Ticker

6/recent/ticker-posts

UGONJWA WA KIFAFA CHA MIMBA



UGONJWA WA KIFAFA CHA MIMBA

PART 1:

 UGONJWA WA KIFAFA CHA MIMBA MAANA YAKE,CHANZO CHAKE,VIHATARISHI VYA KUPATA KIFAFA CHA MIMBA,DALILI ZAKE,MADHARA YAKE NA TIBA YAKE

UGONJWA WA KIFAFA CHA MIMBA NI NINI?

Kifafa cha Mimba- Ni ugonjwa ambayo huhusisha kuwa na Mgandamizo mkubwa wa damu/shinikizo la damu au kitaalam (Pressure) kubwa wakati wa Ujauzito Mfano; Presha Kubwa kuliko au sawa na 140/110mmHg pamoja na kuwepo kwa Protein kwenye Mkojo yaani kitaalam hujulikana kama "PROTEINURIA" mfano; uwepo wa zaidi ya 300mg za Protein kwenye Mkojo.

🔷 KUMBUKA; Ugonjwa wa Kifafa cha Mimba huweza kutokea wakati wa Ujauzito na mara tu baada ya Mama Kujifungua.Lakini leo tutaangalia ugonjwa wa kifafa cha Mimba kipindi mama Akiwa Mjamzito.

☑️ SUMMARY-KIFAFA CHA MIMBA

 ➖ PRESSURE KUWA KUBWA MFANO;140/110mmHg wakati wa Ujauzito

➖PAMOJA NA UWEPO WA PROTEIN KWENYE MKOJO Mfano; Zaidi ya 300mg za Protein kuwepo kwenye Mkojo wakati wa Ujauzito

‼️SABABU HIZO MBILI NILIZOZITAJA HAPO JUU NI VIASHIRIA VYA UGONJWA WA KIFAFA CHA MIMBA

🔺CHANZO CHA UGONJWA WA KIFAFA CHA MIMBA

❝ Sababu za Moja kwa Moja za kutokea kwa Ugonjwa wa Kifafa cha Mimba hazijulikani,Japo vipo vitu ambavyo huweza kukuweka katika hatari ya kupata ugonjwa wa kifafa cha Mimba ❞

📶 VIHATARISHI VYA KUPATA KIFAFA CHA MIMBA

 ‣ Kupata shinikizo la Damu au Presha Kuanzia wiki 20 Za Ujauzito

‣ Kuwa na Uzito mkumbwa wakati wa Ujauzito

‣ Kuwahi kupata kifafa cha Mimba katika Ujauzito uliopita,upo kwenye hatari ya kupata kifafa cha mimba hata katika Ujauzito wa Sasa

‣ Kuwepo kwa historia ya Kifafa cha Mimba katika Familia yenu

‣ Uwepo wa Protein kwenye Mkojo hata kama haijafika 300mg

‣ Kupata Ujauzito kabla ya miaka 20 au baada ya Miaka 40

‣ Uwepo wa Mapacha(Twins) au zaidi ya watoto wawili tumboni(Triplets n.k)

DALILI ZA UGONJWA WA KIFAFA CHA MIMBA

1️⃣ Dalili ya Kwanza na kubwa kuliko zote ni uwepo wa Mgandamizo mkubwa wa damu yaani PRESSURE Mfano; 140/110mmHg pamoja na Uwepo wa Protein kwenye Mkojo yaani kitaalam kama PROTEINURIA

2️⃣ Mjamzito Kuona marue marue au kwa kitaalam huitwa "Blurr vission" pamoja na maumivu makali ya Kichwa,hasa hasa kwa Mbele au pembeni

3️⃣ Mjamzito kuongezeka uzito kwa kasi sana ndani ya Mda mfupi

4️⃣ Mjamzito kuvimba miguu kupita kiasi,mikono na Uso pia

5️⃣ Kupatwa na Degedege au hali ya kutingishwa kwa mwili kitaalam hujulikana kama "Seizures"

[MADHARA YA UGONJWA KIFAFA CHA MIMBA]

✓ kudondoka Gafla kwa Mjamzito na kupata madhara kama Majeraha ya mwili,Au Ujauzito kutoka

✓ Hatari ya Mama Mjamzito kujifungua kwa Upasuaji

✓ Mama mjamzito kupoteza maisha yake mwenyewe

✓ Mtoto aliyetumboni kupoteza maisha

🔴TIBA YA KIFAFA CHA MIMBA

Kuna tiba za awali endapo mama mjamzito akipata kifafa cha mimba kama zile za kudhibiti Presha au Shinikizo la Damu la mama Mjamzito,pamoja na zile za kuzuia hali ya degedege/kutingishwa kwa mwili au kitaalam "FITS"au "SEIZURES" ambazo huhusisha utoaji wa Dawa inayojulikana kama MAGNESSIUM SULPHATE. Lakini Tiba pekee ya Kifafa cha Mimba ni Mtoto azaliwe,Kwa njia yoyote ile hata Kwa Upasuaji.

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KWA MJAMZITO

(1) Zijue dalili zote za Hatari kipindi cha ujauzito mfano; kuvimba Miguu kupita kiasi,mikono na uso,kuona maruerue, kupatwa na hali ya kutingishwa,degedege au kwa kitaalam FITS,Ambapo hizi ni baadhi ya dalili za Kifafa cha mimba, Kuvuja damu wakati wa Ujauzito,Chupa ya uzazi kupasuka(Ruptured membrane) n.k

(2) Usafi wa mwili na mazingira ni muhim sana ili kutokurabisha baadhi ya magonjwa kama UTI,FANGASI,PID n.k.

(3) Kuzingatia lishe sahihi wakati wa Ujauzito ikiwemo swala nzima la Mlo kamili na kanuni zake zote.

(4) Mahudhurio ya Kliniki kwa Mama mjamzito ni muhimu sana kwani,ndyo Nguzo Imara ya Kupata Uzazi bora na Salama. Mfano: 

SOMA HAPA CHINI RATIBA ZA KLINIKI KWA MAMA MJAMZITO

(1) Hudhurio la Kwanza ni ujauzito ukiwa kabla ya wiki 16

(2) Hudhurio la Pili ni ujauzito ukiwa na wiki 20-24

(3) Hudhurio la Tatu ni Ujauzito ukiwa na wiki 28-32

(4) Na hudhurio la Nne ni ujauzito ukiwa na wiki 36-40

🔺 KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU NA TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584,PIGA SIMU AU TUMA UJUMBE MUDA WOWOTE UTAHUDUMIWA POPOTE ULIPO.

PART 2; 

Kifafa cha Mimba- hutokea palea ambapo mwanamke anakuwa na Presha Kubwa pamoja na Uwepo wa Protein kwenye Mkojo yaani kitaalam "Proteinuria"

Ugonjwa huu huwasumbua Wanawake wengi wakiwa Wajawazito na Hata baada tu ya kujifungua,hivo kupelekea maisha yao na viumbe walivyobeba tumboni kuwa katika hatari zaidi ya kupoteza Maisha.

DALILI ZA UGONJWA WA KIFAFA CHA MIMBA

(1) kiashiria cha Kwanza kabsa ni uwepo wa Protein kwenye Mkojo yaani "Proteinuria" pamoja na presha kubwa kwa Mama.

(2) Miguu kuvimba kupita Kiasi,Mikono pamoja na uso pia

(3) Kuona Marue na kizunguzungu pia

(4) Kichwa kuuma kupita kiasi

(5) Kusikia kichechefu na kutapika

(6) Maumivu makali ya tumbo na maumivu ya chini ya Mgongo chanzo kikiwa shida kutokea kwenye Ini

TIBA

Kuna dawa za kudhibiti hali hii,Japo tiba sahihi ya Kifafa cha Mimba kwa Mjamzito,Ni mtoto azaliwe tu,kwa Njia yoyote ile hata kwa Upasuaji ikiwezekana.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KUPITIA NAMBA +255758286584

Karibu Sana..!!



Post a Comment

0 Comments