KANSA YA UTUMBO MPANA(COLON CANCER),VISABABISHI NA DALILI ZAKE

 KANSA YA UTUMBO MPANA


Kansa hii hutolea eneo la utumbo mpana ambapo kwa kitaalam hujilikana kana COLON CANCER. Ambapo tafiti zinaonyesha vipo vihatarishi mbalimbali vya mtu kupata kansa hii ya Utumbo mpana;


VIHATARISHI VYA KUPATA KANSA YA UTUMBO MPANA

Vihatarishi hivo ni pamoja na;


1. Mtindo wa maisha katika jamii,ikiwemo Swala nzima la Lishe, Mfano; kupendelea kula nyama za makopo,baadhi ya mafuta n.k


2. Umri; ambapo tafiti huonyesha watu walio na umri zaidi ya Miaka 50 ndyo hupatwa sana na Kansa hii ya Utumbo.


3. Watu wenye uzito mkubwa pia wapo kwenye hatari ya kupata kansa ya utumbo mpana.


4. Watu wanaofanya kazi katika maeneo yenye Mionzi, au mgonjwa mwenyewe anayepata tiba ya mionzi kwa mda mrefu.



ZIPI NI DALILI ZA KANSA YA UTUMBO MPANA?

Dalili za kansa ya utumbo mpana ni pamoja na;


1. Kupata choo kilichochanganyika na Damu


2. Kupata choo chenye Rangi Nyeusi


3. Kupatwa na shida ya kichefuchefu pamoja na kutapika


4. Mwili kupata uchovu usio wa kawaida


5. Kupatwa na tatizo la kuishiwa na Damu,kitaalam hujulikana kama ANEMIA


6. Rangi ya Ngozi pamoja na macho kubadilika na kuwa ya manjano,ambapo kwa kitaalam hali hii hujikana kama JAUNDICE.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584 




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!