UVIMBE KWENYE MASHAVU YA UKE
• • • • • •
SABABU ZA KUVIMBA KWA MASHAVU YA UKE(TEZI LA BARTHOLIN)
Hali ya kawaida ya uke au sehemu za siri za mwanamke ni ya unyevu unyevu,Endapo kuna ukavu hicho ni kiashiria mojawapo kwamba kuna tatizo. Ifahamike kwamba lipo tezi maalum kwa ajili ya kazi hiyo ya kuleta hali ya unyevu unyevu, au ute ukeni na tezi hilo huitwa Bartholin.
Sasa endapo kutatokea shida kwenye vimirija vidogo vya tezi hili la Bartholin Mfano kuziba N.K huweza kusababisha yale maji yanayozalishwa na tezi hili kwa ajili ya kuleta hali ya Unyevu unyevu ukeni, kujaa na hivo kusababisha mashavu ya Uke kuvimba, Hali hii kwa kitaalam huitwa Bartholin Cyst.
Hali ya kuziba vimirija hivi huweza kuhusishwa na sababu ambazo sio za moja kwa moja,Mfano maambukizi ya magonjwa mbali mbali hasa ya zinaaa kama Kisonono.
DALILI ZA TATIZO HILI
- Kuanza kupata maumivu wakati unafanya mapenzi
- Kupata maumivu wakati wa kutembea
- Shavu la uke upande uliothirika na shida hii Kuvimba
- Kupatwa na dalili zingine kama joto la mwili kupanda
- Kuanza Kutokwa na uchafu ukeni
- Kusikia au kuhisi ule uvimbe wakati wa kutembea
MATIBABU
• Tiba ya awali ni pamoja na kutumia maji ya uvuguvugu,yaweke ndani ya beseni kisha kalia kwa Dakika 15 mpaka 20, lakini hakiksha yanafunika vizuri eneo la uke na pia hii ni kama una umri usiozidi miaka 40, Hakikisha zoezi hili linafanyika kutwa mara tatu ndani ya siku nne.
• Kama tatizo bado lipo,zipo tiba zingine ambazo unaweza kupata hospital kama vile; Upasuaji au kutumbua sehemu ya Uvimbe Pamoja na Dawa,hivo nenda hospital kwa ajili ya kupata tiba.
.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!