UGONJWA WA FIGO KUFELI AU KUSHINDWA KUFANYA KAZI(KIDNEY FAILURE),CHANZO,DALILI,VIPIMO,NA MATIBABU YAKE
UGONJWA WA FIGO KUFELI AU KUSHINDWA KUFANYA KAZI(KIDNEY FAILURE),CHANZO,DALILI,VIPIMO,NA MATIBABU YAKE
Pointi muhimu;
Tatizo la figo kufeli mara nyingi huchangiwa na mwenendo mzima wa kretini/ serum.
Kufeli kwa figo, kunaweza kuleta shida mbali mbali mwilini kama vile;
- kuongezeka kwa maji mwilini na kusababisha uvimbe mfano; Uvimbe wa Miguu n.k
- viwango vya asidi kuongezeka,
- viwango vya potasiamu kuongezek
- viwango vya kalsiamu kuongezeka
- viwango vya phosphate kuongezeka
- Na katika hatua za baadaye, upungufu wa damu mwilini hutokea.
🔷Aina za Figo kufeli au Kushindwa kufanya kazi
Kuna Aina mbili kuu ambayo ni
(i) Figo kushindwa kufanya kazi ndani ya mda mfupi kwa kitaalam tunaita Acute kidney Failure, ambayo hutokana na Figo kuumia gafla na mara nyingi mgonjwa hupata matibabu ya kutosha na hali ikawa sawa
(ii) Figo kushindwa kufanya kazi pamoja na kuwa na ugonjwa sugu wa figo ambapo kitaalam hujulikana kama Chronic kidney failure ambao mara nyingi hauwezi kutibika kabsa. Katika aina zote mbili,kuna sababu ya msingi zinazochangia Ugonjwa wa figo kufeli;
🔷 SABABU ZA UGONJWA WA FIGO KUFELI-KIDNEY FAILURE
Sababu kubwa za kuwa na ugonjwa wa figo usiopona ni pamoja na;
1. Ugonjwa wa Kisukari:
Ugonjwa wa Kisukari ni miongoni mwa sababu kubwa za tatizo la figo kufeli. Tafiti zinaonyesha Asilimia 35% mpaka 40% ya magonjwa ya figo yasiyopona yote husababishwa na ugonjwa kisukari. Ambapo ni sawa na kusema katika kila watu watatu(3) walio na ugonjwa wa kisukari, mmoja(1) wao anaweza kupata ugonjwa sugu wa figo.
2. Tatizo la Presha au shinikizo la damu:
Ugonjwa wa Presha au Shinikizo la damu usipodhibitiwa vizuri,huweza kuwa chanzo kikubwa cha ugonjwa wa figo kufeli au kushindwa kufanya kazi. Tafiti zinasema katika Asilimia 30% ya magonjwa ya figo yasiyopona husababishwa na shinikizo la damu.
3. Kuwa na tatizo lingine la uvimbe kwenye figo au kwa kitaalam huitwa Glomerulonephritis
Tatizo hili la Glomerulonephritis ni la tatu katika kusababisha magonjwa sugu ya figo likiwemo hili la Figo kufeli au kushindwa kufanya kazi.
4. Ugonjwa ambao hujulikana kama Polycycystic Kidney Disease
Huu ni ugonjwa ambao huhusisha kuwepo kwa uvimbe kwenye figo zote mbili na mara nyingi ugonjwa huu unaweza kurithiwa kutoka kwa wazazi.
5. Na uwepo wa Sababu zingine kama vile;
- Umri mkubwa wa figo au Figo kuzeeka
- Tatizo la kufunga kwa mishipa iendayo kwenye figo yaani kwa kitaalam hujulikana kama renal artery stenosis
- Uwepo wa mawe ya Figo(Kidney Stones) ambayo huzuia Mkojo kupita au uwepo wa tatizo la tezi dume iliyo karibu na kibofu
- Tatizo la figo kuathiriwa na matumizi ya baadhi ya dawa
- Tatizo la figo kushambuliwa na magonjwa ya mara kwa mara
- kwa watoto kupatwa na tatizo la kupungua ukubwa wa figo na mwisho mkojo kurudi nyuma.
Utambuzi wa Tatizo hili
Kushindwa kwa figo husababishwa na kupungua kwa uwezo cha kuchuja ndani ya glomerular, ambapo tunazungumzia kiwango cha damu ambacho huchujwa kwenye glomeruli ya figo. Hii hugunduliwa baada ya kupungua kwa au kutokuwepo kwa uzalishaji wa mkojo au taka mwili (creatinine au urea) katika damu. Kulingana na sababu hizo, Hali ya hematuria yaani kutoka kwa damu kwenye mkojo na proteinuria (upotezaji wa protini kwenye mkojo) inaweza kutokea.
🔻DALILI ZA UGONJWA WA FIGO KUFELI-KIDNEY FAILURE
Dalili zinaweza kutofautiana kutoka kwa mtu hadi mtu.
(1) Tatizo la Kuvimba uso,Miguu na tumbo
Tatizo la Kuvimba uso, miguu na tumbo, ni ishara za ugonjwa wa figo. Japo si kila uvimbe hutokana na tatizo la Figo kufeli.
(2) Tatizo la Kukosa hamu ya chakula, kichefuchefu, na kutapika
Tatizo la Kukosa hamu ya chakula huweza kumpata mtu mwenye tatizo la figo kufeli,hii hutokana na uwepo wa sumu nyingi hivo kuleta hali ya kichefuchefu, kutapika na kwikwi.
(3) Kupata tatizo la presha au Shinikizzo la damu
Tatizo hili ni kawaida sana kwa wagonjwa wa Figo kufeli.
(4)Tatizo la ukosefu wa damu
Kupatwa na hali ya udhaifu na kuchoka mapema
(5) Tatizo la kupata maumivu ya mgongo,kujikuna na maumivu ya miguu (cramps) pamoja na Malalamishi ya mkojo
Dalili zingine zinazohusu mkojo ni pamoja na:
1. Kiwango cha Mkojo kupungua
2. Kupata Muwasho wakati wa kukojoa
3. kukojoa mara kwa mara
4. kukojoa damu au usaha
5. Ugumu wa kukojoa
KWA USHAURI ZAIDI/ELIMU/TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!