MADHARA YA KUVAA VIATU VIREFU KWA WANAWAKE
➡️ Ombeni Mkumbwa
ℹ️MADHARA YA KUVAA VIATU VYENYE VISIGINO VIREFU AU VIATU VIREFU
(1) Maumivu ya mgongo
viatu virefu ni mtindo mpya au fashion kwa wadada wengi wa siku hizi wanaopenda mambo ya urembo, lakini pia hupendelewa sana na wasichana wafupi ili nao waonekane warefu.
kuna madhara mengi yatokanayo na uvaaji wa viatu hivi virefu na usipokua makini unaweza kudhani labda ni magonjwa mengine tu yanakuandama kumbe mchawi wako ni viatu vyako mwenyewe. hebu tuyaone madhara hayo kwa kirefu.
maumivu ya mgongo; katika hali ya kutembea na viatu virefu sana mtumiaji hukosa balance yaani uzito wa mwili wake unashindwa kubalance kati ya upande wa kushoto na kulia wa mwili wake hivyo hupata maumivu makali sana ya mgongo na kuhisi dalili za kutoneshwa akiguswa hasa sehemu za mgongo wa chini.
(2) Ugumba
Ugumba; kama nilivyosema kwenye pointi ya kwanza kukosa kwa balance ya mwili husababisha kupotea balance ya kwenye nyonga pia, hali hii hufanya mfuko wa uzazi kukaa vibaya na kua katika sehemu ambayo sio sahihi. hali hii huweza kumnyima mama mtoto na huambatana na dalili kama maumivu wakati wa tendo la ndoa, kushindwa kuzuia mkojo, na kushindwa kubeba mimba.
(3) Maumivu ya misuli ya nyuma ya miguu
maumivu ya misuli ya nyuma ya miguu; viatu virefu huleta maumivu makali ya nyama za nyuma ya mguu litaalamu kama calf muscles na ukiwachunguza vizuri watu wengi wanaovaa viatu hivyo hawawezi kusimama kwa muda mrefu yaani wataomba kiti wakae kila sehemu sababu ya maumivu makali, lakini pia mishipa huchomoza kwenye mishipa hiyo na kuleta maumivu inapoguswa.
(4) Kubadilika kwa muonekano wa Vidole
kubadilika kwa muonekano wa vidole; kutokana na kidole gumba kushindwa kuhimili mgandamizo unaopata kutoka kwenye mwili mzima, kidole hicho hujikuta kinapinda na kuleta shepu ambayo sio ya kawaida, hii sio nzuri sana kwa urembo na huweza kuleta maumivu.
mishipa ya damu kukunjika; mguu unaovishwa kiatu kirefu mara nyingi hujilazimisha kuingia kwenye kiatu kirefu na chembamba hii hufanya mishipa ya damu kujikunja sana na kua midogo sana na katika hali mbaya sana mishipa ya damu huweza kukatika.
(5) Maumivu ya joint ya mguu
maumivu ya joint ya mguu; presha kubwa kwenye joint ya mguu kitaalamu kama knee joint husababisha maumivu makali ya joint hiyo na kua kama chanzo cha ugonjwa wa kuvimba na kuumwa joint kitaalamu kama osteoarthritis.
(6) Kupinda kwa mgongo
kupinda kwa mgongo; kukosa kwa balance ya mwili wakati wa kutembea humfanya mtu kijaribu kupinda kidogo ili kupata balance, baada ya muda mrefu mgongo huanza kuzoea hali ile na kuleta maumivu makali yakiambatana na kupinda kwa eneo la juu na enoe la chini la mgongo.
kuvunjika mifupa; baadhi ya watu wamewahi kupata ajali kwa kushindwa kuvihimili viatu virefu na kuanguka navyo, baadhi yao waliweza kuvunjika mifupa ya kisigino au mifupa ya vidole kama picha hapo chini inavyoonyesha.
(7) maumivu ya unyayo
katika matembezi ya kutumia viatu virefu kwa muda mrefu mgonjwa husikia maumivu makali ya kisigino, unyayo kwa chini na vidole kwa mbele, hii huweza kumnyima raha na kupunguza ufanisi wa shughuli zake za kila siku.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!