SABABU ZA MICHIRIZI YA NGOZI NA MATIBABU YAKE

MICHIRIZI YA NGOZI

• • • • • •

SABABU ZA MICHIRIZI YA NGOZI NA MATIBABU YAKE

Kwa asilimia kubwa Wanawake wajawazito hupatwa na hii hali ya Mpasuko wa Ngozi au Michirizi katika Ngozi hasa hasa maeneo ya Tumboni. Lakini Yapo maeneo mbali mbali ya mwili ambayo huweza kuathiriwa kwa kiasi kikubwa na tatizo hili la michirizi ya Ngozi kama vile;

- Maeneo ya Makalioni

- Maeneo ya kwenye mapaja

- Maeneo ya kwenye matiti

- Maeneo ya Hips

- Pamoja na kwenye tumbo

SABABU ZA KUTOKEA KWA MICHIRIZI YA NGOZI

  1. Kuwepo kwa vinasaba vya tatizo hilo katika koo husika
  2. Ngozi ya mwili kutanuka kwa sababu mbali mbali, kama unene au Ujauzito
  3. Tatizo la michiri huweza kutokana na Unene
  4. Michirizi kutokana na Hali ya Ujauzito
  5. Tatizo la kwenye vichocheo vya mwili Maarafu kama CORTISONE ambavyo huhusika moja kwa moja na kudhoofisha nyuzi nyuzi ambazo huvuta Ngozi pamoja,hivo kupelekea Ngozi kutanuka na kuachana kisha kutengeneza michirizi

WATU WALIO KATIKA HATARI YA KUPATA MICHIRIZI YA NGOZI NI PAMOJA NA;

- Wanawake

- Wajawazito

- Wanene

- Koo yenye shida hii

- Wanaotumia dawa kama prednisone

- Waliofanyiwa upasuaji unaohusisha kukuza maeneo kama hips,makalio au matiti

NINI CHA KUFANYA KUONDOA MICHIRIZI YA NGOZI?

• Paka mafuta yenye mchanganyiko ufuatao mara moja kwa siku;

1. Tumia Nusu kikombe chenye mafuta aina ya zaituni

2. Nusu kikombe chenye ute wa aloe vera

3. Capsules 6 za vitamin E na Capsules 4 za Vitamin A. Pasua capsules hizo ungaunga wake uchanganye pamoja na olive oil na aloevera kisha upake. Kama utatengeneza mchanganyiko zaidi unaweza Kutunza katika jokofu. Mchanganyiko huu ni salama tofauti na cream nyingi zinazouzwa ambazo hazijathibitishwa na mamlaka husika

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!