TATIZO LA MGONGO WAZI KWA WATOTO
➡️ Ombeni Mkumbwa
Uti wa mgongo ulio wazi(Spinal bifida) ni hali ambayo mtoto anazaliwa nayo huku uti wa mgongo(mishipa ya fahamu mkubwa unaotoka kwenye ubongo) ukiwa wazi kutokana na mifupa(vipingili vya uti wa mgongo) kutokufunga vizuri.Mgongo wazi(spinal bifida) inaweza pata watoto 3 kati ya watoto 10000 wanaozaliwa
Uti wa mgongo hutengenezwa mara tu baada ya mimba kutungwa, ikiwa kuna kasoro katika utengenezaji wa uti huu basi sehemu fulani ya uti wa mgongo itabaki bila kuzibwa.
Visababishi
Kuna sababu mbalimbali zinapelekea uti wa mgongo kutoziba, ambazo zinaweza zuhilika, nazo ni Upungufu wa folic acid(vit B9) na vitamin B12 katika kipindi cha ujauzito, katika kipindi cha miezi ya awali
mama mjamzito kupiga X-ray, mattumizi ya dawa za kifafa katika kipindi cha ujauzito
Pamoja na maambukizi ya baadhi ya virusi kwa mama mjamzito.
DALILI ZA UGONJWA HUU
Kuwa na uvimbe nyuma chini ya mgongo
Kuwa na vinyweleo sehemu za chini za mgongo bila kuwa na tatizo la mishipa ya fahamu
Kushindwa kutembea ama kukosa hisia katika miguu
Mtoto anaweza kushindwa kuzuia haja kubwa ama ndogo endapo mishipa yote ya fahamu imepita katika tundu hilo
Na dalili zingine zinazoambatana kuharibika kwa mishipa
MATIBABU YA MGONGO WAZI
(1)Upasuaji
Upasuaji ni tiba pekee ya uti wa mgongo ulio wazi(spinal bifida) inayofanywa na madaktari bingwa wa upasuaji wa mishipa ya fahamu(neurosurgeons) wanachofanya ni kuziba lile tundu lililowazi.
(2)Dawa na viinilishe
Wanawake wengi walio katika kipindi cha kuzaa na wajawazito hawatumii vyakula vyenye vitamin B na folic acid inavyopaswa, vyakula hivyo ni matunda,mboga za majani, mbaazi na choroko.
Mwanamke mjamzito akipata lishe yenye virutubisho hivyo pamoja na kunywa vidonge vya folic acid, kwa asilimia 30% inaweza kupunguza hatarishi ya kupata watoto wenye uti wa mgongo ulio wazi.
Pia kwa wanawake wajawazito katika kipindi cha miezi mitatu ya mwanzo, wanashauriwa kutokupiga X-ray.
#afyacheck_
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!