UGONJWA WA RUBELLA KWA MJAMZITO


UGONJWA WA RUBELLA KWA MJAMZITO

Rubella ni ugonjwa wa kirusi unaosababishwa na kimelea aitwae rubella virus,Ugonjwa huu huambukizwa kwa njia ya hewa ambapo mtu huambukizwa kwa kuvuta matone madogo madogo yatokayo kwa mtu mwenye ugonjwa huu (droplets infection) na matone haya huyapata kama mtu huyo akiwa anaongea,kukohoa au kupiga chafya karibu yako.

Maambukizi ya rubella hasa maambukizi mapya kwa mjamzito yanaweza kupelekea maambukizi ya mtoto aliepo tumboni (Congenital rubella Infectio (CRI)) ambayo yanaweza kuleta madhara makubwa sana kwa mimba na kiumbe kilichopo tumboni au mtoto akazaliwa akiwa na hitilafu mbalimbali katika mwili wake na za kudumu (Congenital Rubella syndromes (CRS)).

MADHARA YA RUBELLA KWA UJAUZITO

Sio wajawazito wote wenye rubella watakua na dalili au madhara makubwa ya kuonekana,walio wengi hawapati kashikashi yeyote na mimba inaweza kuenda vizuri tu na au baadae kupata mtoto mwenye tatizo au matatizo mbalimbali;mojawapo ya madhara ya ugonjwa huu kama yakitokea ni

1) Mimba kuharibika (miscarriages)

2) Kupata mtoto mfu (stillbirth)


MADHARA YA RUBELLA KWA MTOTO

1) Mtoto kudumaa tumboni (Fetal growth restriction)

2) Matatizo ya moyo kama matundu kwenye moyo nk (Cardiac defects)

3) Kua na ukungu ukungu kwenye macho (Cloudy cornea)

4) Mtoto wa jicho (cataract)

5) Presha ya macho ya watoto (infantile glaucoma)

6) Matatizo ya kusikia (Hearing loss)

7) Kuvimba ini na bandama (Hepatosplenomegaly)

8) Kuharisha harisha (diarrhea)

9) Manjano(jaundice)

10) Kutokwa na mitoki(Adenopathy)

11) Matatizo ya mapafu (Interstitial pneumonia)

12) Ngozi kua na vialama alama vyekundu au mabaka mabaka mekundu (Petechiae  and purpura)

13) Wanakua na utosi wa mbele mkubwa kuliko kawaida (large anterior fontanelle)

14) Wanapata homa kali ya ubongo (Meningoencephalitis)

.

Picha:Quora

.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!