UKIMWI
• • • • •
JINSI YA KUSOMA KIPIMO CHA UKIMWI
Kama ilivyochangamoto kusoma kipimo cha Malaria au Mimba ndivo ilivyo changamoto katika kusoma kipimo cha ukimwi na kujua majibu sahihi kwa watu wengi.
Huku wengine wakizidi kuchanganyikiwa kuhusu Neno Positive na Negative. Wakishindwa kujua positive ni mtu ambaye ana ukimwi au hana, na Negative ni mtu ambaye ana ukimwi au hana.
Wengine wakisoma majibu yao,wakikuta wataalam wa afya wametumia maneno mbali mbali kama Reactive na Non- reactive.
1. MANENO YANAYOTUMIKA NA MAANA ZAKE
✓ HIV POSITIVE- Hii ina maana kwamba aliyepima tayari ana maambukizi ya virusi vya Ukimwi
✓ HIV NEGATIVE- Hii ina maana kwamba aliyepima hana maambukizi yoyote ya virusi vya Ukimwi
✓ REACTIVE- Hii ina maana kwamba aliyepima tayari ana maambukizi ya virusi vya Ukimwi
✓ NON-REACTIVE- Hii ina maana kwamba aliyepima hana maambukizi yoyote ya virusi vya Ukimwi
2. JINSI YA KUSOMA KIPIMO CHA UKIMWI
- Baada ya kupima, majibu ya kipimo chetu hutegemea idadi ya mistari itakayojionyesha hapo kwenye Kipimo ambapo;
- Kipimo kikionyesha Mstari Mmoja, ambapo tunasema mstari wa Control, Aliyepima hana maambukizi yoyote ya virusi vya ukimwi au ni NEGATIVE au NON-REACTIVE
- Kipimo kikionyesha Mstari zaidi ya mmoja kama hapo kwenye picha yetu,Aliyepima tayari ana maambukizi ya virusi vya Ukimwi au ni POSITIVE au REACTIVE.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!