CHANZO CHA TATIZO LA MALENGELENGE SEHEMU ZA SIRI PAMOJA NA MATIBABU YAKE
MALENGELENGE
• • • • •
CHANZO CHA TATIZO LA MALENGELENGE SEHEMU ZA SIRI PAMOJA NA MATIBABU YAKE
Malengelenge sehemu za siri ni mojawapo ya magonjwa ya zinaa ambayo hutokana na maambukizi ya Virusi baada ya mtu kufanya mapenzi.
CHANZO CHA TATIZO LA MALENGELENGE SEHEMU ZA SIRI
Chanzo cha tatizo hili la malengelenge sehemu za siri ni kutokana na kirusi jamii ya Herpes Simplex ambaye kwa kifupi ni Maarufu kama HSV ikiwa na maana ya Herpes simplex virus. Aina hii ya virusi ndyo humshambulia mtu na kumsababishia tatizo la malengelenge katika sehemu zake za siri.
Maambukizi haya huchukua mda mrefu kidogo mpaka mtu aanze kuonyesha dalili,lakini endapo ataonyesha dalili,baadhi ya dalili ni kama ilivyo hapa chini kwenye makala hii.
DALILI ZA MAAMBUKIZI HAYA YA HERPES SIMPLEX VIRUS NI PAMOJA NA;
- Kuanza kupata maumivu katika sehemu za siri hasa katika eneo ambalo dalili zingine mbali mbali zimeanza kujionyesha.
- Kupata viuvimbe vidogo vidogo katika maeneo ya sehemu za siri ambayo vina maumivu makali na ambayo huweza kuisha na kurudi zaidi ya mara moja.
- Na mwisho wa siku,kutokea kabsa kwa tatizo la malengelenge katika sehemu za siri za Mgonjwa
- Dalili zingine za ujumla ni pamoja na; Mgonjwa kupandisha joto la mwili au kuwa na homa, Kupata maumivu ya kichwa au kiuno, Mgonjwa kupata uchovu wa mwili kupita kiasi, Mgonjwa kukosa hamu ya kula chakula, N.K
VIPIMO
- Moja ya vipimo muhimu ambavyo husaidia kugundua maambukizi haya ya Herpes Simplex Virus(HSV) mapema hata kabla ya mgonjwa kuonyesha dalili yoyote ni mgonjwa kuchukuliwa sample ya damu na kupimwa maabara.
MATIBABU YA TATIZO HILI
• Hakuna matibabu ya moja kwa moja ya kuondoa au kutibu Mashambulizi ya Virusi hawa wa Herpes Simplex Virusi kama ilivyo Kwa aina nyingi za virusi, Matibabu ya tatizo hili huhusisha kudhibiti dalili tu lakini sio kutibu kabsa hawa Virusi. Matumizi ya Dawa mbali mbali kama vile; Acyclovir hutumika katika kumsaidia mgonjwa kudhibiti dalili hizi za Maambukizi haya ya Herpes simplex Virus.
NB; Orodha ya baadhi ya Magonjwa ya Zinaa ni pamoja na;
- Ugonjwa wa kaswende
- Ugonjwa wa Kisonono
- Ugonjwa wa Ukosefu wa kinga mwilini au Ukimwi
- Tatizo la chlamydia
- Tatizo hili la kuwa na malengelenge sehemu za siri
N.K
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!