TATIZO LA KUOTA NYAMA PUANI
Hili ni tatizo ambalo hutokea kwa baadhi ya watu, na tatizo hili huhusisha kuota kwa nyama laini ndani ya kuta za pua na kuzunguka eneo la mwamba wa Pua.
CHANZO CHA KUOTA NYAMA PUANI
Nyama hizi huweza kuota au kutokea ndani ya Pua kwa sababu mbali mbali kama vile;
• Maambukizi ya magonjwa mbali mbali yanayotokea ndani ya Pua au yanayohusisha mfumo mzima wa hewa
• Tatizo la kusumbuliwa na allergy
• Kutokea kwa Uvimbe ndani ya ngozi laini ya puani au katika mfumo mzima wa hewa
• Kuwa na tatizo La Ugonjwa au shida ya Astha( Pumu)
• Pia kufanya kazi maeneo yanayohusu upuliziaji wa madawa mbali mbali huweza kuchangia uwepo wa tatizo hili
Soma: Tatizo la Kuota kinyama Ukeni-Masundosundo
DALILI ZA KUOTA NYAMA PUANI
- Kuanza kwa Dalili za mafua ya mara kwa mara
- Mgonjwa kushindwa kupumua/kupumua kwa shida au kubanwa kutokana na nyama za puani kuziba nafasi ya hewa kupita Puani.
- Mgonjwa kukoroma
- Mgonjwa kutoa sauti flani wakati wa kuvuta na kutoa Hewa puani
- Wakati mwingine mgonjwa kupata maumivu makali ya meno upande wa juu Pamoja na kuwashwa na Macho
- Mgonjwa kupata tatizo la kushindwa kunusa kitu na kupata harufu ya kitu husika mfano chakula N.k
Madhara ya Nyama Za Puani
Madhara ya nyama za puani,Soma hapa kufahamu madhara ya nyama za puani.
Kama unatatizo la nyama za puani,au una mtoto,ndugu, jamaa au rafiki, haya ndyo madhara yanaweza kutokea kwao endapo wana shida hii ya nyama za puani;
1. Kupata shida ya kupumua,kukosa hewa, kutokuvuta na kutoa hewa vizuri, pamoja na kutoa sauti au kusikika kwa sauti wakati wa kupumua
2. Kupata shida ya pua kuvimba, au kuwa na tatizo la Runny, stuffy nose,
Ingawa mara nyingi nyama hizi hazisababishi maumivu yoyote,mtu huweza kupata madhara kama haya
3. Kuwa na tatizo la mafua ambayo haishi, mafua ya mara kwa mara
4. Kuwa na shida ya unyevu unyevu au makamasi kushuka chini ya koo, tatizo ambalo kitaalam hujulikana kama postnasal drip.
5. Kutokuwa na uwezo wa kuhisi harufu ya vitu vizuri au Kutokuwa na uwezo wa kunusa.
6. Kutokuwa na uwezo wa kujua ladha ya vitu mdomoni(taste)
7. Kupata maumivu ya Uso au kichwa mara kwa mara
8. Wakati mwingine unaweza kuhisi maumivu mpaka kwenye meno
9. Mtu kuhisi hali ya kichwa kuwa kizito sana
10. Mtu Kukoroma n.k
NB: Hakikisha unawahi kwa daktari endapo nyama za puani zinakuletea dalili kama hizi;
✓ Kwanza pale ambapo dalili nilizozitaja hapo juu zinazidi kuwa mbaya
✓ Unaona marue rue,huoni vizuri au unapata mabadiliko ya uwezo wa kuona
✓ Kichwa kinavimba kwa mbele
✓ Unapata maumivu kuzunguka macho au eneo linalozunguka macho kuvimba
✓ Maumivu makali sana ya kichwa
✓ Shingo kukakamaa n.k
MATIBABU YA TATIZO HILI LA KUOTA NYAMA PUANI
✓ Tatizo hili la kuota nyama puani huweza kutibika kwa Njia mbili kubwa, Dawa pamoja na Upasuaji.
1. Matibabu ya dawa, huhusisha aina mbali mbali za Dawa kulingana na chanzo cha tatizo hili,
Epuka matumizi ya dawa kabla ya kuongea na Wataalam wa afya kuhusu tatizo lako.
2. Matibabu kwa Njia ya upasuaji huhusisha kuondoa kinyama ambacho kimeziba puani moja kwa moja.
Pamoja na kupewa dawa kwa ajili ya kuzuia maumivu na asipate maambukizi mapya ya magonjwa kwenye kidonda.
Soma: Tatizo la Kuota kinyama Ukeni-Masundosundo
Nyama za puani kwa mtoto,chanzo,dalili na Tiba
Tatizo la nyama za puani ni tatizo ambalo huweza kuwapata watoto pia, hali ambayo husababisha mtoto kupata shida mbali mbali ikiwemo ya Kupumua.
Dalili za Nyama za puani kwa mtoto
Ikiwa Mtoto wako ana shida ya nyama za puani huweza kuonyesha dalili mbali mbali ikiwemo;
– Kutoa Sauti wakati wa kupumua au mtoto kukoroma(Snoring)
– Kupata shida ya kupumua(kuvuta hewa na kutoa hewa)
– Mtoto kupumua kwa kutumia mdomo badala ya Pua
– Mtoto kuwa na mafua ambayo hayakatiki, ya mara kwa mara
– Mtoto kuvimba pua au kuwa na shida ya Runny nose
– Kupungua kwa uwezo wa kunusa na kusikia harufu ya vitu mbali mbali(Decreased sense of smell)
Mtoto wako anaweza kulalamika kwamba hawezi kunusa na kusikia harufu ya vitu au kuonja chakula na kupata ladha yake, ambayo hii ni athari ya kupungua kwa hisia ya kunusa.
– Pia mtoto anaweza kuonekana kama kuna kitu anajiribu kumeza mara kwa mara, kwa lengo la kusafisha koo na njia ya hewa kwa ujumla,
Na wakati mwingine mtoto anaweza kulalamika kuhisi hali ya muwasho kooni,vidonda n.k
Chanzo cha Nyama za puani kwa mtoto
Sababu halisi ya kusababisha nyama za puani kwa mtoto haijulikani;
“The exact cause of nasal polyps is not known”
Ingawa sababu hizi huongeza hatari ya kupata nyama za puani kwa mtoto;
– Tatizo la mzio au Allergic rhinitis, ikiwa mtoto anapata shida ya mzio kwa baadhi ya vipindi huweza kupata shida ya nyama puani, kuvimba eneo la pua n.k
– Tatizo la Cystic fibrosis, ambapo husababisha mucus kwenye mapafu pamoja na viungo vingine vya mwili kuwa nzito kupita kiasi hali ambayo huweza kupelekea maambukizi ya viini vya magonjwa kwa muda mrefu, kupumua kwa shida n.k,
na mara nyingi tatizo hili hugundulika kwa watoto kuanzia miaka 2
– Tatizo la pumu kwa watoto(Asthma), n.k
Matibabu ya Nyama za puani kwa mtoto
Baada ya kuona dalili zozote kama nilivyoorodhesha hapo awali, hakikisha mtoto wako anapata tiba ya tatizo hili la nyama za puani
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
– Soma Zaidi hapa kuhusu Madhara ya tatizo la Nyama za Puani
- https://www.afyaclass.com/2024/09/madhara-ya-nyama-za-puanisoma-hapa.html
- Rejea za Mada;
- Mayoclinic; https://www.mayoclinic.org/diseases-conditions/nasal-polyps/symptoms-causes/syc-20351888
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!