UGONJWA WA UTI
• • • • •
TATIZO LA UTI SUGU,DALILI ZAKE,MADHARA YAKE NA TIBA YAKE
U.T.I kirefu chake ni URINARY TRACT INFECTION ikiwa na maana ya maambukizi katika njia ya mkojo na huathiri mfumo wa mkojo na mfumo wa uzazi, wadudu huathiri sana kibofu cha Mkojo na Njia ya mkojo au urethra.
Wanawake wapo katika hatari zaidi ya wanaume kutokana na Maumbile yao yalivyo.Maambukizi ya kwenye kibofu huleta maumivu makali, madhara makubwa hutokea endapo maambukizi yakifika mpaka kwenye figo.
Watu wengi wamekuwa wakijiuliza UTI sugu ni Ipi Hiyo?
Kwanza Tuanzie hapa Maana ya UTI;
UTI ni kifupi cha maneno ya kingereza ambapo kirefu chake ni Urinary Track Infection,Na kwa kiswahili Maana yake ni maambukizi katika Mfumo wa Mkojo
Sasa Basi,
UTI-SUGU-Haya ni maambukizi katika mfumo wa Mkojo lakini yenye Tabia ya kujirudia rudia kila siku au mara kwa mara na kwa Mda mrefu bila kujali Mhusika katumia Dawa nyingi mbalimbali lakini bado Ugonjwa Upo.
CHANZO CHA UTI;
UGONJWA HUU husababishwa na wadudu wadogo sana ambao ni bakteria waitwao Escherichia coli (E. coli), wanapoingia mwilini na kuenda kuathiri mfumo wa mkojo.
U.T.I hutibika haraka kwa mtu ambaye atatumia dawa na pia yaweza kuleta madhara makubwa isipotibika,
BAADHI YA DALILI ZA UTI NI HIZI HAPA
*Maumivu makali wakati wa Kukojoa pamoja na Hali ya Mkojo kuchoma wakati unakojoa
*Maumivu chini ya kitovu hasa hasa upande wa kushoto
*Kupata Homa
*Kupatwa na kichefu chefu na kutapika pia
*Maumivu ya joint,misuli ya mwili Pamoja na Viungo vyote
*Mkojo kuchoma hasa wakati unamaliza kukojoa
*Mkojo kuwa na Harufu sana pamoja na Rangi zisizoeleweka
*Mwili kupata uchovu uliopitiliza hata kama hujafanya kazi yoyote Ngumu
MADHARA YA UTI;
UTI huweza kuathiri mfumo wa uzazi, kibofu, na sehemu mbalimbali mwilini.
- Jua kwamba,ukiwa na maambukizi ya UTI za mara kwa mara ni rahisi pia kupata Magonjwa Mengine kama Fangasi au PID,
- Uke mkavu,
- kupoteza ute ute,
- Maumivu wakati wa Tendo la Ndoa
- Na Hata siku zako za Hedhi kubalika ikiwemo tatizo la Maumivu ya tumbo wakati wa Hedhi pamoja na kutoa blid nyeusi na yenye mabonge mabonge kama Vipande vya Maini
KUMBUKA,UTI huweza kusababisha madhara makubwa sana,Mfano kwa mama Mjamzito,UTi huweza hata kusababisha Ujauzito kutoka,
hasa maambukizi yale yanapohama na kuanza kuingia sehemu ya Mji wa Mimba ambapo ndipo Mtoto alipo, UTI sugu inaweza kusababisha matatizo ya kudumu ya Kibofu cha Mkojo,Figo n.k
UTI Sugu huweza kukusababishia hata uwezo wako wa Kupata Ujauzito ukawa Ni mdogo pia.
Lakini pia matumizi ya dawa Nyingi hasa zile zenye makemiko makali huweza Kuathiri Kibofu cha Mkojo,Figo na hata kuleta Matatizo ya Ini Pia.
MADHARA YA MDA MREFU YA UTI SUGU
Nmeshataja baadhi,Japo ngoja nitoe orodha hii itakusaidia wewe kuelewa kwa Haraka zaidi
~Kuharibu kibofu cha Mkojo,Ini,pamoja na Figo
~Maumivu ya tumbo ambayo hayaishi ukiwa kwenye Hedhi na ukiwa haupo kwenye Hedhi
~Uwezo wa mwanamke kupata ujauzito kupungua
~Mimba kuharibika hasa maambukizi ya UTI yanapofika kwenye Via vya Uzazi ambapo mara nyingi huwa ni PID japo mwanzoni ilianza kama UTI.
☑️ TIBA NA DAWA YA UTI
Tumia dawa ambazo zitafanikiwa kuwatoa kabsa hawa Bacteria,Ndyo utafanikiwa kutibu Tatizo hili la UTI, kwahyo ili kupata tiba sahihi au dawa sahihi wasiliana na wataalam wa afya sehemu ulipo au tuwasiliane pia utapata Msaada.
KWA USHAURI ZAIDI/ELIMU/TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584
afya
afyaclass
afyatips
magonjwa
magonjwa ya wanaume
magonjwa ya wanawake
magonjwa ya watoto
makala
mpya
muhimu
new
post
uzazi
videos
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!