FAHAMU KUHUSIANA NA VIRUSI VYA CORONA (COVID-19), HISTORIA, DALILI, USAMBAAJI, NA NJIA ZA KUJIKINGA
CORONA
• • • • • •
FAHAMU KUHUSIANA NA VIRUSI VYA CORONA (COVID-19), HISTORIA, DALILI, USAMBAAJI, NA NJIA ZA KUJIKINGA
KIRUSI CHA CORONA NI NINI?
corona virus ni kundi kubwa la virusi ambao kimaumbile hufananishwa na kofia ya kifalme yan crown ambayo kwa kilatini huitwa corona na hivyo kupelekea virusi hawa kuitwa hivyo.
Wapo virusi corona wa aina nyingi ambao husababisha dalili katika mfumo wa upuaji na mfumo wa mmeng'enyo wa chakula. Baadhi ya virusi hawa husababisha dalili za kawaida lakin baadhi kama SARS (ambaye kwa mara ya kwanza aligundulika china 2003), MERS (ambaye pia aligundulika kwa mara ya kwanza saudi arabia 2012) na corona virusi wa mwaka 2019 ambaye aligundulika kwa mara ya kwanza china katika kundi la watu wenye nimonia na ambao walikuwa na uhusiano wa moja kwa moja na vyakula vya baharini pamoja na mifugo katika mji wa wuhan. Virusi hawa huwa na dalili kali.
CHANZO
inafahamika kuwa virusi vya corona huzunguka katika wanyama mbalimbali na wakati mwingine huamia kwa binadamu. Sababu za kuhama huweza kuwa mabadiliko ya kijenetiki au kuongezeka kwa ukaribu kati ya binadamu na wanyama kwa mfano Ngamia na Paka. Mpaka sasa haijafamika moja kwa moja corona wa 2019 anaishi hasa katika mnyama gani.
USAMBAAJI
Virusi hawa husambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kupitia vijitone vitengenezwavyo wakati mtu mwenye maambukizi anapoongea, kukohoa au kupiga chafya. Vijitone hivi vyenye vimelea huweza kutua kwenye mdomo au pua za watu walio karibu. Kutokana na ukubwa wa vijitone hivi vyenye vimelea, haviwezi kusambaa umbali mrefu na hivyo vinauwezo wa kusafiri umbali wa mita moja tu na kuanguka katika kuta au sehemu tofauti tofauti.
DALILI
1. homa
2. Kikohozi
3. Upumuaji wa shida
4. Nimonia (pneumonia)
5. Figo kushindwa kufanya kazi
6. Na hata kifo iwapo hatua sitahiki hazijachukuliwa
UCHUNGUZI
uchunguzi wake ufanyika kupitia ukaguzi wa vijenzi vya virusi hawa kupitia PCR.
NJIA ZA KUJIKINGA
1. safisha mikono kwa sabuni na maji
2. Zuia mdomo wako kwa kukunja mkono au kitambaa/tishu au karatasi na kisha itupe mara moja katika pipa la taka kisha lifunike.
3. Punguza ukaribu au migusano isiyo ya lazima na mtu mwenye dalili
By Emmanuel Lwamayang
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!