UTUMBO KUJIKUNJA(UTUMBO MKUBWA & UTUMBO MDOGO),VISABABISHI VYAKE PAMOJA NA DALILI ZAKE
Utumbo Kujikunja(Utumbo Mkubwa & Utumbo Mdogo),Visababishi Vyake Pamoja Na Dalili Zake
Tatizo la Utumbo kujikunja huweza kutokea kwa mtu wa Umri wowote, ambapo kwa mtu mzima utumbo kujikunja kitaalam huitwa VOLVULUS na kwa watoto wadogo ambapo utumbo huingia ndani hujulikana kama INTUSUSSEPTION.
ZIPO SABABU MBALI MBALI AMBAZO HUWEZA KUCHANGIA KUTOKEA KWA TATIZO HILI
Sababu hizo ni pamoja na;
✓ Mtu kupata choo kigumu kwa mda mrefu( hali ya kudumu) au Kwa kitaalam huitwa Chronic Constipation
✓ Kupatwa na minyoo ya Utumbo maarufu kama Round worms
✓ Kukaa Mda mrefu bila kula Chakula
✓ Kuwahi kufanyiwa operation ya utumbo hapo nyuma
✓ Matumizi ya Laxatives kwa wingi
✓ Umri pia huweza kuchangia kuwepo kwa shida hii
DALILI ZA UTUMBO KUJIKUNJA
- Ni pamoja na Mgonjwa kuvimba tumbo upande mmoja
- Tumbo kujaaa
- Hali ya kukosa choo
- Kuishiwa na maji
- Kupatwa na homa
- Mapimo ya moyo kwenda mbio
- Maumivu makali sana ya tumbo hasa ukijaribu kulishika
KWA USHAURI ZAIDI, ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!