FAHAMU KUHUSU KUTOKWA NA MAJIMAJI AU UCHAFU UKENI

MAJIMAJI+UCHAFU

• • • • • •

FAHAMU KUHUSU KUTOKWA NA MAJIMAJI AU UCHAFU UKENI.


Kutokwa na uchafu ukeni imekuwa ni tatizo kubwa kwa watu wengi. Uchafu huu unaweza kuwa ni majimaji ya uke ambayo hutengenezwa kwa kiwango kikubwa au inawezekana yakawa yamesababishwa na tatizo.


 Uchafu huu unaweza kuwa umechanganyikana na damu, mkojo au kinyesi.


Maji maji ya kawaida ya uke hufanana maji kabisa na wakati mwingine huwa ni meupe yasiyo na harufu.


SABABU

Sababu zinazoplekea kutokwa na uchafu ukeni zipo kwenye makundi nayo ni,

1. Zisizo za maambukizi. Miongoni mwake ni kutengenezwa kwa maji maji ya uke kwa wingi sana na hivyo kupelekea kuloana kwa sehemu ya nje ya uke au nguo za ndani kuwa na madoa ya njano au kahawia baada ya kukaukia. Maji maji haya au uchafu huu hauna harufu na kwakawaida hausababishi muwasho au kuchubuka. Utengenezaji wa maji maji ya uke utegemea homoni ya estrogen. Iwapo itaongezeka vivyo hivyo utengenezaji wa maji maji haya huongezeka. 

Katika hali ya kawaida tunategemea kuona ongezeko la maji maji(uchafu) haya wakati wa,

a)balehe

b)mimba

c) kupevuka kwa yai

d) tendo la ndoa.


Sababu nyingine za kutokwa na uchafu ni.

2. Zisababishwazo na maambukizi kama fangasi, magonjwa ya zinaa, na magonjwa mengine yasababishwayo na bakteria. Katika baadhi ya magonjwa haya uchafu huu huambatana na kuwashwa kwa sehemu za siri.


Sababu nyingine zinazoweza sababisha muwasho ni allergy itokanayo na kujisafisha ukeni kwa sabuni, kuvaa nguo za ndani zilizo na nylon au kufua nguo za ndani kwa baadhi ya sabuni. 

3. Saratani au uvimbe katika sehemu za mfumo wa uzazi, kulika au kuvutika kutoka nje kwa sehemu ya shingo ya kizazi, sehemu ya uzazi kutokeza nje

4. Kuwepo kwa kitu ukeni. Kwa mfano kuingiza pamba au kitambaa na kisha kukisahau.


Nyingine ni upungufu wa madini ya chuma, folic acid, vitamini B12 na vitamini A, kunywea kwa baadhi ya sehemu za mfumo wa uzazi na hivyo kuweka tezi nje na hivyo kuongeza kiwango cha utengenezaji wa maji maji hasa kwa wanawake waliofikia ukomo wa hedhi, matatizo ya kisukari.


By Emmanuel Lwamayanga




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!