Ticker

6/recent/ticker-posts

MATUMIZI SAHIHI YA KONDOMU YA KIUME

MATUMIZI SAHIHI YA CONDOM

Matumizi sahihi ya kondomu ya kiume hujumuisha  uvaaji wa kondomu kwa usahihi kabla ya kuingiliana kimwili mpaka wakati wa mshindo au kupiga goli na kisha kuvua na kuvaa nyingine kama mnaendelea na tendo.

Matumizi yasiyo sahihi ya kondomu hupunguza ufanisi wake na  kuleta hatari ya maambukizi ya magonjwa ya zinaa, VVU na mimba zisizotarajiwa.

🔻Zifuatazo Sio Njia Sahihi za Kutumia Kondomu

- Kuvaa kondomu baada ya kuingiliana sehemu za siri hata kama hamjafikia mshindo.

- Kutoishusha kondomu mpaka kwenye shina la uume

- Kutumia vilainishi vya mafuta

- Kutumia Kondomu Zaidi ya moja kwa wakati mmoja

- Kutoishika kondomu katika shina wakati wa kuivua

🔻Matumizi Sahihi Ya Kondomu

Kabla ya kuanza kuitumia kondomu zingatia mambo yafuatayo;

1.Tazama pakiti ya kondomu hakikisha haijaharibika, kupasuka au kutoboka.

2. Hakikisha muda wa matumizi wa kondomu (expiry date) haujapita.

3. Usitumie kondomu uliyoihifadhi kwenye mfuko wa suruali wa nyuma, waleti au sehemu ya kuwekea glovu kwenye gari.

4. Kondomu isihifadhiwe sehemu yenye joto kali, mwanga mkali sana wa jua au mgandamizo.

➡️ Namna Ya Kuvaa Kondomu Kwa Usahihi

Unapotaka kutumia kondomu ya kiume wakati wa kufanya mapenzi, fuata hatua zifuatazo ili kuivaa kwa usahihi.

  • Hakikisha uume umesimama vizuri kabla ya kuanza kuvaa kondomu.
  • Fungua kondomu kwa kutumia mikono yako,
  •  kata kwenye kona za paketi ya kondomu. Kuwa makini usiichane.
  •  Usitumie vitu vyenye ncha laki kama nyembe au mkasi.
  • Chukua kondomu yako ikiwa kama ilivyokunjwa kwenye paketi yake, 
  • minya chuchu ya kondomu kwa nje kisha iweke juu ya uume uliosimama. 
  • Usiikunjue kondomu kabla ya kuiweka kwenye uume.
  • Kunjua kondomu polepole kwa vidole vyako mpaka kwenye shina la uume. 
  • Usitumie mkono wote kukunjua kondomu huku ukiishika,kwani utapunguza mafuta ya kulainisha kondomu hiyo. 
  • Kama haujatahiriwa vuta govi chini kabla ya kuvaa kondomu.
  • Hakikisha kondomu imekaa vizuri na kufika kwenye shina la uume.
  •  Pia chuchu ya kondomu iwe na nafasi kukusanya shahawa.Sasa unaweza kuanza kufanya mapenzi.Baada ya kumwaga shahawa au kupiga goli, vua kondomu kabla ya uume kusinyaa. 

kondom inazuia ukimwi kwa asilimia ngapi

Nimekutana na Maswali mbalimbali kwa baadhi ya Watu wakiuliza kwamba mbona wametumia Kondomu na bado wana dalili za magonjwa ya Zinaa?

Kutumia Kondomu hakukupi asilimia 100% ya kutokupata Magonjwa ya Zinaa hasa usipotumia kwa USAHIHI WAKE,

Na kwa Utafiti mdogo tulioufanya Mwaka 2022,kati ya watu wengi wanaotumia kondomu Karibu asilimia 80% hawatumii kondomu kwa usahihi wake,

Utafiti|Research:Utafiti Kuhusu Matumizi sahihi ya Kondomu

Utafiti huu ulifanyika mnamo mwaka 2022, ambapo ulijumuisha Washiriki 200,

  • Wanaume wakiwa 150
  • na wanawake 50,

Majibu ya Tafiti yalionyesha Karibu asilimia 80% ya Washiriki wote hawajui kabsa Swala la kuhusu Matumizi Sahihi ya Kondomu na wala hawajawahi kusikia hicho kitu,

Asilimia 15% Wanajua kwamba kuna habari ya matumizi sahihi ya kondomu hata kama hawafuati kanuni zake,

Na asilimia 5% Pekee ndyo wanaojua na Kutumia kanuni za matumizi sahihi ya Kondomu.

KONDOM INAZUIA UKIMWI KWA ASILIMIA NGAPI

Matumizi sahihi ya kondomu yanaweza kusaidia kukukinga na magonjwa mbali mbali ya Zinaa Pamoja na Kuzuia Mimba,

Ukitumia Kondomu kwa usahihi inaweza Kupunguza hatari ya Kupata magonjwa ya zinaa yaani sexually transmitted diseases (STDs) pamoja na Kupunguza hatari ya wewe Kupata maambukizi ya Virusi vya Ukimwi(VVU) kwa kiwango kikubwa,

Ingawa pia Matumizi ya Kondomu hayawezi kukukinga kwa Asilimia zote mia moja(100%),

Na hivo basi, Njia pekee ya Kukukinga na magonjwa ya Zinaa ikiwemo maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kwa asilimia Mia moja(100%) ni kutokujihusisha kabsa na kufanya mapenzi(abstain from sexual activity),

au kuwa na Mpenzi Mmoja ambaye hana maambukizi kama haya kwa wakati wote.

Na hatari zaidi ni Kwamba,baadhi watu hasa Wanawake wanaweza kuwa na magonjwa ya Zinaa Kwa muda tu pasipo kuonyesha dalili zozote,

Zipo tafiti mbali mbali za kimaabara ambazo huonyesha kwamba Latex condoms zinaweza kusaidia kuzuia vizuri hata vimelea wadogo zaidi wa magonjwa ya Zinaa(smallest STD pathogens) kupenya ndani.

Pia tafiti zinaonyesha Kiwango cha maambukizi ya virusi vya Ukimwi kati ya watu wanaotumia Condom kwa wakati wote wanaposhiriki tendo la ndoa(Consistent condom use)ambao wenza wao tayari wana maambukizi ya Virusi vya ukimwi ni kidogo,

ikilinganishwa na wale ambao hawatumii kabsa Condom na wanashiriki tendo na wenza wao ambao tayari wana maambukizi,

Hivo basi kutokana na Utafiti huu,inaonyesha Matumizi ya condom yanaweza kupunguza hatari ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kwa kiwango kikubwa.

Vivyo hivo kwenye Magonjwa ya Zinaa(STDs), Matumizi ya Condom yanasaidia pia kupunguza hatari ya Kupata Magonjwa ya Zinaa endapo umeshiriki tendo na mwenza wako akiwa tayari ana magonjwa ya zinaa,

Hasa yale magonjwa ambayo ni rahisi kuyapata kupitia majimaji au fluid sehemu za siri(genital fluids),Hapa nazungumzia magonjwa kama vile;Kisonono,Chlamydia trichomoniasis, n.k,

Tofauti na yale magonjwa ya Zinaa ambayo ni rahisi kuyapata hata kwa njia tu ya mgusano yaani skin-to-skin contact, kama vile genital herpes, maambukizi ya human papillomavirus [HPV], Kaswende pamoja na chancroid.

HITIMISHO:

MATUMIZI SAHIHI YA KONDOMU

Matumizi sahihi ya kondomu ya kiume hujumuisha  uvaaji wa kondomu kwa usahihi kabla ya kuingiliana kimwili mpaka wakati wa mshindo au kupiga goli na kisha kuvua na kuvaa nyingine kama mnaendelea na tendo.

Matumizi yasiyo sahihi ya kondomu hupunguza ufanisi wake na  kuleta hatari ya maambukizi ya magonjwa ya zinaa, VVU na mimba zisizotarajiwa.

🔻Zifuatazo Sio Njia Sahihi za Kutumia Kondomu

- Kuvaa kondomu baada ya kuingiliana sehemu za siri hata kama hamjafikia mshindo.

- Kutoishusha kondomu mpaka kwenye shina la uume

- Kutumia vilainishi vya mafuta

- Kutumia Kondomu Zaidi ya moja kwa wakati mmoja

- Kutoishika kondomu katika shina wakati wa kuivua

🔻Matumizi Sahihi Ya Kondomu

Kabla ya kuanza kuitumia kondomu zingatia mambo yafuatayo;

1.Tazama pakiti ya kondomu hakikisha haijaharibika, kupasuka au kutoboka.

2. Hakikisha muda wa matumizi wa kondomu (expiry date) haujapita.

3. Usitumie kondomu uliyoihifadhi kwenye mfuko wa suruali wa nyuma, waleti au sehemu ya kuwekea glovu kwenye gari.

4. Kondomu isihifadhiwe sehemu yenye joto kali, mwanga mkali sana wa jua au mgandamizo.

➡️ Namna Ya Kuvaa Kondomu Kwa Usahihi

Unapotaka kutumia kondomu ya kiume wakati wa kufanya mapenzi, fuata hatua zifuatazo ili kuivaa kwa usahihi.

  • Hakikisha uume umesimama vizuri kabla ya kuanza kuvaa kondomu.
  • Fungua kondomu kwa kutumia mikono yako,
  •  kata kwenye kona za paketi ya kondomu. Kuwa makini usiichane.
  •  Usitumie vitu vyenye ncha laki kama nyembe au mkasi.
  • Chukua kondomu yako ikiwa kama ilivyokunjwa kwenye paketi yake, 
  • minya chuchu ya kondomu kwa nje kisha iweke juu ya uume uliosimama. 
  • Usiikunjue kondomu kabla ya kuiweka kwenye uume.
  • Kunjua kondomu polepole kwa vidole vyako mpaka kwenye shina la uume. 
  • Usitumie mkono wote kukunjua kondomu huku ukiishika,kwani utapunguza mafuta ya kulainisha kondomu hiyo. 
  • Kama haujatahiriwa vuta govi chini kabla ya kuvaa kondomu.
  • Hakikisha kondomu imekaa vizuri na kufika kwenye shina la uume.
  •  Pia chuchu ya kondomu iwe na nafasi kukusanya shahawa.Sasa unaweza kuanza kufanya mapenzi.Baada ya kumwaga shahawa au kupiga goli, vua kondomu kabla ya uume kusinyaa. 

KUMBUKA HAYA;

  1. Matumizi ya mara kwa mara na sahihi ya kondomu za mpira(latex condoms) hupunguza hatari ya kupata magonjwa yanayotokana na Uwepo wa vidonda sehemu za siri, kama vile genital herpes, kaswende pamoja na chancroid,, pale tu eneo linaloweza kusababisha maambukizi limekingwa.
  2. Utumiaji thabiti na sahihi wa kondomu za mpira(Latex Condoms) unaweza kupunguza hatari ya maambukizi ya Human papillomavirus (HPV) na magonjwa yanayohusiana na HPV kama vile Masundosundo(genital warts) pamoja na saratani ya Mlango wa kizazi.
  3. Ili Condomu iwe kinga kwako ni Lazima utumie kwa Usahihi na kila mara unaposhiriki tendo la Ndoa.
  4.  Kwa Asilimia kubwa, Kushindwa kwa kondomu kukulinda dhidi ya magonjwa mbali mbali ya zinaa Pamoja na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kunatokana na matumizi yasiyosahihi ya Condomu.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!

Post a Comment

0 Comments