Connect with us

Magonjwa

UGONJWA WA UKOMA PAMOJA NA DALILI ZAKE

Avatar photo

Published

on

Dalili za UKOMA

……………

UGONJWA WA UKOMA PAMOJA NA DALILI ZAKE

Kwa kawaida Ugonjwa wa Ukoma ni ugonjwa ambao huathiri viungo mbali mbali vya mwili wa binadamu kama  Vile Mikono,miguu,Macho,Uso pamoja na Ngozi pia.

UKOMA ni ugonjwa ambao huweza kuathiri viungo mbali mbali vya mwili,Na ugonjwa huu hujulikana pia kama Hansen’s disease au leprosy,

Kwa Mujibu wa Vituo vya Udhibiti na Kuzuia magonjwa yaani Centers for Diseases control and Prevention(CDC),

Ugonjwa huu husababishwa na bacteria ambao kasi yao ya Ukuaji ni ndogo sana(slow-growing bacteria), Na bacteria hawa Hujulikana kama Mycobacterium leprae.

Bacteria hawa huathiri mfumo wa fahamu au nerves, Ngozi,macho,pamoja na eneo la Puani kwenye nasal mucosa.

Ugonjwa huu ukigundulika Mapema na mgonjwa kupata Tiba,basi hupona kabsa,

WATU HUPATAJE UGONJWA WA UKOMA?

Haijulikani hasa jinsi ugonjwa wa Ukoma unavyoenea kati ya watu,

Ila Wanasayansi kwa sasa wanafikiri kuwa inaweza kutokea wakati mtu aliye na ugonjwa wa Ukoma anakohoa au kupiga chafya, na mtu ambaye hana kuvuta hewa ndani yenye matone yaliyo na bakteria hawa,

Hata hivo ni lazima kuwe na Ukaribu sana na wa muda mrefu na mtu aliye na ukoma ambao haujatibiwa kwa muda wa miezi mingi ili kupata ugonjwa huo,

Huwezi kupata ukoma unapomgusa mtu ambaye ana ugonjwa wa UKOMA au Kwa njia kama vile:

  •  Kupeana mikono
  • kukumbatiana
  • Kuketi karibu na mtu mwenye Ukoma kwenye basi
  • Kuketi pamoja na mtu mwenye Ukoma wakati wa kula chakula n.k

Ugonjwa wa Ukoma pia hauambukizwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto ambaye hajazaliwa wakati wa ujauzito na pia hauenezwi kwa njia ya kujamiiana.

Kutokana na hali ya ukuaji wa polepole wa bakteria na muda mrefu inachukua MUDA pia kuonekana kwa dalili za ugonjwa huo, na mara nyingi ni vigumu sana kupata chanzo cha maambukizi.

Pia Unaweza kuwa kwenye Hatari ya Kupata Ugonjwa wa Ukoma endapo unaishi kwenye maeneo au nchi ambapo Ugonjwa huu umesambaa Sana,

Kwa Mujibu wa Shirika la Afya Duniani(WHO)

Nchi ambazo ziliripoti Zaidi ya Cases Mpya 1,000 za Ugonjwa wa UKOMA( Hansen’s disease) kati ya Mwaka 2011 na 2015 ni Pamoja na:

(1) Africa:

  • Democratic Republic of Congo
  • Ethiopia
  •  Madagascar
  • Mozambique
  • Nigeria
  • United Republic of Tanzania

(2) Asia:

  • Bangladesh
  •  India
  • Indonesia
  • Myanmar
  • Nepal
  • Philippines
  •  Sri Lanka

(3) Americas:

  • Brazil

BAADHI YA DALILI ZA UGONJWA WA UKOMA NI PAMOJA NA;

– Kukatika baadhi ya Viungo vya Mwili kama vile Vidole vya Miguu au mikono

– Ugonjwa wa ukoma huweza kusababisha Ganzi miguuni au mikononi pia

– Kuhisi hali ya kuchomwa eneo lote la Vidole vya miguuni au mikononi

– Vidole vya miguu pamoja na mikono kupooza

– Ugonjwa huu wa ukoma unaweza kusababisha matatizo ya macho ikiwa ni pamoja na upofu wa macho

– Ugonjwa huu wa ukoma huweza kuwa chanzo kikubwa cha uharibifu wa shape ya Pua pamoja na Uso kwa Ujumla.

– Ugonjwa wa ukoma huweza kubadilisha rangi ya ngozi na kuifanya kuwa nyeusi na kuwa na vitu mithili ya ukurutu Hasa mikononi na miguuni.

MATIBABU YA UGONJWA WA UKOMA

Ugonjwa wa Ukoma hutibiwa kwa combination ya dawa mbali mbali Jamii ya antibiotics,

Na mara nyingi huhusisha Matumizi ya Dawa mbili au tatu(2/3) jamii ya antibiotics kwa Wakati Mmoja.

Na dawa hizo ni kama Vile; dapsone pamoja na rifampicin, na wakati mwingine mgonjwa huweza kuongezewa clofazimine kwa baadhi ya aina,

Aina hii ya Matibabu hujulikana kama multidrug therapy.

Njia hii ya matibabu husaidia kuzuia ongezeko la upinzani kwa antibiotic pamoja na bakteria wenyewe, ambayo inaweza kutokea kwa sababu ya matibabu haya kuchukua Muda mrefu zaidi.

Kwa kawaida Matibabu haya huweza kuchukua kati ya mwaka mmoja hadi miwili. Ugonjwa huo unaweza kuponywa ikiwa matibabu yatakamilika kama ilivyoagizwa.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE LINALOKUSUMBUA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In https://afyaclass.com Also Follow us on Instagram @afyaclass

YOU MUST READ(IMPORTANT)

Magonjwa2 months ago

Maumivu chini ya kitovu ni dalili za ugonjwa gani

Maumivu chini ya kitovu ni dalili za ugonjwa gani. Watu wengi huweza kupata maumivu chini ya kitovu, lakini umewahi kujiuliza...

Magonjwa3 months ago

Kaswende ni ugonjwa gani, soma hapa kufahamu

Kaswende ni ugonjwa gani, Kaswende ni maambukizi yanayosababishwa na bakteria. Mara nyingi, huenea kupitia mawasiliano ya kingono au kwa kujamiiana....

Magonjwa3 months ago

Koo kukauka ni dalili ya ugonjwa gani

Koo kukauka ni dalili ya ugonjwa gani Koo kukauka kunaweza kusababishwa na sababu kadhaa, ikiwa ni pamoja na: Upungufu wa...

Magonjwa3 months ago

Amiba ni ugonjwa gani,Fahamu kuhusu Ugonjwa wa Amebiasis

Amiba ni ugonjwa gani Wengi wamezoea kusema hivo ila Amiba(amoeba) ni vimelea vyinavyosababisha ugonjwa, na Ugonjwa huo kitaalam ndyo hujulikana...

Magonjwa5 months ago

kuwashwa nyayo za miguu husababishwa na nini? chanzo na Tiba

kuwashwa nyayo za miguu husababishwa na nini? chanzo na Tiba kuwashwa nyayo za miguu; zipo sababu nyingi ambazo huchangia shida...

magonjwa ya wanawake5 months ago

Ujue Ugonjwa Wa PID (Pelvic Inflammatory Disease)

Ujue Ugonjwa Wa PID (Pelvic Inflammatory Disease) Pid ni ugonjwa gani? PID ni Maambukizi ya bacteria Kwenye Via vya Uzazi...

Magonjwa2 years ago

SHINGO YA MTOTO KULEGEA(CHANZO CHAKE)

SHINGO YA MTOTO KULEGEA(CHANZO CHAKE) Mabadiliko ya Watoto wengi huanza kwenye miezi mitatu ya Mwanzo wakati ambapo Shingo ya mtoto...

Magonjwa3 years ago

MAUMIVU MAKALI SEHEMU YA HAJA KUBWA

Baadhi ya watu wanachanganya tatizo la maumivu makali sehemu ya haja kubwa pamoja na tatizo la Bawasiri,japo mojawapo ya chanzo...

Magonjwa3 years ago

TATIZO LA MASIKIO KUPIGA KELELE,CHANZO NA TIBA YAKE(Tinnitus)

TATIZO LA MASIKIO KUPIGA KELELE,CHANZO NA TIBA YAKE(Tinnitus) tatizo la masikio kupiga kelele Tinnitus, ni Tatizo la masikio kupiga kelele,...

Magonjwa3 years ago

DALILI ZA UGONJWA WA GONO(KISONONO)

 UGONJWA WA KISONONO DALILI ZA UGONJWA WA GONO(KISONONO) Ugonjwa wa gonorrhea maarufu kama GONO au Kisonono ni ugonjwa wa zinaa...

Magonjwa3 years ago

TATIZO LA UKE KUJAMBA PAMOJA NA TIBA YAKE(chanzo cha tatizo hili ni nini?)

Tatizo la Uke Kujamba TATIZO LA UKE KUJAMBA PAMOJA NA TIBA YAKE(chanzo cha tatizo hili ni nini?) Moja ya vitu...

Magonjwa3 years ago

DALILI ZA FANGASI UUMENI,KORODANI PAMOJA NA MATIBABU YAKE

 FANGASI • • • • • DALILI ZA FANGASI UUMENI,KORODANI PAMOJA NA MATIBABU YAKE Mashambulizi ya Fangasi sehemu za siri...

Magonjwa3 years ago

CHANZO CHA TATIZO LA KUOTA NYAMA PUANI PAMOJA NA MATIBABU YAKE

Chanzo cha tatizo la NYAMA PUANI,Dalili zake Pamoja na Tiba yake, Soma makala hii kwa Makini ili upate Kujua kuhusu...

Magonjwa3 years ago

SABABU ZA KUVIMBA KWA MASHAVU YA UKE(TEZI LA BARTHOLIN)

KUVIMBA MASHAVU YA UKE • • • • • • Katika Makala hii tumechambua zaidi kuhusu sababu za kuvimba mashavu...

Magonjwa4 years ago

TATIZO LA MWANAUME KUOTA MATITI(gynecomastia)

TATIZO LA MWANAUME KUOTA MATITI(gynecomastia) Tatizo hili linatokea kwa Baadhi ya wanaume,na hata kupelekea Wanaume hao kuwa na Matiti kama...

MAGONJWA MBALI MBALI

Magonjwa2 days ago

kuharisha na kutapika ni dalili za ugonjwa gani

kuharisha na kutapika ni dalili za ugonjwa gani Unapopata tatizo la kuharisha na kutapika kwa wakati mmoja unaweza kuwaza sana,...

Magonjwa4 days ago

Dalili za infection kwenye damu,mchafuko wa damu

Dalili za infection kwenye damu Mchafuko wa damu,chanzo,dalili na Tiba Mchafuko wa damu; hiki ni kiswahili ambacho watu wamezoea kukitumia...

Magonjwa7 days ago

Ugonjwa wa ngozi sehemu za siri

Ugonjwa wa ngozi sehemu za siri Yapo magonjwa mbali mbali ya ngozi ambayo huweza kuathiri Sehemu za Siri za Mwanaume...

Magonjwa2 weeks ago

Dalili za acid reflux,Soma hapa Kufahamu

Dalili za acid reflux: Tatizo la Gastroesophageal reflux disease (GERD), ni tatizo ambalo huwapata Watu wengi,Tatizo hili hujulikana kwa jina...

Magonjwa4 weeks ago

Ugonjwa wa ngozi kuwa nyeupe,VITILIGO

Ugonjwa wa ngozi kuwa nyeupe,VITILIGO Vitiligo ni ugonjwa wa ngozi kuwa nyeupe au ni ugonjwa ambao huhusisha ngozi kupoteza rangi...

Magonjwa4 weeks ago

Mlipuko wa ugonjwa wa macho,Macho Mekundu

Mlipuko wa ugonjwa wa macho,Macho Mekundu Baada ya Ugonjwa huu wa macho kusumbua watu wengi kwa kipindi cha Hivi Karibuni,...

Magonjwa1 month ago

Scabies ni ugonjwa gani? Soma hapa kufahamu

Scabies ni ugonjwa gani? Soma hapa kufahamu Utangulizi: Scabies huhusisha mtu kuwa na vipele na muwasho kwenye ngozi yake ambapo...

Magonjwa1 month ago

Dalili za ugonjwa wa gono kwa mwanaume

Dalili za ugonjwa wa gono kwa mwanaume Gono ni neno maarufu ambalo kirefu chake ni Gonorrhea na kiswahili chake ni...

Magonjwa1 month ago

Dalili Mpya za ukimwi kwenye ngozi

Zipi ni Dalili za ukimwi kwenye ngozi Zipi ni dalili za Ukimwi kwenye ngozi ya mtu? Fahamu hapa kupitia makala...

Magonjwa1 month ago

Madhara ya COVID-19: Athari za Ugonjwa, Asili na Matibabu

Madhara ya COVID-19: Athari za Ugonjwa, Asili na Matibabu Huu ni ugonjwa wa kuambukiza uliosababishwa na kirusi cha corona, ambao...

Trending