Ticker

6/recent/ticker-posts

FAHAMU KUHUSIANA NA UGONJWA WA NGOZI KWA WATOTO WAVAAO NEPI/ DIAPER (DIAPER DERMATITIS)



UGONJWA WA NGOZI KWA WATOTO

• • • • • •

FAHAMU KUHUSIANA NA UGONJWA WA NGOZI KWA WATOTO WAVAAO NEPI/ DIAPER (DIAPER DERMATITIS)


Diaper rash ni miongoni mwa magonjwa ya ngozi yanayowakumba sana watoto wachanga. Vipele hivi hutokea maeneo kama ambayo yanagusana moja kwa moja na nepi/ diaper maeneo hayo ni makalio, sehemu ya chini ya tumbo, sehemu za siri na sehemu ya juu ya mapaja.

Tatizo hili huweza kutokea kuanzia wiki moja mara baada ya mtoto kuzaliwa na huwapata zaidi watoto wenye miezi 9-12.


Sababu nyingi zinahusishwa katika utokeaji wa vipele hivi nazo ni

1. Unyevu unyevu

2. Msuguano

3. Kuongezeka kwa pH

4. Kuongezeka kwa ufanyaji kazi wa vimeng’enya

Vyote hivi hupelekea kuharibika kwa uwezo wa kinga wa ngozi katika eneo hilo.


Kuongezeka kwa unyevu nyevu kutokanao na joto ama majimaji ya kinyesi au mkojo husababishwa michubuko na hivyo kuharibika kwa ngozi. Na iwapo ngozi itaharibika baada ya michubuko basi kemikali pamoja na wadudu watajipenyeza na kuingia mwilini. Wadudu/ bakteria hutengeneza kimeng’enya kiitwacho urease ambacho huambatana na mkojo kupandisha pH. Kupanda kwa pH kunachochea vimeng’enya vilivyo kwenye kinyesi ambavyo huathiri ngozi. Lakin pia mabadiliko ya pH husababisha bakteria wengine pamoja na fangasi kuvamia maeneo hayo.


VIHATARISHI 

1. Mtoto Kuharisha au kujisaidia mara kwa mara

2. Kutumia aina nyingine za maziwa kama maziwa ya kopo

3. Matumizi ya dawa za kuuwa wadudu


DALILI 

Dalili zake zaweza kuwa vijiupele vidogo vidogo vinavyopelekeq ngozi kuwa nyekundu, kuchubuka kwa nguzi, vipele au vidonda vinavyouma kwenye eneo husika.


DAKTARI ATAKAEMUONA MWANAO ATATAKA KUJUA

1. Dalili zilizoambatana na tatizo hilo

2. Aina ya nepi/diaper, inabadilishwa mara ngapi kwa siku na kama ni ya kufua basi inafuliwa vipi

3. Namna unavyosafisha eneo la mwili ambalo huvalishwa nepi/diaper

4. Uwepo wa magonjwa mengine ya kuambukiza

5. Historia ya magonjwa y ngozi , allegies katika familia na magonjwa ya kuambukizwa

6. Matumizi ya kuuwa wadudu

7. Dawa ambazo zilitumika kumtibu mtoto apo awali.


Kuwepo kwa dalili nilizozitaja hapo awali hakumaanishi moja kwa moja kuwa mtoto anatatizo hili hivyo daktari au mtoa huduma atafanya upembuzi yakinifu kutambua tatizo ni nn hasa.


By Emmanuel 

.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!






Post a Comment

0 Comments