HOMA YA MANJANO
• • • • •
UGONJWA WA HOMA YA MANJANO(YELLOW FEVER),CHANZO,DALILI NA TIBA YAKE
Ugonjwa wa homa ya Manjano ni ugonjwa ambao husabibishwa na Virusi huku Msambazaji Mkubwa wa Virusi hao akiwa ni Mbu aina ya Aedes Mosquito.
Mgonjwa huweza kupata athari ya Ngozi kubadilika rangi na kuwa ya Manjano, pamoja na athari ya viungo mbali mbali kama Ini,Figo au Moyo. Pia Ugonjwa huu huweza kumuathiri mtu wa umri wowote au Jinsia yoyote.
DALILI ZA UGONJWA WA HOMA YA MANJANO NI PAMOJA NA;
1. Joto la mwili la Mgonjwa kupanda au kuwa na Homa
2. Kubadilika rangi ya Ngozi pamoja na macho kuwa Manjano
3. Mgonjwa kuwa na maumivu makali kwenye joint, Viungo pamoja na misuli ya mwili
4. Mgonjwa kuwa na maumivu makali ya kichwa
5. Mgonjwa kupoteza kabsa appetite ya Chakula
6. Mgonjwa kuhisi hali ya kichefuchefu pamoja na kutapika
7. Mgonjwa kupata shida pakiwa na mwanga
8. Ugonjwa ukiwa katika hatua mbaya,Mgonjwa huweza kutapika damu, kutokwa na Damu maeneo kama Puani,mdomoni na kwenye macho
9. Mgonjwa kupatwa na tatizo la kuhisi mkojo kila mara
10. Mgonjwa kupoteza fahamu
11. Mgonjwa kuwa na shida ya Figo au Ini
12. Kupungua kwa mapigo ya moyo kwa Mgonjwa huweza kutokea pia.
MATIBABU YA UGONJWA WA HOMA YA MANJANO
Kama ilivyo Tiba kwa magonjwa mengi ambayo chanzo chake ni Aina flani ya Virusi, Mgonjwa atapewa tiba kwa asilimia kubwa kutokana na Dalili atakazozionyesha, na endapo mgonjwa atachelewa kuanza tiba pia huweza kupoteza maisha kabsa.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!