BAWASIRI
• • • • • •
FAHAMU KUHUSU UGONJWA WA BAWASIRI VIHATARISHI, DALILI NA AINA ZAKE
Mfereji wa haja kubwa umezungukwa na mishipa ya damu kwa ndani ambayo hufanya kazi kama mto na husaidia katika ufungaji mzuri wa mrefeji huu (puru)
Ugonjwa wa bawasiri ambao kitaalamu hufaamika kama hemorrhoids hutokea baada ya kuvimba au kutuna kwa mishipa ya damu katika mfereji/ njia ya haja kubwa.
Kuna aina kuu mbili za bawasiri ambazo hutenganishwa na mstari ambao kitaalamu hufahamika kama mstari wa denteti. Aina hizo ni
1. Bawasiri za nje- hizi hutokea chini ya mstari wa denteti
2. Bawasiri za ndani- hizi hutokea juu ya mstari wa denteti. Aina hii ya bawasiri zimewekwa katika makundi au madaraja makuu manne nayo ni
I) mishipa ya damu imevimba lakini haijatokeza nje na haijitokezi hata wakati wa aja kubwa
II) bawasiri hizi hujitokeza wakati wa haja kubwa lakini hurudi ndani zenyewe mara baada ya kujisaidia
III) hizi hutoka nje wakati wa kujisaidia lakini huweza kurudishwa kwa kutumia kidole au mkono wa muhusika
IV) hizi hutokeza nje na haziwezi rudishwa ndani hata kwa kidole au mkono.
Ikumbukwe kuwa asilimia kadhaa ya watu huwa na aina zote mbili za bawasiri.
VISABABISHI/VIHATARISHI
Japo kuwa sababu kubwa inayopelekea kuvimba kwa mishipa hii ya damu na hivyo kutokea kwa bawasiri haifahamiki, ziko sababu mbalimbali ambazo zinahusishwa katika kuchangia kutokea kwa bawasiri nazo ni
1. Ukosefu wa chakula chenye faiba
2. Kufanya kazi nzito au kubeba vitu vizito
3. Kuharisha kwa muda mrefu au kupata choo kigumu
4. Kujikaza sana wakai wa haja kubwa
5. Kuongezeka kwa shinikizo la ndani la fumbatio kutokanako na mimba, wakati wa kujifungua au kujaa kwa tumbo
6. Uzito uliopitiliza
7. Kufanya mapenzi kinyume na maumbile
DALILI
1. Kuwashwa katika eneo la haja kubwa
2. Uvimbe au vinyama eneo la haja kubwa
3. Kinyesi chenye damu au kutoa damu ng’aavu wakati wa kujisaidia
4. Kutokwa na ute ute katika tundu la haja kubwa
5. Maumivu makali
MADHARA
1. Upungufu wa damu japo ni nadra
2. Maumivu makali wakati wa kujisaidia
3. Saratani ya utumbo mpana
4. Kuathirika kisaikolojia
Kunywa maji ya kutosha, kula vyakula vya faiba, mbogamboga na matunda, itasaidia kujikinga.
By Dr. Lwamayanga
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!