Ticker

6/recent/ticker-posts

UGONJWA WA PRESHA AU SHINIKIZO LA DAMU



  UGONJWA WA PRESHA YA KUPANDA AU SHINIKIZO LA DAMU,CHANZO,DALILI,TIBA

➡️ Web

Shinikizo la juu la damu (HTN) au presha ya juu ya damu (pia huitwa shinikizo la mishipa ya damu, HBP), ni ugonjwa sugu ambapo nguvu ya msukumo wa damu katika mishipa ni kubwa kuliko kawaida. Ongezeko hilo husababisha moyo kufanya kazi kupita kiasi ili uzungushe damu katika mishipa ya damu. Kwa kawaida halina dalili, ila likidumu lina madhara makubwa kwa afya.

Shinikizo la juu la damu ndilo sababu kubwa (kihatarishi) ya upoozaji, mshtuko wa moyo (mashambulizi ya moyo), moyo kushindwa kufanya kazi, kutuna kwa ukuta wa mishipa (k.m., kutuna kwa ukuta wa aota au mkole), chujio la mshipa wa kupeleka damu kwenye moyo au peripheral arterial disease, na inasababishwa na ugonjwa sugu wa figo. Hata ongezeko la wastani la shinikizo la damu hupunguza matarajio ya muda wa kuishi.

 
vipimo viwili vya shinikizo la damu, yaani systolic na diastolic: shinikizo au presha ya systolic ni kipimo cha damu ambacho kinapima nguvu ya msukumo wa damu katika mishipa ya damu wakati moyo unadunda. Shinikizo au presha ya diastole inapima nguvu ya msukumo wa damu katika mishipa ya damu wakati moyo umetulia au kati ya mapigo ya moyo (diastole).

Kipimo cha kawaida cha shinikizo la damu ni 100–140 milimita za zebaki (mmHg) upande wa systolic (kipimo cha juu) na 60–90  milimita za zebaki upande wa diastolic (kipimo cha chini). Shinikizo la juu la damu hutokea kama kipimo kikiwa zaidi ya 140/90 mmHg kwa muda mrefu.

Kuna aina mbili za shinikizo la juu la damu: shinikizo la juu la damu la asili na shinikizo la damu linalosababishwa na magonjwa mengine. Kadiri ya asilimia 90–95 za watu wanaathiriwa na "shinikizo la juu la damu la asili", yaani wana ugonjwa huu bila kuwa na chanzo cha kisayansi kinachofahamika.Magonjwa mengine ya mafigo, mishipa, moyo, mfumo wa homoni huathiri asilimia 5–10 iliyobaki ya watu wenye shinikizo la damu (ndilo shinikizo la damu linalosababishwa na magonjwa mengine).

Ili kudhibiti shinikizo la damu, lishe bora na mabadiliko katika mtindo wa kuishi lazima yazingatiwe pamoja na kupunguza matatizo yanayoathiri afya. Hata hivyo, matumizi ya dawa ni muhimu kwa watu ambao mabadiliko ya mtindo wa maisha hautoshelezi kupunguza shinikizo la juu la damu, kutuna kwa ukuta wa ateri mithili ya puto kutokana na udhaifu wa sehemu hiyo.

🔺Watu wazima

➖ Kwa watu wenye umri wa miaka 18 au zaidi, shinikizo la juu la damu linaweza kuwa systolic na/au diastolic kama kipimo hicho ni zaidi kuliko kipimo cha kawaida kinachokubalika ambacho ni (139 mmHg systolic, 89 mmHg diastolic: Kama vipimo vinapatikana baada ya kutumia chombo kinachopima presha kwa masaa 24 (24-hour ambulatory) au kufanya maangalizi nyumbani, vipimo vya chini vinatumiwa (135 mmHg systolic or 85 mmHg diastolic). 

➖ Pia miongozo ya kimataifa ya hivi karibuni imegawanya shinikizo la damu katika vikundi mbali mbali vyenye vipimo chini ya kipimo cha shinikizo la juu la damu ili kuthibitisha hatari iliyopo ya shinikizo la juu la damu. Wanatumia neno dalili ya kuwa na shinikizo la juu la kwa presha ya damu iliyo kati ya 120 na 139 mmHg systolic na/au 80–89 mmHg diastolic, 

➖ wakati Miongozo ya ESH-ESC (2007) and BHS IV (2004) inatenganisha katika vikundi vya hali inayofaa, vya kawaida, na vya kawaida kiasi kutofautisha presha zilizopo chini ya 140 mmHg systolic na 90 mmHg diastolic. Shinikizo la juu la damu pia imegawanywa katika vikundi vifuatavyo: 

➖ JNC7 inatofautisha shinikizo la juu la damu aina ya I, shinikizo la juu la damu aina ya II, na shinikizo la juu la damu hatua kali sana. Shinikizo la juu la damu ambayo ni kali sana (Isolated systolic hypertension) ni presha ya juu sana inayoambatana na presha ya kawaida ya diastolic, hali hii huwatokea sana wazee.

➖ The ESH-ESC Guidelines (2007) and BHS IV (2004) inatambua aina ya tatu (aina ya III) ya shinikizo la juu la damu kwa watu ambao wana presha ya juu ya systolic inayozidi 179 mmHg au presha ya diastolic inayozidi 109 mmHg. Shinikizo la juu la damu liko katika kundi la "sugu" kama madawa hayapunguzi shinikizo la damu hadi vipimo vya kawaida.

🔺Watoto wadogo na wachanga

Si kawaida kwa watoto waliozaliwa karibuni kuwa na shinikizo la juu la damu na ni asilimia 0.2 hadi 3% ya watoto wachanga ambao wanapata. Shinikizo la damu haipimwi mara kwa mara kama watoto ni wadogo na wana afya nzuri. Shinikizo la damu huwapata watoto ambao wako katika hatari kubwa. Kuna masuala tofauti ya kuangalia, kama vile kipindi cha ujazito, umri baada ya utungaji mimba, na uzito wakati wa kuzaliwa kabla ya kuamua kama kipimo cha shinikizo la damu ni cha kawaida kwa mtoto mchanga.

🔺Watoto na vijana

Ni kawaida kwa watoto na vijana kupata shinikizo la damu (asilimia 2–9% hutegemea na umri, jinsia, na asili) and is associated with long-term risks of ill-health. Hivi sasa kuna pendekezo la kuwapima damu watoto wenye zaidi ya miaka mitatu na kuangalia kama wana shinikizo la juu la damu kila wanapoenda kupimwa afya yao.

 Kabla ya kuthibitisha kama mtoto ana shinikizo la juu la damu mtoto lazima apimwe mara kadhaa. Shinikizo la damu huongezeka utotoni kufuatana na umri , wa watoto, shinikizo la damu linatambulika kama ni systolic ya kawaida au diastolic baada ya kupimwa zaidi ya mara tatu au zaidi ya asilimia 95 ambayo ni kawaida kufuatana na jinsia, umri na urefu wa mtoto. Dalili ya shinikizo la juu la damu (Prehypertension) kwa watoto linatambulika kama shinikizo au presha ya kawaida ya systolic au shinikizo au presha ya diastolic kama ni zaidi au sawa na asilimia 90, lakini ni chini ya asilimia 95. Kwa vijana, inapendekezwa kwamba shinikizo la juu la damu na dalili ya shinikizo la juu la damu zichunguzwe na kuainisha kwa kutumia vigezo vya watu wazima.

📶 Ishara na dalili

Mara nyingi watu wenye shinikizo la damu hawana dalili yoyote, na huwa inagundulika baada ya kufanya uchunguzi kwa kawaida kupitia screening, au wakati maangalizi ya afya yanafanywa kwa sababu nyingine. Watu wengine wenye shinikizo la damu huwa wanapata maumivu ya kichwa (haswa nyuma ya kichwa na asubuhi), pamoja na kuchanganyikiwa, kizunguzungu, sikio kelele (mvumo au mazomeo masikioni), kutoweza kuona vizuri au matukio ya kuzirai.

Baada ya uchunguzi wa mwili, kunakuwa na wasiwasi wa shinikizo la juu la damu kama kuna upanuzi wa mishipa ya damu ya retina baada ya kufanya uchunguzi wa optic fundus iliyopo nyuma ya jicho kwa kutumia chombo cha kufanyia uchunguzi yaani ophthalmoscopy. Classically, ukali wa mabadiliko ya shinikizo la damu ya retina linagawanya kwenye vikundi kuanzia I hadi IV, ingawa inaweza kuwa vigumu kuzitofautisha aina kali kiasi. Chombo cha kufanyia uchunguzi wa macho kinaweza kuonyesha muda ambao mtu amekuwa na shinikizo la juu la damu=Fisher2005/>

Shinikizo la juu la damu litokanalo na magonjwa mengine
Dalili zingine zinaweza kusababishwa na magonjwa mengine, yani shinikizo la damu linaloletwa na sababu zingine zinazojulikana kama vile magonjwa ya figo au mabadiliko ya mfumo wa homoni. Kwa mfano, unene wa kifua na tumbo, uthibiti mbaya wa sukari, moon facies au mkusanyiko wa mafuta usoni, mkusanyiko wa mafuta mgongoni ("buffalo hump") na purple striae au alama za unene huonyesha dalili ya ugonjwa wa homoni wa Cushing's syndrome.

Ugonjwa unaoathiri kikoromeo na acromegaly yaani mwili hutengeneza homoni ya kukuza umbo pia huweza kuleta shinikizo la juu la damu na dalili zake za kawaida huonekana. Wembamba wa mishipa ya tumbo au abdominal bruit inaweza kuwa ni ishara ya renal artery stenosis au kuziba kwa mishipa ya damu ipelekayo damu kwenye figo.

 Shinikizo la chini la damu katika miguu au mapigo ya mshipa wa mguu yanayochelewa au ukosefu wa mapigo mapigo ya mshipa wa mguu inaweza kuwa ni dalili ya aortic coarctation (kupungua kwa upana wa mshipa mkuu utoao damu kwenye moyo kwenda mwilini). Shinikizo la damu ambalo linalotofautiana sana na kuumwa kwa kichwa, mpapatiko wa moyo, kubadilika rangi ya ngozi, na utoaji jasho ni lazima kuwe na wasiwasi wa pheochromocytoma yaani saratani ya tezi iliyo juu ya figo.

Hali ya hatari ya shinikizo la juu la damu
Shinikizo la damu lililo juu kupita kiasi (sawa au zaidi ya 180 au diastolic ya 110, wakati mwingine huitwa shinikizo la damu linaloweza kuleta kifo au linaloharakisha kifo) inatambulika kama "hali ya hatari ya shinikizo la juu la damu." 

Shinikizo la damu vinavyozidi vipimo hivi vinaonyesha hali kubwa ya hatari ya ugonjwa huu. Watu wenye viwango hivi vya shinikizo la damu wanaweza wasiwe na dalili zozote, ila wanaweza kulalamika kuumwa kwa kichwa (asilimia 22% ya wagonjwa) na kuwa na kizunguzungu kuliko watu wa kawaida. Dalili zingine za hali ya hatari ya shinikizo la damu ni kutoona vizuri au kutopumua vizuri kwa sababu moyo haufanyi kazi vizuri au kutojisikia vizuri uchovu kwa sababu mafigo yanashindwa kufanya kazi. Watu wengi wenye hali ya hatari ya shinikizo la damu wanatambulika kuwa na msukumo mkubwa wa damu, lakini vichocheo vingine vinaweza kuongezea msukumo.

"Shinikizo la damu la ghafla", zamani ilikuwa inajulikana kama "shinikizo la damu inayodhuru", hutokea ikiwa kuna ithibati ya madhara yanayotokea katika ogani za mwili kwa sababu ya shinikizo la juu la damu. Madhara haya yanaweza kuwa hypertensive encephalopathy au shinikizo kichwani, inasababishwa na uvimbe wa ubongo na kutofanya kazi vizuri, na husababisha kichwa kuumwa na kupoteza fahamu (kuchanganyikiwa au kusinzia). 

Retinal papilloedema and fundal kuvuja damu kutokana na mpasuko wa mishipa midogo ya macho na kutoa usaha au maji ni dalili nyingine ya madhara ya ogani. Maumivu ya kifua yanaweza kuwa ni dalili ya uharibifu wa misuli ya moyo (ambayo baadaye yanaleta upungufu wa damu kati ya misuli ya moyo) au wakati mwingine ukuta wa ndani wa aorta huchanika na damu, kuchanika kwa ukuta wa mshipa mkuu uitwao aota/mkole. 

Kukosa pumzi, kukohoa, na kukohoa makohozi yenye damu ni dalili ya pulmonary edema au mapafu kujaa maji. Hali hii inaleta uvimbe wa seli za mapafu unaosababishwa na udhaifu wa upande wa kushoto wa moyo, na uwezo mdogo wa upande wa kushoto wa moyo kusukuma damu kutoka kwenye mapafu hadi mishipa ya damu. Figo kupoteza uwezo wake wa kufanya kazi upesi (figo kushindwa kufanya kazi kwa ghafla) na microangiopathic hemolytic anemia au upungufu wa damu (uharibifu wa seli za damu) unaweza kutokea.

 Katika hali hizi, shinikizo la chini la damu ni muhimu ili kupunguza madhara ya ogani. Kwa upande mwingine, hakuna ushahidi unaonyesha kuwa shinikizo la damu linatakiwa kupunguzwa kwa kasi wakati wa matatizo ya dharura ya shinikizo la juu la damu iwapo kuna ogani iliyoathirika. Upunguzaji wa ghafla wa shinikizo la damu unaweza kuwa ni hatari. Matumizi ya dawa ya kushusha shinikizo la damu hatua kwa hatua zaidi ya masaa 24 hadi 48 yanapendekezwa wakati wa dharura inayotokana na shinikizo la juu la damu.

➖Ujauzito

Shinikizo juu la damu hutokea takriban 8-10% za ujauzito. Wanawake karibu wote wenye shinikizo juu la damu wakiwa na mimba walikwishaumwa na shinikizio la damu la kawaida. Hali hiyo ikitokea katika ujaa uzito ni dalili ya kwanza ya kifafa cha mimba kabla hakijashikika kabisa. Maradhi hayo hutokea katika muda wa pili wa ujaa uzito na majuma machache baada ya kujifungua. 

Uaguzi wa maradhi hayo ni pamoja na shinikizo la damu kuongezeka na dalili za protini ndani ya mkojo. Maradhi hayo hutokea takribin 5% ya ujaa uzito yakisababisha takribin 16% ya vifo vya wenye ujaa uzito. Hatari ya kifo cha mtoto inaongezeka maradufu kutokana na maradhi hayo dunia nzima. Kwa kawaida hakuna dalili maalum za kifafa cha mimba kabla hakijashikika kabisa hugunduliwa na uchujaji wa kawaida. Zinapotokea dalili za maradhi hayo hizo ndizo ni kuumwa kichwani, taabu za kuona vizuri (mwanga wa kumulika ghafla) kutapika, maumivu ya epigastriumu na kuvimba.

 Kifafaa cha mimba kabla hakijashikika kabisa wakati mwingine inaweza kuletea hali inayotisha maisha inayoitwa kifafa cha mimba. Kifafa cha mimba kinaleta hali ya dharura ya shinikizo la damu inayotatiza sana. Matatizo hayo ni pamoja na upofu, kuvimba kwa ubongo, utendaji wa kiklonasi ulio katika hali ya kukazika au kuvutika na kutia kifafa, kuharibika kwa mafigo, edema ya mapafu, disseminated intravascular coagulation (kutoganda vizuri kwa damu).

Watoto wadogo na wachanga

Kushindwa kustawi, kutiliwa kifafa, usumbufu, uchovu/kukosa nguvu, hali inayorudiarudia ya kudhikisha kwa mapofu kushindwa kuhema vizuri. Kuhusu watoto wachanga ambao wameshahitimu umri zaidi pamoja na wana, shinikizo la juu la damu linaweza kuumiza kichwa, usumbufu usioelezeka, uchovu (uchovu wa kiganga), kushindwa kustawi, macho kutiliwa kiwi, kutokwa na damu puani, hatimaye kiharusi uso kupoozwa baadaye.

Kuzidi kwa ukali wa shinikizo la juu la damu
Shinikizo la juu la damu linachangia vifo vya watoto wachanga kuliko athari nyingine, nalo linaweza kupatiwa kinga.


Shinikizo la juu la damu la hatua ya pili
Shinikizo la juu la damu la hatua ya pili linatokana na chanzo kinachojulikana. Maradhi ya mafigo ni chanzo kinachozidi cha shinikizo la juu la damu hatua ya pili.Chanzo kingine cha shinikizo la juu la damu ni hali tofauti za tezi zenye kunyesa ndani kwa ndani kama kwa mfano Cushing's syndrome, hyperthyroidism, hypothyroidism, acromegaly, Conn's syndrome or hyperaldosteronism, hyperparathyroidism, and pheochromocytoma. Vyanzo vingine vya shinikizo la juu la damu hatua ya pili ni pamoja na [unene], [kushindwa kupumua kunakoleta usingizi wa mang’amung’amu], [kuwa na mimba], [kufinyika kwa aota], ulaji zaidi wa [urukususu] na dawa fulani zilizo halali zikiwa na zile zote zisizo halali pamoja na dawa za kienyeji.

KWA USHAURI ZAIDI/ELIMU/TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584






Post a Comment

0 Comments