Connect with us

Magonjwa

UGONJWA WA NGIRI(HERNIA) NINI?,CHANZO,DALILI ZAKE NA MATIBABU YAKE

Avatar photo

Published

on

UGONJWA WA NGIRI(HERNIA) NINI?,CHANZO,DALILI ZAKE NA MATIBABU YAKE

➡️ Ombeni Mkumbwa

Ngiri hujulikana pia kama “Hernia” kwa Kiingereza. Ugonjwa wa mshipa wa ngiri ni matokeo anayopata mtu kutokana na misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikilia au kubeba viungo fulani mwilini kupoteza uimara wake. Au kuta hizo kuwa na uwazi na kupelekea viungo hivyo kutoshikiliwa vizuri katika sehemu vinapostahili kuwepo.

CHANZO CHA UGONJWA WA NGIRI

?Tunaweza kuufahamu zaidi ugonjwa wa ngiri kama hali inayotokea katika mwili ambapo sehemu fulani ya nyama ya viungo mbalimbali vya mwili hujipenyeza kupitia sehemu iliyo dhaifu ya mwili na kutokeza upande wa pili. Sehemu inayoathiriwa mara nyingi ni maeneo ya tumbo, kokwa, pumbu na kadhalika ambapo baadhi ya viungo vya mwili vilivyomo tumboni hujipenyeza kupitia vitundu vinavopitisha mishipa ya fahamu inayohudumia kokwa (Spesmatic Cord), hivyo baada ya kujipenyeza huteremka hadi ndani ya korodani hali ambayo hukamilisha kuwepo kwa ugonjwa wa mshipa wa ngiri.

?MAENO AMBAYO HUATHIRIWA NA UGONJWA WA NGIRI

Sehemu ambazo Ngiri inaweza kutokea ni pamoja na maeneo ya: · Tumboni · Eneo la kinena · Eneo la paja kwa juu · Eneo ambalo mtu amewahi kufanyiwa upasuaji siku za nyuma · Kifuani n.k. Ugonjwa huu wa ngiri unawapata watu wa jinsia zote na wa umri wowote.

?AINA ZA NGIRI AU HERNIA

Aina za Ngiri: Ugonjwa wa mshipa wa ngiri unaweza kujitokeza maeneo mbalimbali ya mwili na aina ya ngiri hutegemea na sehemu ngiri ilipojitokeza. 

 

(1) Ngiri maji – Hii ni aina ya ngiri ijulikanayo pia kwa kitaalamu kama (hydrocele) 

 

(2)Ngiri kavu (Hernia) – hujulikana pia kama ‘fermoral hernia’ kwa wanawake na huitwa ‘scrotal hernia’ kwa wanaume

 

(3) Ngiri ya kwenye kifua – hujulikana pia kitaalamu kama ‘hiatus hernia

 

(4) Ngiri ya tumbo – hujulikana pia kama ‘Abdominal Hernia

 

(5) Ngiri ya kwenye kitovu – hujulikana pia kama ‘Umbilical Hernia”

 

(6) Ngiri ya sehemu ya haja kubwa – hujulikana pia kama ‘Anal Hernia’

 

?DALILI ZA UGONJWA WA NGIRI-HERNIA

 

Dalili za aina zote za ngiri hazitofautiani sana na ngiri hujitokeza bila maumivu yoyote ingawa kuna baadhi ya ngili hua na maumivu makali hutegemea ngiri ilivotokeza.

Ngiri ya kwenye kinena ni ngiri ambayo kitaalamu huitwa inguinal hernia hutokea wakati tishu laini hujitokeza kupitia eneo la udhaifu au kasoro katika misuli yako ya chini ya tumbo. Mara nyingi huwa karibu na eneo la kinena. Mtu yeyote anaweza kupata henia hii, lakini ni kawaida zaidi kwa wanaume kuliko wanawake.

Upasuaji sio lazima kila wakati, lakini henia kwa ujumla henia inasumbua sana bila hiyo. Katika baadhi ya matukio, henia isiyotibiwa inaweza kuwa hatari ya kutishia maisha. Ingawa kuna madhara na hatari zinazohusiana na upasuaji, watu wengi wana matokeo mazuri.

Nini husababisha ngiri ya kinenani? Sababu ya ngiri ya kinenani haijulikani, lakini inaweza kuwa ni matokeo ya maeneo dhaifu katika ukuta wa tumbo. Ulegevu unaweza kuwa kutokana na kasoro zilizopo wakati wa kuzaliwa au mwili kuingiliwa na sumu baadaye katika maisha. Baadhi ya sababu za hatari kwa henia ya kinenani ni pamoja na: · Maji au shinikizo katika tumbo · Kuinua vitu vizito, kama vile weightlifting · Kufunga choo (kusukuma choo kwa nguvu nyingi wakati wa kujisaidia haja kubwa · Kikohozi cha muda mrefu au Mimba

Watu wazima na watoto wanaweza kupata henia ya kinenani. Wanaume wana uwezekano mkubwa zaidi wa kupata henia ya kinenani. Watu wenye historia ya ngiri wanakuwa katika hatari kubwa zaidi ya kuwa ngiri nyingine pia. Ngiri ya pili hutokea kwa upande mwingine.

➖ Je! ni zipi dalili za henia ya kinena? Dalili za ngiri ya kwenye kinena zinajumuisha 

  maumivu au, shinikizo, hasa wakati wa kuinua kitu, au kukohoa. Dalili hizi kawaida hupungua wakati wa kupumzika. Wanaume pia wanaweza kuwa na uvimbe katika eneo la ngiri.

 Huwezi kutambua dalili yoyote ikiwa hernia yako ya ngumu na ndogo.

 

MATIBABU YA UGONJWA WA HERNIA

 

Je, unahitaji upasuaji? Kwa kawaida upasuaji haupendekezwi kama henia haijasababisha tatizo. Hata hivyo, ni muhimu kutambua kwamba wangonjwa wengi hutibiwa kwa upasuaji, wachache sana hupona kwa dawa. 

Daktari wako anaweza kupendekeza upasuaji kama: · hernia yako inakuwa kubwa · maumivu yanaendelea au ongezeko · una shida kufanya shughuli za kila siku n.k

Hernia inaweza kuwa hatari sana ikiwa  sehemu ya utumbo wako umetoka au kupigwa. Ikiwa hii itatokea, unaweza kuwa na: · 

  • Homa 
  •  Kiwango cha mapigo ya moyo kilichoongezeka
  • Maumivu 
  • Kichefuchefu 
  •  Kutapika 
  •  Uvimbe
  •  kuona giza ? Ikiwa una dalili hizi au  yoyote kati ya hizi wasiliana na daktari wako mara moja. Hii ni hali inayohatarisha maisha inayohitaji upasuaji wa dharura. 

 

  • ?Je, ngiri huathiri nguvu za kiume? Kama ngiri bado ni ndogo. Haiwezi kuathiri chochote katika nguvu za kiume. Hata hivyo, henia ambayo imeshakuwa kubwa inaweza kuathiri nguvu za kiume – – huathiri kazi ya utaratibu na hali ya homoni. Ukosefu wa testosterone ya homoni inaweza kusababisha upungufu wa nguvu za kiume. Upasuaji wa ngiri unaweza kusababisha shida katika korodani kufanya uwezekano wa homoni ya testosterone kuwa chini. Hata hivyo, kwa sababu watu wengi wana korodani mbili, hata kama moja inaweza kuwa na shida, nyingine inaweza kuzalisha viwango vya kutosha vya homoni. Ngiri pia huweza kusababisha upungufu wa nguvu za kiume kutokana na kuharibu mishipa ya neva iliyo kwenye uume.

Kumbuka; Yapo MATIBABU ya kutumia  dawa za asili na mbadala za kutibu matatizo ya ngiri aina zote bila kupasua. Lakini changamoto yake nikupata tiba sahihi,maana sio kila dawa za asili hutibu ugonjwa huu wa Ngiri.

 

Yaliyomo;

 

(1) Utangulizi-Maana ya Ugonjwa wa Ngiri (hernia)

(2) Aina za Ngiri au kitaalam hernia

(3) chanzo cha Ugonjwa ngiri

(4) Dalili za Ugonjwa wa Ngiri

 (5) Tiba ya Ugonjwa wa Ngiri

KWA USHAURI ZAIDI/ELIMU/TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584

Karibu Sana..!!

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In https://afyaclass.com Also Follow us on Instagram @afyaclass

YOU MUST READ(IMPORTANT)

Magonjwa2 months ago

Maumivu chini ya kitovu ni dalili za ugonjwa gani

Maumivu chini ya kitovu ni dalili za ugonjwa gani. Watu wengi huweza kupata maumivu chini ya kitovu, lakini umewahi kujiuliza...

Magonjwa3 months ago

Kaswende ni ugonjwa gani, soma hapa kufahamu

Kaswende ni ugonjwa gani, Kaswende ni maambukizi yanayosababishwa na bakteria. Mara nyingi, huenea kupitia mawasiliano ya kingono au kwa kujamiiana....

Magonjwa3 months ago

Koo kukauka ni dalili ya ugonjwa gani

Koo kukauka ni dalili ya ugonjwa gani Koo kukauka kunaweza kusababishwa na sababu kadhaa, ikiwa ni pamoja na: Upungufu wa...

Magonjwa3 months ago

Amiba ni ugonjwa gani,Fahamu kuhusu Ugonjwa wa Amebiasis

Amiba ni ugonjwa gani Wengi wamezoea kusema hivo ila Amiba(amoeba) ni vimelea vyinavyosababisha ugonjwa, na Ugonjwa huo kitaalam ndyo hujulikana...

Magonjwa5 months ago

kuwashwa nyayo za miguu husababishwa na nini? chanzo na Tiba

kuwashwa nyayo za miguu husababishwa na nini? chanzo na Tiba kuwashwa nyayo za miguu; zipo sababu nyingi ambazo huchangia shida...

magonjwa ya wanawake5 months ago

Ujue Ugonjwa Wa PID (Pelvic Inflammatory Disease)

Ujue Ugonjwa Wa PID (Pelvic Inflammatory Disease) Pid ni ugonjwa gani? PID ni Maambukizi ya bacteria Kwenye Via vya Uzazi...

Magonjwa2 years ago

SHINGO YA MTOTO KULEGEA(CHANZO CHAKE)

SHINGO YA MTOTO KULEGEA(CHANZO CHAKE) Mabadiliko ya Watoto wengi huanza kwenye miezi mitatu ya Mwanzo wakati ambapo Shingo ya mtoto...

Magonjwa3 years ago

MAUMIVU MAKALI SEHEMU YA HAJA KUBWA

Baadhi ya watu wanachanganya tatizo la maumivu makali sehemu ya haja kubwa pamoja na tatizo la Bawasiri,japo mojawapo ya chanzo...

Magonjwa3 years ago

TATIZO LA MASIKIO KUPIGA KELELE,CHANZO NA TIBA YAKE(Tinnitus)

TATIZO LA MASIKIO KUPIGA KELELE,CHANZO NA TIBA YAKE(Tinnitus) tatizo la masikio kupiga kelele Tinnitus, ni Tatizo la masikio kupiga kelele,...

Magonjwa3 years ago

DALILI ZA UGONJWA WA GONO(KISONONO)

 UGONJWA WA KISONONO DALILI ZA UGONJWA WA GONO(KISONONO) Ugonjwa wa gonorrhea maarufu kama GONO au Kisonono ni ugonjwa wa zinaa...

Magonjwa3 years ago

TATIZO LA UKE KUJAMBA PAMOJA NA TIBA YAKE(chanzo cha tatizo hili ni nini?)

Tatizo la Uke Kujamba TATIZO LA UKE KUJAMBA PAMOJA NA TIBA YAKE(chanzo cha tatizo hili ni nini?) Moja ya vitu...

Magonjwa3 years ago

DALILI ZA FANGASI UUMENI,KORODANI PAMOJA NA MATIBABU YAKE

 FANGASI • • • • • DALILI ZA FANGASI UUMENI,KORODANI PAMOJA NA MATIBABU YAKE Mashambulizi ya Fangasi sehemu za siri...

Magonjwa3 years ago

CHANZO CHA TATIZO LA KUOTA NYAMA PUANI PAMOJA NA MATIBABU YAKE

Chanzo cha tatizo la NYAMA PUANI,Dalili zake Pamoja na Tiba yake, Soma makala hii kwa Makini ili upate Kujua kuhusu...

Magonjwa3 years ago

SABABU ZA KUVIMBA KWA MASHAVU YA UKE(TEZI LA BARTHOLIN)

KUVIMBA MASHAVU YA UKE • • • • • • Katika Makala hii tumechambua zaidi kuhusu sababu za kuvimba mashavu...

Magonjwa4 years ago

TATIZO LA MWANAUME KUOTA MATITI(gynecomastia)

TATIZO LA MWANAUME KUOTA MATITI(gynecomastia) Tatizo hili linatokea kwa Baadhi ya wanaume,na hata kupelekea Wanaume hao kuwa na Matiti kama...

MAGONJWA MBALI MBALI

Magonjwa1 day ago

Dalili za infection kwenye damu,mchafuko wa damu

Dalili za infection kwenye damu Mchafuko wa damu,chanzo,dalili na Tiba Mchafuko wa damu; hiki ni kiswahili ambacho watu wamezoea kukitumia...

Magonjwa4 days ago

Ugonjwa wa ngozi sehemu za siri

Ugonjwa wa ngozi sehemu za siri Yapo magonjwa mbali mbali ya ngozi ambayo huweza kuathiri Sehemu za Siri za Mwanaume...

Magonjwa1 week ago

Dalili za acid reflux,Soma hapa Kufahamu

Dalili za acid reflux: Tatizo la Gastroesophageal reflux disease (GERD), ni tatizo ambalo huwapata Watu wengi,Tatizo hili hujulikana kwa jina...

Magonjwa3 weeks ago

Ugonjwa wa ngozi kuwa nyeupe,VITILIGO

Ugonjwa wa ngozi kuwa nyeupe,VITILIGO Vitiligo ni ugonjwa wa ngozi kuwa nyeupe au ni ugonjwa ambao huhusisha ngozi kupoteza rangi...

Magonjwa4 weeks ago

Mlipuko wa ugonjwa wa macho,Macho Mekundu

Mlipuko wa ugonjwa wa macho,Macho Mekundu Baada ya Ugonjwa huu wa macho kusumbua watu wengi kwa kipindi cha Hivi Karibuni,...

Magonjwa4 weeks ago

Scabies ni ugonjwa gani? Soma hapa kufahamu

Scabies ni ugonjwa gani? Soma hapa kufahamu Utangulizi: Scabies huhusisha mtu kuwa na vipele na muwasho kwenye ngozi yake ambapo...

Magonjwa1 month ago

Dalili za ugonjwa wa gono kwa mwanaume

Dalili za ugonjwa wa gono kwa mwanaume Gono ni neno maarufu ambalo kirefu chake ni Gonorrhea na kiswahili chake ni...

Magonjwa1 month ago

Dalili Mpya za ukimwi kwenye ngozi

Zipi ni Dalili za ukimwi kwenye ngozi Zipi ni dalili za Ukimwi kwenye ngozi ya mtu? Fahamu hapa kupitia makala...

Magonjwa1 month ago

Madhara ya COVID-19: Athari za Ugonjwa, Asili na Matibabu

Madhara ya COVID-19: Athari za Ugonjwa, Asili na Matibabu Huu ni ugonjwa wa kuambukiza uliosababishwa na kirusi cha corona, ambao...

Magonjwa1 month ago

Ishara za Maambukizi ya Njia ya Mkojo (UTI) kwa Wanaume na Wanawake

Ishara za Maambukizi ya Njia ya Mkojo (UTI) kwa Wanaume na Wanawake Karibu! Hapa kwa makala yenye taarifa muhimu kuhusu...

Trending