🔻UGONJWA WA INI DALILI ZAKE
• • • • •
MWANZO NA CHANZO CHA UGONJWA
Ini ni kiungo muhimu sana katika mwili wa binadamu ambacho kinafanya kazi nyingi sana kuliko viungo vingine katika mwili wa binadamu,huku ikikadiriwa kwamba zaidi ya kazi 500 huweza kufanywa na Ini Peke yake katika mwili wa Binadamu.
Moja ya kazi muhimu sana ambayo inafanywa na Ini ni pamoja na kupambana na sumu zote zinazoingia katika mwili wa binadamu kutoka katika vyanzo tofauti.
Moja ya vitu vinavyoathiri kwa kiasi kikubwa utendaji kazi wa Ini ni pamoja na Magonjwa yanayoshambulia Ini,Unywaji wa pombe kupindukia N.K
Ini hushambuliwa na Virusi ambavyo hujulikana kama HEPATITIS VIRUSES, ambavyo vipo aina nyingi ila aina B na C ndyo husababisha ugonjwa wa homa ya ini kwa kiasi kikubwa, Hivo basi tunaweza kusema HEPATITIS B AND C VIRUSES Are main cause of HUMAN HEPATITIS DISEASES.
NJIA ZA KUPATA UGONJWA
Maji maji kutoka kwenye mwili wa Mgonjwa,mate,jasho, au Damu huweza kusababisha kuenea kwa ugonjwa huu.
Njia za kupata Ugonjwa huu wa homa ya Ini,hazitofautiani sana na Njia za kupata maambukizi ya Ugonjwa wa UKIMWI, na njia hizo ni kama;
- Kuchangia vifaa vyenye ncha kali
- Ngono zembe
- kuchangia damu na mtu mwenye Ugonjwa
-N.k
UGONJWA WA INI DALILI ZAKE NI PAMOJA NA;
1. Mgonjwa kutoa Mkojo ambao umebadilika rangi mithili ya rangi ya COCA-COLA
2. Kubadilika rangi ya Ngozi pamoja na Macho kuwa ya Manjano
3. Mwili kuchoka na kuishiwa nguvu
4. Mgonjwa Kupoteza kabsa hamu ya kula
5. Kupatwa na hali ya kichefuchefu pamoja na kutapika
KUMBUKA; Chanjo ya kuzuia Ugonjwa wa homa ya Ini yaani Hepatitis B vaccine hutolewa kwa Mtu ambaye bado hajaumwa au kupatwa na tatizo hili. Hivo basi ni muhimu kupata chanjo ya Ugonjwa huu kwani hakuna tiba ya moja kwa moja ya Ugonjwa huu.
Takwimu zinaonyesha Wanawake ndyo waathirika wa Kubwa wa Ugonjwa wa Homa ya Ini kuliko wanaume.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!