Ticker

6/recent/ticker-posts

MATIBABU YA MIMBA INAYOTISHIA KUTOKA(THREATEN ABORTION)



MIMBA KUTISHIA KUTOKA

• • • • • •

Tatizo hili hutokea mapema wakati wa ujauzito. Hali hii hujionesha kwa damu kutoka ukeni wakati njia ya shingo ya uzazi ikiwa bado imefunga. Mara nyingi mimba inayotishia kutoka haina tabia ya kuambatana na maumivu yeyote ya tumbo.


Daktari anapompima mgonjwa (Tumezoea kuita kupimwa njia) hukuta shingo ya kizazi ikiwa imefunga na hakuna dalili zozote za kiumbe kutoka ingawa mgonjwa hutokwa na damu sehemu za siri. Aidha mgonjwa huwa hana maumivu yeyote ya tumbo.


MATIBABU YA MIMBA INAYOTISHIA KUTOKANA (THREATENED ABORTION)


Kwenye hali hii, mgonjwa hutakiwa


1. Kupumzika kitandani bila kufanya kazi yeyote (complete bed rest) angalau kwa wiki moja au zaidi mpaka hapo damu itakapoacha kabisa kutoka


2. Kumpa ushauri na uhakika mama ili kumfanya atulie kiakili (assurance and proper councelling)


3. Mama pia hupewa huweza dawa za kumtuliza na kumfanya apumzike (sedatives) kama vile phernobabitone


4. Aidha mama huweza kupewa dawa kwa ajili ya kupunguza kusukuma kwa uterus (antispamodics) kama vile salbutamol


5. Kutofanya tendo la ndoa kwa wiki mbili au tatu


6. Aidha mama na mumewe hupewa ushauri juu ya tatizo hilo na jinsi ya kuendelea na matibabu


#afyabongo


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!







Post a Comment

0 Comments