Connect with us

afyatips

SABABU ZA KUVIMBA KWA MASHAVU YA UKE(TEZI LA BARTHOLIN)

Doctor Ombeni

Published

on

Imeboreshwa July 14, 2026 by Doctor Ombeni

UVIMBE KWENYE MASHAVU YA UKE

Kuvimba kwenye Mashavu ya Uke au Uke kuvimba(Vaginal swelling) ni tatizo ambalo hutokea kwa Wanawake wengi na linakufanya usiwecomfortable. 

Zipo Sababu mbali mbali ambazo huweza kusababisha hali hii ya kuvimba Mashavu ya Uke ikiwemo;

  • Mabadiliko Kipindi cha Ujauzito
  • Tatizo la Cellulitis
  • Tatizo la maambukizi ya bacteria, bacterial vaginosis,
  • Maambukuzi ya Fangasi Sehemuza Siri(Yeast Infection) kama vile Fangasi jamii ya Candida albicans
  • Maambukizi ya Magonjwa ya Zinaa(Sexually transmitted infections),
  • Tatizo la Mzio au allergies dhidi ya Vitu mbali mbali kama vile Sabuni za kuogea,Dawa,Mafuta,nguo za ndani n.k
  • Au kuumia kwa kugongwa na kitu,misuguano mikali(physical irritation). n.k

 

Endapo umepata mashambulizi ya Fangasi Sehemu za Siri,Dalili hizi huweza kukutokea;

-Kuvimba kwa Mashavu ya Uke

-Rangi ya ngozi ya Mashavu ya Uke kuwa nyekundu zaidi kuliko kawaida

-Kupatwa na Miwasho ukeni

-Kutokwa na Uchafu kama maziwa Mtindi n.k

•Sababu nyingine ya Kuvimba Mashavu ya Uke inaweza kuwa;

  1. Tatizo la Uvimbe(Cyst)
  2. Tatizo la Jipu au Majipu kwenye eneo hili

Sasa tuchambue Uvimbe;Unaojulikana kama Bartholin Cyst.

Bartholin cyst ni aina ya Uvimbe wa ukeni ambao huweza kutokea pande zote mbili za midomo yako ya uke karibu na mlango wa uke wako. Uvimbe huu umepewa jina la Bartholin Cyst kwa Sababu ya jina la tezi za Bartholin(Bartholin gland), ambazo ni tezi mbili ndogo (zilizoko pande zote mbili za uke wako) zinazotoa umajimaji unaosaidia kulainisha uke wako.

SABABU ZA KUVIMBA KWA MASHAVU YA UKE(TEZI LA BARTHOLIN)

Hali ya kawaida ya uke au sehemu za siri za mwanamke ni ya unyevu unyevu,Endapo kuna ukavu hicho ni kiashiria mojawapo kwamba kuna tatizo. Ifahamike kwamba lipo tezi maalum kwa ajili ya kazi hiyo ya kuleta hali ya unyevu unyevu, au ute ukeni na tezi hilo huitwa Bartholin.

Sasa endapo kutatokea shida kwenye vimirija vidogo vya tezi hili la Bartholin Mfano kuziba N.K huweza kusababisha yale maji yanayozalishwa na tezi hili kwa ajili ya kuleta hali ya Unyevu unyevu ukeni, kujaa na hivo kusababisha mashavu ya Uke kuvimba, Hali hii kwa kitaalam huitwa Bartholin Cyst.

Hali ya kuziba vimirija hivi huweza kuhusishwa na sababu ambazo sio za moja kwa moja,Mfano maambukizi ya magonjwa mbali mbali hasa ya zinaaa kama Kisonono.

DALILI ZA TATIZO HILI LA KUVIMBA MASHAVU YA UKE

– Kuanza kupata maumivu wakati unafanya mapenzi

– Kupata maumivu wakati wa kutembea

– Shavu la uke upande uliothirika na shida hii Kuvimba

– Kupatwa na dalili zingine kama joto la mwili kupanda

– Kuanza Kutokwa na uchafu ukeni

– Kusikia au kuhisi ule uvimbe wakati wa kutembea

MATIBABU ya tatizo hili la Kuvimba Mashavu ya Uke

• Kama una tatizo hili,zipo tiba kama vile;

  •  Matumizi ya dawa
  • Tiba zingine ambazo unaweza kupata hospital ni kama vile; Upasuaji au kutumbua sehemu ya Uvimbe Pamoja na Dawa.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Reference;
https://my.clevelandclinic.org/health/diseases/17737-bartholin-cyst
https://www.medicalnewstoday.com/articles/321333
https://www.verywellhealth.com/swollen-vagina-5179412

🏆Certified| Doctor from Afyaclass.Hapa utapata Ushauri & Tiba juu ya magonjwa mbali mbali. Kwa msaada Zaidi Tuwasiliane kupitia namba: +255758286584.Pata dondoo za afya kila siku kwa kufuatilia kupitia: @Facebook | @Instagram | @YouTube.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *