UGONJWA WA PRESHA YA MACHO(GLAUCOMA),DALILI ZAKE NA TIBA YAKE

 UGONJWA WA PRESHA YA MACHO

••••••••

UGONJWA WA PRESHA YA MACHO(GLAUCOMA),DALILI ZAKE NA TIBA YAKE


Ugonjwa huu wa presha ya macho ambapo kwa kitaalam hujulikana kama GLAUCOMA, ni ugonjwa unaohusika na kupandisha presha ya Macho kuwa kubwa zaidi ya kiwango cha kawaida ambacho ni 10mmhg hadi 21mmhg. Ikitokea hivi tunasema una presha ya Macho.


VISABABISHI VYA UGONJWA HUU WA PRESHA YA MACHO AU GLAUCOMA


- Presha ya macho hutokea pale ambapo maji katika jicho yanayojulikana kama Aquous homour yakizidi kiwango chake cha kawaida


Zipo sababu ambazo huchangia Mtu kupata presha ya macho,ambazo ni pamoja na;


  1. Urithi wa vinasaba vya tatizo hili katika ukoo flani. Kuwepo kwa mtu mwenye tatizo la Presha ya macho katika ukoo flani,huwaweka wanaukoo huo kuwa katika hatari ya kupata shida hyo kwa wale ambao hawana.
  2. Kuwa na magonjwa mengine ya macho huweza kumsababisha mtu kuwa katika hatari yakupata presha ya macho pia
  3. Kupata majeraha ya macho au kuumia macho kutokana na sababu mbali mbali kama kuanguka,ajali n.k
  4. Kuwa na umri mkubwa Mfano miaka 50 na kuendelea,huweza kuchangia mtu kupata presha ya macho
  5. Kuwa na magonjwa mengine kama kisukari
  6. Matumizi ya baadhi ya dawa Mfano wa Predinisolone
  7. N.K


ZIPI NI DALILI ZA PRESHA YA MACHO?


  • Mgonjwa  kutokuona vizuri shida ambayo mara nyingi huanza kwa jicho moja baadae macho yote mawili
  • Kupata shida ya macho kuona ukungu mbele
  • Macho kuanza kutoa machozi yenyewe huku kwa wengine ikiambatana na maumivu makali ya kichwa
  • Rangi ya macho kubadilika na kuwa njano kwenye weusi wa katikati ya jicho
  • Na kwa baadhi ya wagonjwa macho kuwa na rangi nyekundu kuzunguka jicho

MATIBABU YA PRESHA YA MACHO


Mpaka sasa hakuna tiba au dawa inayotibu kabsa Presha ya wacho, Dawa zote ni kwa ajili ya kuidhibiti kama ilivyo presha zingine katika mwili wa Binadamu.

Hivo basi Mgonjwa atapewa dawa ya kudhibiti hali ya presha ndani ya jicho,na endapo hali itakuwa mbaya zaidi,atafanyiwa upasuaji unaohusisha kutoboa kitundu kidogo ndani ya jicho kwa ajili ya kuruhusu maji (aquous homour) yanayozidi ndani ya jicho kupungua.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.










0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!