FAHAMU KUHUSIANA NA SABABU, DALILI, NA MATIBABU YA MANJANO KWA WATOTO WACHANGA (NEONATAL JAUNDICE)

MANJANO

• • • • • •

FAHAMU KUHUSIANA NA SABABU, DALILI, NA MATIBABU YA MANJANO KWA WATOTO WACHANGA (NEONATAL JAUNDICE) 


Umanjano ni hali ya ngozi,  macho,  mikono na unyayo wa miguu kuwa na rangi ya njano.  Hali hii ni tofauti na homa ya manjano naomba tusichanganye. 


65% ya watoto wanaozaliwa hupata tatizo hili ikiwa kiwango cha bilirubin kwenye damu ni zaid ya 6mg/dl ndan ya sku 7 za kwanza za maisha yao.  8-10% ya watoto wanaozaliwa wanapata kiwango kikubwa cha bilirubin kwenye damu, na asilimia chache hupata kiwango kikubwa sana ambacho huathiri ubongo. Bilirubin hutokana na heme. 


AINA ZA MANJANO


A.  Manjano ya kifisiolojia

Sifa

1. Hutokea masaa 24 baada ya mtoto kuzaliwa

2. Kiwango cha kuongezeka kwa bilirubin kwenye damu ni <5mg/dl kwa siku

3. Kiwango cha juu hufikiwa siku ya 3-5 na manjano haya huisha ndan ya wiki 1 kwa watoto waliotimiza siku na wiki 2 kwa waliozaliwa njiti(kabla ya siku kutimia)

 

Sababu zinazopelekea manjano haya


1. Kuwako kiwango kidogo cha ufanyaji kazi wa kimeng'enya aina ya UDPGT

2. Kuwako kwa kiwango kikubwa cha seli nyekundu za damu

3. Kutokuwepo kwa wadudu rafiki tumboni

4. Chakula kutembea taratibu kutoka sehemu moja kwenda nyingine

5. Kurudishwa kwa bilirubin kutoka kwenye utumbo kurud ktk mwili/damu. 


Watoto wachanga wanakiwango kikubwa sana cha seli nyekundu za damu siku chache wanapozaliwa.  Seli hizi humsaidia mtoto kupata oksijen awapo tumbon mwa mama ake,  anapozaliwa seli hizi zinakuwa haziitajiki kwa wingi kama hapo awali na hivyo huvunjwavunjwa na kupelekea manjano. 


B.  Manjano yasiyo ya kifisiolojia

Sababu

1. Kutokuwiana kwa makundi ya damu kati ya mama na mtoto

2. Kushambuliwa kwa seli nyekundu za mtoto na antibodies za mama

3. Matatizo ya kurithi kama yale yanayoathiri ukuta wa seli nyekundu za damu

4. Ukosefu wa kimeng'enyo aina ya G6PD 

5. Kuvilia na kukusanyika kwa damu ktk maeneo kama kichwan

6. Mtoto njiti

7. Maziwa yanayotokana ma maziwa

8. Maziwa yanayotokana na unyonyeshaji hafifu 


Dalili za bilirubin ktk ubongo

Iwapo kiwango kitakuwa kikubwa kwenye ubongo kitapelekea

1. Uchovu

2. Kunyonya kwa shida

3. Kilio kikali

4. Degedege nk


MATIBABU 

1. Kuwekwa kwenye mashine ya mwanga

2. Kubadilishwa damu.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!