FAHAMU KUHUSU CHUNUSI, CHANZO NA HATUA ZA MATIBABU YAKE
CHUNUSI
• • • • • •
FAHAMU KUHUSU CHUNUSI, CHANZO NA HATUA ZA MATIBABU YAKE.
Chunusi ni kitu cha kawaida kwa vijana wanaobarehe na mara nyingi huisha kadri mtu anavyokuwa. Chunusi huleta shida kisaikolijia. 75%-95% ya vijana wamekuwa wakisumbuliwa na chunusi. Na kwabaadhi ya watu wazima hasa wanawake wenye chunusi, chunusi hizi husababishwa na matatizo katika homoni.
VISABABISHI
1. Kurithi
2. Homoni
JINSI AMBAVYO CHUNUSI HUTOKEA.
1. Kuongezeka kwa kiwango cha ufanyaji kazi wa tezi ya sebaceous.
Tezi za sebaceous zinapatikana katika sehemu zote za mwili lakini kubwa hupatikana usoni, mgongoni, kifuani na kwenye mabega.
Tezi hizi hutengeneza mafuta ya ngozi yafahamikayo kama sebum ambayo hutolewa nje kupitia vitundu vilivyo katika vinyweleo.
Utengenezaji na utolewaji wa sebum husimamiwa na homoni katika mwili. Tezi hizi kufanya kazi zaidi wakati wa barehe kwasababu ya ongezeko la homoni aina ya androgens.
Kuongezeka kwa utengenezaji wa sebum huzidi uwezo wake wa kutolewa nje na hivyo kupelekea kuziba kwa matundu na kuvimba kwa sehemu zile.
Ongezeko la homoni baada ya kupevuka kwa yai hupelekea ongezeko la utengenezaji wa sebum kwa wanawake na hivyo kupata chunusi ndan ya siku 2-7 kabla ya hedhi. Ongezeko la sebum husababisha kupungua kwa asidi aina ya linoleic na hivyo kupelekea kutokutengenezwa kwa baadhi ya virutubisho vya ngozi na hivyo kupata mabaka meusi kwene chunusi.
2. Mabadiliko katika seli ziitwazo keratinocytes.
Kwa watu wenye chunusi hizi seli hushikana hivyo kupelekea kuziba kwa matundu na hali hii huruhusu kuzaliana kwa vijidudu pale ambavyo husababishwa kuvimba kwa chunusi, kutengeneza usaha na kutengeneza mabaka au rangi nyeusi.
3. Vijidudu aina ya propionibacterium acne. Japo tafiti zimeonesha kuwapo kwa hivi vijududu katika ngozi ya mtu mzima na pasipo kuwapo kwa matatizo. Vijidudu hawa wamekutwa kwenye ngozi za vijana wenye chunusi na hivyo kuaminika kuwa ni moja ya sababu za kutokea kwa chunusi.
MATIBABU.
Matibabu ya chunusi hutegemea aina ya ngozi na mara nyingi huchukua muda mrefu yaani wiki 8 au zaidi.
Matibabu huusisha hatua tano. Hatua hizo nitazieleza kwenye andiko jingine. KUMBUKA USITUMIE DAWA YOYOTE BILA MAELEKEZO KUTOKA KWA DAKTARI.
By Lwamayanga
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!