MADHARA YA POMBE KWA MJAMZITO

 MADHARA YA POMBE KWA MJAMZITO

➡️ Ombeni Mkumbwa

Utangulizi:

Watu wengi hawajui kwamba ukiwa Mjamzito kuna vitu vingi hutakiwi kuvifanya kwa ajili ya mtoto aliye tumboni pamoja na afya yako pia.
Vitu hivi vinahusisha Mtindo wa maisha wa mama Mjamzito,ikiwemo kutokuvaa nguo zinazobana,Viatu virefu, Kutokutumia Dawa hovyio kwani baadhi ya dawa zina madhara makubwa Kwa Mjamzito, na Kuacha Vilevi vyote ikiwemo POMBE na SIGARA kwani vyote hivi madhara yake kwa Mjamzito ni makubwa.
Leo tutaangalia Baadhi Ya Madhara Ya Pombe kwa Mjamzito

MADHARA YA POMBE KWA MJAMZITO

Kuna madhara makubwa sana ya Utumiaji wa Pombe wakati wa Ujauzito,na Madhara hayo ni Pamoja na Haya yafuatayo;

~ Mimba kuharibika, Mtumiaji wa Pombe wakati wa Ujauzito ana hatari kubwa ya Kupata tatizo la Mimba kuharibika kabla hata hajajifungua, na hii huchangiwa kwa kiasi kikubwa na machemical yaliyopo kwenye pombe au hata hatari za kudondoka wakati ukiwa umelewa

~ Kuzaa mtoto mwenye Uzito mdogo sana ambapo kitaalam Huitwa Low Birth weight (LBW), Asilimia kubwa ya wakina mama ambao hunywa pombe kipindi cha Ujauzito huzaa watoto wenye uzito mdogo sana, na mara nyingi watoto hawa wanakuwa wadhaifu kupita kiasi.

~ Fahamu pia pombe huadhiri ubongo kwa kiasi kikubwa hasa katika Maswala ya kumbumbuku,Hivo pia mama anayetumia pombe wakati wa Ujauzito huweza kuleta athari katika ubongo wake pamoja na Ubongo wa mtoto pia,na kumfanya mtoto aliyezaliwa kutokuwa na uwezo mkubwa wa kutunza kumbukumbu,Hivo kuwa tatizo kubwa katika maisha yake hata katika Swala la Elimu pia.

~ Maumivu makali ya Tumbo huweza kutokea pia kwa Mama Mjamzito anayetumia pombe katika kipind hicho

KUMBUKA YAFUATAYO KAMA WEWE NI MJAMZITO

✓ Acha kutumia kilevi chochote kama POMBE na SIGARA kwa ajili ya afya yako na afya ya mtoto aliyetumboni

✓ Acha kuvaa nguo zinazobana,Mikanda,au Viatu virefu wakati wa Ujauzito

✓ Epuka matumizi ya dawa hovio bila maelekezo ya wataalam wa afya kwani dawa zingine zina madhara makubwa kwa Ujauzito wako na kiumbe ulichobeba tumboni

✓ Lishe bora izingatiwe wakati wa Ujauzito

✓ Usafi wa mwili wako ni muhim sana

✓ Hudhuria Kliniki zote kipindi cha Ujauzito

🔺SUMMARY

Vitu ambavyo tumevizungumzia katika makala hii ni pamoja na;

(1) Utangulizi

(2) Madhara ya Pombe kwa mama mjamzito

(3) Mambo muhimu ya Kuzingatia kwa mama mjamzito

(4) Maelekezo ya kupata Elimu,ushauri au Tiba kama una tatizo lolote la kiafya

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KUPITIA NAMBA +255758286584

 MADHARA YA POMBE KWA MJAMZITO

➡️ Ombeni Mkumbwa


Pombe ina madhara makubwa sana kwa Mjamzito ikiwemo;

Mama mjamzito kupata maumivu makali ya tumbo na Ujauzito kuharibika wenyewe

Kuzaa mtoto mwenye uzito mdogo na matatizo ya ubongo ikiwemo swala nzima la kutokuwa na kumbukumbu vizuri.

Kuwa katika hatari ya mama kupata Uzito kupita kiasi au Obesity,hali ambayo ni hatari kuleta magonjwa kama kisukari wakati wa Ujauzito,presha wakati wa Ujauzito(PREGNANCY INDUCED HYPERTENSION n.k

Epuka matumizi ya pombe hasa wakati wa Ujauzito kwa ajili ya afya yako pamoja na Mtoto aliyetumboni kwako




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!