Ticker

6/recent/ticker-posts

JINSI YA KUSOMA KIPIMO CHA MIMBA MAARUFU KAMA UPT



MIMBA

• • • • •

JINSI YA KUSOMA KIPIMO CHA MIMBA MAARUFU KAMA UPT


Kipimo cha Mimba Maarufu kama UPT, ambapo kirefu chake ni urinary pregnancy test na maana yake ni kipimo cha mimba kwa njia ya Mkojo.


Kipimo hiki huweza kusoma pale tu kichocheo kinachojulikana kama human gonadotrophin hormone(HCG) kuzalishwa na Kondo la Nyuma(Placenta) na kuwepo kwenye Mkojo.


Kama ilivyochangamoto kusoma kipimo cha Malaria au Ukimwi ndivo ilivyo changamoto katika kusoma kipimo cha MIMBA na kujua majibu sahihi kwa watu wengi.


Huku wengine wakizidi kuchanganyikiwa kuhusu Neno Positive na Negative. Wakishindwa kujua positive ni mtu ambaye ana mimba au hana, na Negative ni mtu ambaye ana mimba  au hana.


Wengine wakisoma majibu yao,wakikuta wataalam wa afya wametumia maneno mbali mbali kama Reactive na Non- reactive.





1. MANENO YANAYOTUMIKA NA MAANA ZAKE


✓ POSITIVE- Hii ina maana kwamba aliyepima tayari ana mimba au ni mjamzito


✓ HIV NEGATIVE- Hii ina maana kwamba aliyepima hana ujauzito wowote au mimba


✓ REACTIVE- Hii ina maana kwamba aliyepima tayari ana mimba au ni mjamzito


✓ NON-REACTIVE- Hii ina maana kwamba aliyepima hana mimba au Ujauzito


2. JINSI YA KUSOMA KIPIMO CHA MIMBA MAARUFU KAMA UPT


- Baada ya kupima, majibu ya kipimo chetu hutegemea idadi ya mistari itakayojionyesha hapo kwenye Kipimo ambapo;


  • Kipimo kikionyesha Mstari Mmoja, ambapo tunasema mstari wa Control, Aliyepima hana mimba au ni NEGATIVE au NON-REACTIVE

  • Kipimo kikionyesha Mstari zaidi ya mmoja kama hapo kwenye picha yetu,Aliyepima tayari ana mimba au ni POSITIVE au REACTIVE.

Hivo ndivyo tunavyosoma kipimo hiki cha mimba maarufu kama UPT.


Kumbuka; Muda wa kusoma wa kipimo hiki cha UPT,hutegemea muda ambao tayari kichocheo cha HCG kama nilivyoeleza hapo mwanzo kuwepo ndani ya Mkojo.


Watu wengi hawajui na kuanza kupima siku hyo hyo baada ya kufanya mapenzi siku za hatari.Hutafanikiwa kuona chochote hata kama umepata mimba siku hyo.



KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




Post a Comment

0 Comments