Connect with us

Magonjwa

UGONJWA WA TEZI DUME(SARATANI YA TEZI DUME),CHANZO,DALILI,VIPIMO NA TIBA YAKE

Avatar photo

Published

on

  UGONJWA WA TEZI DUME(SARATANI YA TEZI DUME),CHANZO,DALILI,VIPIMO NA TIBA YAKE

➡️ Ombeni Mkumbwa

Moja ya matatizo yanayoathiri aina ya Tezi linalojulikana kama tezi dume ni saratani ya tezi dume. Saratani ya tezi dume huchukua nafasi ya tatu katika kusababisha vifo kwa wanaume wenye umri mbalimbali duniani. Lakini pia Ugonjwa huu ni chanzo kikubwa cha vifo kwa wanaume wenye umri wa miaka 70 na kuendelea. Hata hivyo, ni nadra sana kwa saratani ya Tezi Dume kuwapata wanaume chini ya miaka 40.

? WATU AMBAO WAPO KWENYE HATARI YA KUPATA SARATANI YA TEZI DUME

Kundi la watu ambao wapo kwenye hatari kubwa ya kupata Ugonjwa huu wa Saratani ya Tezi Dume;
  1. Wanaume ambao asili yao ni Afrika wana uwezekano mkubwa wa kupata ugonjwa wa Saratani ya tezi Dume ikilinganishwa na wazungu
  2. Wanaume wenye umri wa kuanzia miaka 60 na kuendelea
  3. Wanaume ambao wana historia ya tatizo la Saratani ya Tezi Dume katika familia zao, Mfano, wale ambao mmoja wa ndugu zake (kaka au mdogo wa kiume) au baba amewahi kuugua ugonjwa huu.
  4. Wanaume walevi au wanaokunywa pombe kupindukia
  5. Wanaume Wanaofanya kazi kwenye viwanda mbali mbali hasa vya kutengeneza rangi au wanaofanya kazi ya kupaka rangi
  6. Wanaume ambao ni Wakulima wanaotumia aina fulani ya mbolea zenye kemikali
  7. Wanaume Wanaofanya kazi katika viwanda vya utengenezaji matairi
  8. Wanaume wanaofanya kazi ya kuchimba madini hususani aina ya cadmium
  9. Wanaume wanaokula chakula chenye kiasi kikubwa cha mafuta hasa ya wanyama

?DALILI ZA UGONJWA WA SARATANI YA TEZI DUME

-Tafiti zinaonyesha kwamba saratani ya Tezi Dume ikiwa katika stage au hatua za mwanzoni, dalili zake hazitofautiani sana na zile za kuvimba kwa tezi dume (BPH). Dalili hizo ni pamoja na;

  • Mwanaume Kupata maumivu au kuteseka wakati wa kukojoa
  • Mwanaume kupatwa na hali ya kutiririka kwa mkojo baada ya kumaliza kukojoa
  • Mwanaume kukojoa mkojo wenye mtiririko dhaifu
  • Mwanaume kukojoa mara kwa mara hasa nyakati za usiku
  • Mwanaume kujikakamua wakati wa kukojoa na kushindwa kumaliza mkojo wote
  • Mwanaume kutoa mkojo uliochanganyika na damu
  • Mwanaume kutoa mbegu za kiume( shahawa) zilizochanganyika na damu

Endapo Ugonjwa huu wa Saratani ya Tezi dume umesambaa kwa kiasi kikubwa,Mgonjwa ataonyesha dalili zifuatazo;

➖ Mwanaume kupata Maumivu makali ya mifupa katika maeneo ya nyonga, mapajani na kiunoni

➖ Hali ya Uume kushindwa kusimama (uhanithi)

➖ Pia mwanaume mwenye tatizo la Saratani ya Tezi dume huweza kupata dalili Za jumla kama vile;uzito, kuhisi kichefuchefu, uchovu, kizunguzungu n.k

? VIPIMO CHA TATIZO LA TEZI DUME

Ili kuweza kutambua tatizo la saratani ya tezi dume kuna mambo mbali mbali hufanyika kama vile;

* Kutaka kujua historia ya magonjwa mbali mbali katika familia husika,ikiwemo historia ya tatizo hili la Saratani ya Tezi Dume

*kutaka kufahamu kuhusu dalili mbali mbali anazopata Mgonjwa au zinazojionyesha kwa Mgonjwa

*Ufanyaji wa Vipimo mbali mbali kama vile;

  • Digital rectal exam: Hapa mtaalam wa afya au Daktari ataingiza kidole cha shahada katika puru (rectum) ili kuhisi tezi dume kupitia ukuta wa puru. Aidha atahisi pia sehemu zote zinazozunguka tezi dume kutambua iwapo tezi ni ngumu au kama ina uvimbe wowote.
  • Kuna kipimo cha damu kuchunguza Prostate Specific Antigen (PSA): PSA ni aina ya protein inayozalishwa na seli za tezi dume. Uzalishaji wake huongezeka wakati wa BPH, tezi dume inapopata uambukizi (prostitis) , na saratani ya tezi dume.
  • DRE pamoja na PSA huonesha uwepo wa tatizo kwenye tezi dume lakini vipimo hivi havina uwezo wa kutofautisha iwapo tatizo hilo linamaanisha saratani au BPH. Hivyo basi, ili kuweza kutofautisha kati ya magonjwa hayo mawili, kipimo kiitwacho Prostate biopsy hufanywa.
  • Prostate biopsy: Kipimo hiki hufanywa kwa kuchukua kipande cha nyama (tishu) kutoka tezi dume kwa ajili ya uchunguzi maabara.
  • Kipimo kingine huitwa transrectal ultrasound ambacho husaidia kuonesha ukubwa na sura ya tezi dume lilivyo.


☑️ MATIBABU YA SARATANI YA TEZI DUME

Matibabu ya Ugonjwa wa Saratani ya Tezi Dume ni pamoja na;

– Mgonjwa kufanyiwa upasuaji na tiba ya mionzi,

-Lakini kwa wagonjwa wazee, kuendelea kufatiliwa kwa ukaribu zaidi pasipo kufanyiwa upasuaji au tiba yoyote inayohisu mionzi.

-Endapo saratani imesambaa kwa kiasi kikubwa na kuathiri sehemu nyingine za mwili, matibabu yake yanaweza kujumuisha upasuaji wa kuondoa korodani, matumizi ya dawa za kupunguza kiwango cha homoni ya testosterone katika damu (hormonal therapy), au matumizi ya kemikali za kuua seli za saratani (chemotherapy).

– Tiba ya miozi huweza kutumika Kwa wagonjwa walio katika hatua ya mwisho ya saratani yaani wale ambao saratani tayari imeshasambaa mwilini ili kupunguza maumivu makali ya mifupa.

? Lakini Madhara ya tiba hii ya mionzi ni pamoja na mwanaume kushindwa kusimamisha uume au uhanithi, kukosa hamu ya kula, uchovu, ngozi kubabuka, kuharisha na kutoa mkojo uliochanganyika na damu.

– Matibabu yanayohusu homoni

Aina hii ya tiba inahusu matumizi ya dawa zinazopunguza kiwango au ufanyakazi wa homoni ya testosterone mwilini. Testosterone ni homoni ya kiume inayochochea ukuaji wa tezi dume, hivyo basi matumizi ya dawa hizi husaidia kupunguza ukuaji pamoja na kusambaa kwa seli za saratani.

? Lakini pia,Madhara yanayoweza kusababishwa na matumizi ya dawa hizi ni pamoja na kichefuchefu na kutapika, upungufu wa damu, kuongezeka uzito, uhanithi na kukosa hamu ya tendo la ndoa,matatizo katika ini na matiti kuwa makubwa.

KWA USHAURI ZAIDI/ELIMU/TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584

Karibu Sana..!!


Ushauri|Tiba|CheckIn 🩺🌡️ContactUs; +255758286584 or INBOX📩. For More Healthtips everyday Link In https://afyaclass.com Also Follow us on Instagram @afyaclass

YOU MUST READ(IMPORTANT)

Magonjwa4 weeks ago

Maumivu chini ya kitovu ni dalili za ugonjwa gani

Maumivu chini ya kitovu ni dalili za ugonjwa gani. Watu wengi huweza kupata maumivu chini ya kitovu, lakini umewahi kujiuliza...

Magonjwa1 month ago

Kaswende ni ugonjwa gani, soma hapa kufahamu

Kaswende ni ugonjwa gani, Kaswende ni maambukizi yanayosababishwa na bakteria. Mara nyingi, huenea kupitia mawasiliano ya kingono au kwa kujamiiana....

Magonjwa2 months ago

Koo kukauka ni dalili ya ugonjwa gani

Koo kukauka ni dalili ya ugonjwa gani Koo kukauka kunaweza kusababishwa na sababu kadhaa, ikiwa ni pamoja na: Upungufu wa...

Magonjwa2 months ago

Amiba ni ugonjwa gani,Fahamu kuhusu Ugonjwa wa Amebiasis

Amiba ni ugonjwa gani Wengi wamezoea kusema hivo ila Amiba(amoeba) ni vimelea vyinavyosababisha ugonjwa, na Ugonjwa huo kitaalam ndyo hujulikana...

Magonjwa3 months ago

kuwashwa nyayo za miguu husababishwa na nini? chanzo na Tiba

kuwashwa nyayo za miguu husababishwa na nini? chanzo na Tiba kuwashwa nyayo za miguu; zipo sababu nyingi ambazo huchangia shida...

magonjwa ya wanawake4 months ago

Ujue Ugonjwa Wa PID (Pelvic Inflammatory Disease)

Ujue Ugonjwa Wa PID (Pelvic Inflammatory Disease) Pid ni ugonjwa gani? PID ni Maambukizi ya bacteria Kwenye Via vya Uzazi...

Magonjwa2 years ago

SHINGO YA MTOTO KULEGEA(CHANZO CHAKE)

SHINGO YA MTOTO KULEGEA(CHANZO CHAKE) Mabadiliko ya Watoto wengi huanza kwenye miezi mitatu ya Mwanzo wakati ambapo Shingo ya mtoto...

Magonjwa3 years ago

MAUMIVU MAKALI SEHEMU YA HAJA KUBWA

Baadhi ya watu wanachanganya tatizo la maumivu makali sehemu ya haja kubwa pamoja na tatizo la Bawasiri,japo mojawapo ya chanzo...

Magonjwa3 years ago

TATIZO LA MASIKIO KUPIGA KELELE,CHANZO NA TIBA YAKE(Tinnitus)

TATIZO LA MASIKIO KUPIGA KELELE,CHANZO NA TIBA YAKE(Tinnitus) tatizo la masikio kupiga kelele Tinnitus, ni Tatizo la masikio kupiga kelele,...

Magonjwa3 years ago

DALILI ZA UGONJWA WA GONO(KISONONO)

 UGONJWA WA KISONONO DALILI ZA UGONJWA WA GONO(KISONONO) Ugonjwa wa gonorrhea maarufu kama GONO au Kisonono ni ugonjwa wa zinaa...

Magonjwa3 years ago

TATIZO LA UKE KUJAMBA PAMOJA NA TIBA YAKE(chanzo cha tatizo hili ni nini?)

Tatizo la Uke Kujamba TATIZO LA UKE KUJAMBA PAMOJA NA TIBA YAKE(chanzo cha tatizo hili ni nini?) Moja ya vitu...

Magonjwa3 years ago

DALILI ZA FANGASI UUMENI,KORODANI PAMOJA NA MATIBABU YAKE

 FANGASI • • • • • DALILI ZA FANGASI UUMENI,KORODANI PAMOJA NA MATIBABU YAKE Mashambulizi ya Fangasi sehemu za siri...

Magonjwa3 years ago

CHANZO CHA TATIZO LA KUOTA NYAMA PUANI PAMOJA NA MATIBABU YAKE

Chanzo cha tatizo la NYAMA PUANI,Dalili zake Pamoja na Tiba yake, Soma makala hii kwa Makini ili upate Kujua kuhusu...

Magonjwa3 years ago

SABABU ZA KUVIMBA KWA MASHAVU YA UKE(TEZI LA BARTHOLIN)

KUVIMBA MASHAVU YA UKE • • • • • • Katika Makala hii tumechambua zaidi kuhusu sababu za kuvimba mashavu...

Magonjwa3 years ago

TATIZO LA MWANAUME KUOTA MATITI(gynecomastia)

TATIZO LA MWANAUME KUOTA MATITI(gynecomastia) Tatizo hili linatokea kwa Baadhi ya wanaume,na hata kupelekea Wanaume hao kuwa na Matiti kama...

MAGONJWA MBALI MBALI

Magonjwa1 day ago

Chanzo cha tatizo la NYAMA PUANI,Dalili zake Pamoja na Tiba yake

Chanzo cha tatizo la NYAMA PUANI,Dalili zake Pamoja na Tiba yake, Soma makala hii kwa Makini ili upate Kujua kuhusu...

Magonjwa3 days ago

Ugonjwa unaosababishwa na kula nyama mbichi

Ugonjwa unaosababishwa na kula nyama mbichi Madhara ya kula nyama ya ng’ombe mbichi Ni desturi ya baadhi ya watu kula...

Magonjwa1 week ago

Mkojo kuuma ni dalili ya ugonjwa gani

Mkojo kuuma ni dalili ya ugonjwa gani Mkojo kuuma au kupata maumivu wakati wa kukojoa ni hali ambayo kwa kitaalam...

Magonjwa1 week ago

Ugonjwa wa gonorrhea maarufu kama GONO au Kisonono dalili Zake

 UGONJWA WA KISONONO DALILI ZA UGONJWA WA GONO(KISONONO) Ugonjwa wa gonorrhea maarufu kama GONO au Kisonono ni ugonjwa wa zinaa...

Magonjwa2 weeks ago

Maana ya hiv negative,Soma hapa kufahamu

Maana ya hiv negative,Soma hapa kufahamu Haya ni maneno ambayo umekuwa ukiyasikia sana linapokuja swala la vipimo cha UKIMWI, je...

Magonjwa3 weeks ago

Kama ndiyo Umegunduliwa ugonjwa wa Kisukari,Soma hii itakusaidia

Kama ndiyo Umegunduliwa ugonjwa wa Kisukari,Soma hii itakusaidia. Kutana na Ilene Raymond Rush ambaye aligunduliwa Kisukari aina ya Pili(Type 2...

Magonjwa3 weeks ago

Ugonjwa unaosababishwa na konokono

Ugonjwa unaosababishwa na konokono Ugonjwa unaosababishwa na konokono unaitwa schistosomiasis, au bilharzia. Ni ugonjwa wa maambukizi unaosababishwa na minyoo wanaoitwa...

Magonjwa3 weeks ago

Ugonjwa wa Pink Eye,chanzo,dalili na Matibabu yake

Ugonjwa wa Pink Eye,chanzo,dalili na Matibabu yake. Wengi tumesikia kuhusu Red Eyes(Macho mekundu) Lakini je umewahi kusikia kuhusu Pink Eyes,?...

Magonjwa3 weeks ago

Omeprazole inatibu ugonjwa gani,Fahamu hapa

Omeprazole inatibu ugonjwa gani Omeprazole inatibu ni nini?, Hili ni swali ambalo limekuwa likiulizwa mara kwa mara na wafwatiliaji wengi...

Magonjwa4 weeks ago

Mate kujaa mdomoni ni dalili ya ugonjwa gani

Mate kujaa mdomoni ni dalili ya ugonjwa gani Mate kujaa Mdomoni,ni tatizo ambalo hutokea kwa baadhi ya watu, na zipo...