DALILI ZA FANGASI UUMENI,KORODANI PAMOJA NA MATIBABU YAKE

 FANGASI

• • • • •

DALILI ZA FANGASI UUMENI,KORODANI PAMOJA NA MATIBABU YAKE

Mashambulizi ya Fangasi sehemu za siri hutokea kwa Jinsia zote mbili yaani kwa mwanaume na mwanamke. Na hapa tunazungumzia fangasi jamii ya Candida Albicans ambayo hupenda sana kushambulia maeneo ya sehemu za siri, Ingawa aina hii ya Fangasi hupenda kushambulia sehemu za siri za Mwanamke zaidi ya Mwanaume.

Wapo fangasi wa maeneo mengine mbali mbali kama vile;

- Fangasi wa kwenye Damu

- Fangasi wa miguuni

- Fangasi wa tumboni

- Fangasi wa kooni

- Fangasi wa kichwani 

N.K

DALILI ZA FANGASI KWA WANAUME NI PAMOJA NA;

1. Kupata miwasho sehemu za siri,Kuzunguka eneo la uume,pamoja na ngozi yote ya korodani na eneo la chini linalotenganisha kati ya Njia ya haja kubwa na Uume, na wakati mwingine miwasho hufika mpaka eneo la haja kubwa

2. Kupata hali ya ngozi kuvimba ambayo hii hupendelea sana kutokea maeneo ya karbu na njia ya haja kubwa

3. Ngozi ya korodani kubadilika rangi na kuwa nyekundu mithili ya mtu aliyeunguzwa

4. Ngozi ya eneo la uume hasa hasa chini ya uume karibu na korodani kubadilika rangi na kuwa nyekundu

5. Kupata michubuko sehemu za siri

6. Na wakati mwingine mwanaume kuhisi maumivu wakati wa kufanya mapenzi

7. Kuhisi kama hali ya kuungua kwenye ngozi ya eneo la sehemu za siri

8. Kutoa harufu mbaya sehemu za siri japo dalili hii huwatokea sana wanawake

MADHARA YA FANGASI WA SEHEMU ZA SIRI NI PAMOJA NA;

- Kero ya kuwashwa na kujikuna hata kama ukiwa mbele za watu

- Kuhisi kama hali ya kuungua mara kwa mara

- Maumivu wakati wa tendo la ndoa

- Harufu mbaya sehemu za siri

MATIBABU YA FANGASI WA UUMENI PAMOJA NA KORODANI

- Dawa mbali mbali za fangasi huweza kutumika na tatizo hili la fangasi sehemu za siri likaisha kabsa. Japo usitumie dawa yoyote pasipo kuongea na wataalam wa afya

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!