya leo,tutaangalia vipengele vifuatavyo,kuhusu Ugonjwa huu wa kuota Kinyama Ukeni;

(1) Utangulizi/introduction kuhusu tatizo hili la kuota Kinyama ukeni

(2) Chanzo cha Tatizo hili la Kuota kinyama Ukeni

(3) Kundi ambalo lipo kwenye hatari ya Kupata ugonjwa huu wa Masundosundo

(4) Dalili za Ugonjwa huu wa masundosundo/Genital warts

(5) Madhara ya kuwa na Tatizo hili la Kuota kinyama Ukeni

(6) Tiba ya Ugonjwa huu wa masundosundo

(7) Maelekezo kuhusu kupata ushauri,elimu au Tiba kama unahitaji.

🔷 SOMO KAMILI

Masundosundo-Ni ugonjwa wa kuota kinyama au viupele upele katika ngozi laini ya sehemu za siri za mwanamke(ukeni) ambapo kwa kitaalam hujulikana kama Genital warts. Vinaweza kutokea katika maeneo kama,Uke,uume,shingo ya uzazi,mashavu ya uke na kuzunguka njia ya Haja kubwa kwa nje au kwa ndani pia. Ugonjwa huu unawasumbua wanawake wengi sana kwa sasa hivi. Kuna vyanzo au sababu za kutokea kwa Tatizo hili.

CHANZO CHA TATIZO LA KUOTA KINYAMA UKENI

Ngoja tuone sababu za Kutokea kwa Tatizo hili la kuota kinyama Ukeni; 🔻

Ugonjwa huu wa kuota Kinyama Ukeni au katika sehemu za siri za mwanamke husababishwa na kirusi kinachoitwa HUMAN PAPILLOMA VIRUS-(HPV), ambapo kuna aiana nyingi sana za Kirusi hichi ambapo ndyo zinazoleta magonjwa mbalimbali kama Saratani ya Shingo ya Kizazi(cervical cancer) n.k, aiana hizi zimewekwa katika kundi linalojulikana kama HIGH RISK HPV. 

 

Soma: Chanzo cha Kuota Nyama Puani na Tiba yake


 KUNDI AMBALO LIPO KWENYE HATARI YA KUPATA TATIZO HILI

  • Mtu ambaye huanza mapenzi mapema hasa kabla ya miaka 18
  • Mtu mwenye wapenzi wengi- yaani multiple partners
  • Ngono zembe
  • Mwenye Virusi vya Ukimwi
  • Mwenye Saratani ya shingo ya Kizazi
  • Mjamzito kutokana na Upungufu wa kinga mwilini kipindi cha Ujauzito
  • Mtumiaji wa sigara na Pombe

🔴 DALILI ZA UGONJWA WA MASUNDOSUNDO/GENITAL WARTS

Dalili kubwa ya Ugonjwa huu ni kuota kinyama katika Ngozi laini ya Uke,Mirija ya mkojo,Uume,shingo ya kizazi,sehemu ya Nje na ndani kuzunguka eneo la haja kubwa.
Kupata Viupele upele katika maeneo ya sehem za Siri kama vile; katika mashavu ya Uke,uume n.k

Kupatwa na miwasho eneo lenye kinyama au viupele, na wakati mwingine,eneo lote hili kukosa hisia yaani Kupata GANZI

Kutokwa na Uchafu ukeni,maumivu wakati wa tendo la Ndoa, na hata wakati mwingine kutokwa na damu ukeni,wakati wa Tendo la Ndoa.

VIPIMO NA TIBA

Ni muhimu sana kwa Mtu mwenye dalili za Ugonjwa huu kwenda hospitalin kufanya vipimo mbali mbali ikiwemo,kufanya full checkup ya Saratani ya Shingo ya Kizazi,kwani pia virusi hivi vya HUMAN PAPILLOMA VIRUS (HPV), ndivo vinavyoleta Ugonjwa au tatizo la Saratani ya shingo ya Kizazi kwa Kitaalam tunaita cervical Cancer.




KWA USHAURI ZAIDI/ELIMU/TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584 POPOTE ULIPO....




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!