Ticker

6/recent/ticker-posts

TATIZO LA MIMBA KUTUNGA NJE YA MFUKO WA UZAZI (ECTOPIC PREGNANCY)



MIMBA

• • • • • •

TATIZO LA MIMBA KUTUNGA NJE YA MFUKO WA UZAZI (ECTOPIC PREGNANCY)


  Mimba kutunga nje ya mfuko wa uzazi wa mwanamke au ectopic pregnancy ni tatizo ambalo limetokea kuathiri wanawake mbalimbali. Kwa kawaida, isipokuwa mara chache sana, mimba zitungazo nje ya mfuko wa uzazi hazina uwezo wa kukua kuwa mtoto kamili. Aidha, mimba hizi ni hatari kwa afya ya mama mjamzito kwa vile humfanya kupoteza damu nyingi na hatimaye kusababisha kifo.


Nini hutokea?

Kazi za mirija ya fallopian ni kusafirisha mayai kutoka katika kiwanda chake cha uzalishaji (ovary) mpaka kwenye mfuko wa uzazi (uterus). Utungisho wa yai la kike (ovum) na mbegu ya kiume (sperm) hufanyika kwenye mirija hii.


Mara baada ya utungisho, misuli inayozunguka mirija ya fallopian ikishirikiana na vinyweleo vilivyopo ndani ya mirija hii husukuma kiinitete au yai lililorutubishwa kulipeleka kwenye uterus. Yai lililorutubishwa, au kiinitete, lifikapo kwenye uterus hujipachika katika mojawapo ya kuta zake kwa ajili ya kuendelea kurutubishwa, kukua taratibu na hatimaye kufanya mtoto.


Inapotokea misuli hii kushindwa kufanya kazi au vinyweleo hivi kukosekana, kiinitete hushindwa kusafirishwa kuingia kwenye uterus na hivyo hujitunga nje ya uterus kusababisha ectopic pregnancy. Karibu asilimia 1-2% ya mayai yaliyorutubishwa hutunga nje ya mfuko wa uzazi wa mwanamke.


Aidha, zaidi ya asilimia 95% ya mimba zinazotunga nje ya uterus hutokea kwenye mrija wa fallopian. Mimba zinazotunga kwenye mrija wa fallopian husababisha kiinitete (embryo) kujipachika katika kuta zake na hivyo kusababisha mishipa ya damu inayopita karibu na mrija wa fallopian kupasuka na damu kutoka kwa wingi hali ambayo isiposhughulikiwa mapema husababisha madhara zaidi na hata kifo.


Aina za Ectopic Pregnancy

Kuna aina kuu nne za mimba zinazotunga nje ya mfuko wa uzazi, nazo ni

Mimba zinazotunga kwenye mirija ya fallopian,

Mimba zinazotunga nje ya uterus na nje mirija ya fallopian,

Mimba zinazotunga ndani na nje ya uterus kwa wakati mmoja,

Mimba zinazojirudia kutunga nje ya mfuko wa Uzazi.

Mimba zinazotunga kwenye mirija ya fallopian






Post a Comment

0 Comments