UGONJWA WA FISTULA MAANA YAKE,CHANZO CHAKE,DALILI NA TIBA YAKE
Karibu katika makala hii,kujua Zaidi Ugonjwa huu wa FISTULA,Vipo vipengele ambavyo tutavigusia kama ifuatavyo;
- Utangulizi Kujua maana ya Ugonjwa wa FISTULA na Aina za Fistula
- Chanzo cha Ugonjwa huu wa Fistula
- Makundi ambao yapo katika hatari za kupata Ugonjwa wa Fistula
- Dalili zote za Ugonjwa wa Fistula
- Tiba za Ugonjwa wa Fistula
- Maelekezo Jinsi ya kupata Ushauri,Elimu au Tiba kama Unahitaji
🔻SOMO KAMILI
Ugonjwa wa Fistula ni nini?
FISTULA- Huu ni Ugonjwa unawapata WANAWAKE ambapo unahusisha kuwepo kwa tundu au upenyo katika layer mbili Mfano; Tundu kati ya Njia ya Mkojo na Kibofu cha Mkojo, Tundu kati ya Njia ya Mkojo na Njia ya Haya Kubwa,Tundu kati ya Njia ya Mkojo na Utumbo Mkubwa n.k. Ambapo matokeo yake husababisha mwanamke kushindwa Kujizuia kukojoa, au Uchafu wa Haja Kubwa kutokea Njia ya Haja Ndogo n.k
👉 BAADHI YA AINA ZA UGONJWA WA FISTULA
(1) RectoVaginal Fistula(RVF)- Hii ni aina ya Fistula ambayo huhusisha Tundu kati ya Njia ya Haja Kubwa na Uke wa mwanamke
(2) ColoVaginal Fistula(CVF)-Hii ni aina ya Fistula ambayo huhusisha Tundu kati ya utumbo mkubwa na Uke wa mwanamke
(3) VesicoVaginal Fistula (VVF)- Hii ni aina ya Fistula ambayo huhusisha Tundu kati ya kibofu cha Mkojo na Uke au Njia ya Mkojo ya mwanamke
Chanzo cha Ugonjwa Huu wa FISTULA
- Majeraha au Tundu ambalo hutokea wakati Mwanamke anajifungua,ambapo linaweza kusabibishwa na uzembe wakati wa upasuaji,au mgandamizo wa mtoto wakati anatoka,au wakati mama anasaidiwa kutolewa mtoto wakati anajifungua kwa Njia ya kawaida,ambapo hii huhusisha matumizi ya vifaa vyenye ncha kali Mfano wakati wa procedure inaitwa Episiotomy au Forceps Delivery.
- Maambukizi ya Magonjwa mbali mbali kama HIV na magonjwa mengine ya Zinaa,uwepo wa Ugonjwa wa CANCER,Ugonjwa wa TB, na Magonjwa katika Utumbo ambapo kitaalam tunasema Intestinal diseases like;Crohn's disease and diverticulitis.
- Matibabu yanayohusisha Mionzi ambapo kitaalam Hujulikana kama RADIATION TREATMENT
Dalili za Ugonjwa wa Fistula
✓ Mwanamke kutokwa na Mkojo pasipo Kujizuia (Dalili kubwa na kiashiria kikubwa cha Ugonjwa wa Fistula)
✓ Uchafu wa Haja Kubwa(Kinyesi) kutoka katika Njia ya Haja Ndogo(ukeni)
✓ Mwanamke kuwa na Harufu ya Mkojo mda wote (Urine Smell)
✓ Mwanamke kutembea kama Amepinda
✓ Mwanamke kunuka Harufu ya Kinyesi
✓ Mwanamke kupata homa,maumivu makali ya Ubavu na Tumbo chini ya kitovu
📶 Kundi Ambalo lipo kwenye Hatari ya Kupata Ugonjwa wa Fistula
- Kuwa mwanamke au Jinsia ya Kike
- Mwanamke Mjamzito na anayejifungua
- Mwanamke mwenye magonjwa kama HIV na magonjwa mengine ya Zinaa(sexual Transmitted Diseases),CANCER,tuberculosis(TB), Magonjwa ya Utumbo ambapo kitaalam tunasema Intestinal diseases like;Crohn's disease and diverticulitis
- Mwanamke anayepata huduma au tiba ya mionzi- RADIATION TREATMENT
Vipimo; Vipo vipimo mbali mbali,kama vile vya magonjwa yote ya maambukizi,vipimo vya Mkojo,Na pia kufwatilia kwa Makini kuhusu Dalili za Ugonjwa wa Fistula kwa Mgonjwa
TIBA AU MATIBABU YA UGONJWA WA FISTULA
Ugonjwa wa Fistula,baada ya kugundulika zipo njia mbali mbali za Kutibu tatizo hili kulingana na Chanzo cha Tatizo hili,Na Njia hizo ni kama;👉Mwanamke kufanyiwa Upasuaji kisha kuzibwa sehemu ya Tundu la FISTULA,👉 Baada ya Upasuaji,mwanamke atapewa dawa mbali mbali ikiwemo za kuzuia na kutibu maambukizi mbali mbali
KUMBUKA;
Ugonjwa huu wa FISTULA unatibika kabsa,kwahyo basi kama unatatizo hili umekata tamaa,Tiba ipo usiabike,nenda Hosptal kapate matibabu, fistula inatibika kabsa.
#FISTULA #TIBA #USHINDI
@Kwa Ushauri Zaidi,Elimu au Tiba tuwasiliane kwa namba +255758286584,Tuma Ujumbe au Piga simu utasikilizwa na kuhudumiwa kwa haraka popote Ulipo.
afya
afyaclass
afyatips
magonjwa
magonjwa ya wanaume
magonjwa ya wanawake
magonjwa ya watoto
makala
muhimu
new
post
uzazi
videos
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!