MKANDA WA JESHI
➡️ MKANDA WA JESHI NI UGONJWA GANI? ❝ SWALI AMBALO NIMEULIZWA SANA WIKI HII INBOX ❞
☑️ MAJIBU:
Mkanda wa jeshi (shingles) ni jina linalotumika mitaani kuutaja ugonjwa unaoshambulia ngozi na kujenga tabaka la vijipele vikubwa venye majimaji ambavyo mara nyingi hukamata upande mmoja wa mwili.
Ingawa vijipele vya mkanda wa jeshi vinaweza kutokea sehemu yo yote ya mwili, mara nyingi hupenda kuota kifuani, shingoni, usoni, mgongoni na mikononi.
Vijipele hivi hukaa juu ya ngozi kwa muda wa wastani wa wiki mbili hadi sita kisha hupotea. Vipele vya mkanda wa jeshi huambatana na maumivu makali na kusikia ngozi kuwaka moto.
🆑KUMBUKA: SIO KILA MWENYE MKANDA WA JESHI NI MUATHIRIKA WA UKIMWI
📶 WATU AMBAO WAPO KWENYE HATARI YA KUPATA MKANDA WA JESHI
‣ Mkanda wa jeshi huwapata zaidi watu wenye umri mkubwa, zaidi ya miaka 50, utafiti ukionyesha kuwa zaidi ya nusu ya watu wenye umri wa zaidi ya miaka 80 hupatwa na mkanda wa jeshi.
‣ Vilevile huwapata zaidi watu waliopatwa na magonjwa yanayopunguza kinga za mwili, kama vile, UKIMWI na saratani.
‣ Tiba za mionzi na chemotherapy huweza kupunguza kinga za mwili za mgonjwa na kumfanya awe kwenye hatari kubwa ya kupata mkanda wa jeshi.
#SOMA Zaidi hapa kuhusu tatizo la Mkanda wa Jeshi
KWA USHAURI ZAIDI/ELIMU/TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!