MAGONJWA YA ZINAA-SEXUAL TRANSMITTED DISEASES(STD's),AINA ZAKE,DALILI ZAKE PAMOJA NA MATIBABU YAKE
MAGONJWA YA ZINAA-SEXUAL TRANSMITTED DISEASES(STD's),AINA ZAKE,DALILI ZAKE PAMOJA NA MATIBABU YAKE
➡️ Ombeni Mkumbwa
🔴 SUMMARY
Katika Makala hii tutajadili kuhusu Magonjwa ya zinaa, na tutagusia katika Vipengele vifuatavyo;
(1) Maana ya Magonjwa ya Zinaa ambapo kitaalam Hujulikana kama Sexual Transmitted Diseases(STD's)
(2) Aina zote za Magonjwa ya Zinaa pamoja na visababishi vyake- Sexual Transmitted Diseases(STD's) types and Causes.
(3) Dalili za Magonjwa ya Zinaa- Sexual Transmitted Diseases(STD's)
(4) Makundi ambayo yapo katika hatari zaidi ya kupata Magonjwa ya Zinaa- Sexual Transmitted Diseases(STD's)
(5) Tiba ya Magonjwa ya zinaa- Sexual Transmitted Diseases(STD's)
☑️ SOMO KAMILI
Magonjwa ya zinaa ambapo kwa Kitaalam hujulikana kama Sexual Transmitted Diseases(STD's)- Ni magonjwa yote ambayo Njia kuu ya uenezwaji wake ni Ngono au huambukizwa kutoka kwa Mtu Mmoja kwenda kwa Mwingine kwa Njia ya Ngono ama Kujamiana/Kufanya Tendo la Ndoa(Sexual Intercourse). Na magonjwa haya yapo mengi na aina tofauti tofauti kama Ufatavyo;
AINA ZA MAGONJWA YA ZINAA-SEXUAL TRANSMITTED DISEASES(STD's)
- Ugonjwa wa UKIMWI-HIV
- Ugonjwa wa Kisonono au kwa itaalam huitwa Gonorhea
- Ugonjwa wa Kaswende au kwa kitaalam huitwa syphilis
- Ugonjwa wa Homa ya Ini ambapo kaa kitaalam huitwa Hepatitis
- Ugonjwa wa Chlamydia N.k
VISABABISHI VYA MAGONJWA YA ZINAA-SEXUAL TRANSMITTED DISEASES(STD's)
- Kufanya Mapenzi katika Umri mdogo- Kufanya Ngono zembe pasipo kutumia Kinga Kama vile Kondom- Kufanya mapenzi au kushiriki tendo la Ndoa kinyume na maumbile- Tabia ya kuwa na wapenzi wengi
DALILI ZA MAGONJWA YA ZINAA KWA UJUMLA WAKE-SIGNS AND SYMPTOMS OF SEXUAL TRANSMMITED DISEASES(STD's)
🔻Kutokwa na Usaha sehemu za siri kwa mwanaume na mwanamke pia
🔻Kutokwa na Uchafu wenye rangi kama maziwa,njano,Cream n.k ambao huambatana na harufu kali ukeni
🔻Kupatwa na miwasho ukeni au katika sehemu za Siri kwa mwanaume na mwanamke
🔻Kutokwa na Damu ukeni wakati wa kushiriki Tendo la Ndoa
🔻Kupata maumivu makali sana ukeni wakati wa Tendo la Ndoa
🔻Maumivu makali ya Tumbo chini ya kitovu
🔻Kuumwa na Homa, mwili kukosa Nguvu,kusikia kichefuchefu na kutapika Pia
🔻Kutokwa na Maji maji yenye harufu mbaya sehemu za Siri
🔻Kupata maumivu makali wakati wa kukojoa,sehemu za siri kuungua,kuchubuka na mkojo kuchoma
MADHARA YA KUPATA MAGONJWA YA ZINAA- EFFECTS OF SEXUAL TRANSMMITED DISEASES
- Kukosa mtoto au kushindwa kubeba Mimba kwa mwanamke
- Maumivu wakati wa tendo la Ndoa
- Kukimbiwa na mume kutokana na kutokwa na uchafu au maji maji yenye harufu kali ukeni
- Kifo
MAKUNDI YA WATU AMBAO WAPO KWENYE HATARI YA KUPATA MAGONJWA YA ZINAA- RISK GROUPS FOR SEXUAL TRANSMMITED DISEASES
1️⃣ Watu wenye wapenzi wengi
2️⃣ Watu wanaoshiriki mapenzi kinyume na maumbile
3️⃣ Wanaofanya ngono zembe-Unsafe sexual intercourse
4️⃣ Wanaoanza kufanya mapenzi wakiwa katika Umri Mdogo
MATIBABU
Matibabu Ya Magonjwa ya Zinaa hutegemea na aina ya Ugonjwa wa zinaa uliokupata,hivo basi kwa Ushauri ni bora kwenda hosptal kama Una dalili zozote ambazo huzielewi ili kupata Msaada kutoka kwa Wataalam wa afya,Ili kupata tiba kutokana na Ugonjwa Husika.
@kwa Ushauri zaidi,Elimu au Tiba tuwasiliane kwa namba +255758286584 piga simu au Tuma Ujumbe utahudumiwa kwa haraka popote ulipo.
#Magonjwayazinaa #afyabora #ushindi
afya
afyaclass
afyatips
magonjwa
magonjwa ya wanaume
magonjwa ya wanawake
magonjwa ya watoto
makala
mpya
muhimu
new
post
uzazi
videos
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!