MASUNDOSUNDO
• • • • • •
FAHAMU KUHUSIANA NA MASUNDOSUNDO (genital warts)
Genital warts ni moja ya magonjwa ya zinaa ambayo huambukizwa kwa njia ya kujamiiana. Genital warts ni vinyama ambavyo huota sehemu za siri (mashavu ya uke, uke wenyewe, shingo ya kizazi kwa mwanamke, uume ngozi ya korodan mrija wa mkojo kwa wanaume na maeneo mbalimbali ya sehemu za siri na maeneo kuzunguka sehemu ya haja kubwa kwa jinsia zote.
SABABU
Genital warts husababishwa na virusi aina ya human papilloma virusi hasa aina ya 6 na ya 11. Ziko zaidi ya aina 100 ya virusi hawa ambao pia husababisha masundosundo katika macho mikono mdomo na koo la hewa. Pia wanahusishwa katika kusababisha saratani ya shingo ya kizazi.
Inachukua wiki tatu mpaka miezi nane toka mtu apate kirusi huyu mpaka kuonesha dalili.
VIHATARISHI
1. Kujamiiana pasipo kinga na kuwa na wapenzi wengi
2. Kuanza kujamiiana katika umri mdogo
3. Kupungua kwa kinga ya mwili
4. Uvutaji wa sigara
5. Kuwa na historia ya kuugua magonjwa mengine ya zinaa
Virusi hawa huota sehemu zenye unyevunyevu.
DALILI
Asilimia kadhaa ya watu huwa na virusi hawa paispo kuwa na dalili. Dalili za tatizk hili ni kuota kwa vinyama sehemu ya siri ambavyo huweza kuungana na kutengeneza umbo la cauliflower. Vinyama hivi vinaweza kuwasha kuleta maumivu au kukufanya ujihisi unachomwa moto na iwapo ni vikubwa huweza kutoa damu
MATIBABU
Iwapo genital warts zitaleta shida
1. Dawa za kupaka sehemu husika hutumika na iwapo vitakuwa vi vikubwa sana
2. Upasuaji kuvikata kwa vifaa maalumu au kuvichoma
NJIA YA KUJIKINGA
Njia stahiki na kujikinga na magonjwa ya zinaa hutumika lakini pia kupata chanjo dhidi ya HPV.
By Emmanuel Lwamayanga
Afya ni kitu bora zaidi
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!