DALILI ZA FANGASI WA KICHWANI(VIBARANGO,MAPUNYE) PAMOJA NA MATIBABU YAKE
FANGASI KICHWANI
• • • • •
DALILI ZA FANGASI WA KICHWANI PAMOJA NA MATIBABU YAKE
Fangasi wa kichwani hupenda kuwashambulia watoto wadogo zaidi ya watu wazima, Japo hata watu wazima wanaweza kupatwa na tatizo hili la Fangasi wa kichwani. Hapa ndipo majina mbali mbali yakatokea kama vile Mapunye, vibarango N.K lakini yote yanamaanisha dalili za mashambulizi ya ugonjwa wa Fangasi wa kichwani.
Lakini kuna fangasi pia wa maeneo mengine mbali mbali ya mwili kama vile;
- Fangasi wa Kwenye kucha
- Fangasi wa kwenye damu
- Fangasi wa miguuni
- Fangasi wa kwenye Ngozi
- Fangasi wa kwenye ulimi
- Fangasi wa kooni
- Fangasi wa tumboni
- Fangasi wa ukeni
- Fangasi wa uumeni na korodani
- Fangasi wa mdomoni
N.K
• Soma: Ugonjwa wa Lawalawa,chanzo,dalili na Tiba yake
DALILI ZA FANGASI WA KICHWANI NI PAMOJA NA;
1. Ngozi ya kichwani kuanza kukakamaa na kubadilika rangi kwa mafungu
2. Kuwa na vitu kama mashalingi ya rangi nyeupe kichwani
3. Kutoa kama mba eneo la kichwani
4. Na wakati mwingine eneo la mashilingi kutoa vitu kama usaha
5. Kuwa na vidonda na michubuko kwenye ngozi ya kichwani
6. Kuwashwa sana kwenye Ngozi ya kichwani
• Soma: Ugonjwa wa Lawalawa,chanzo,dalili na Tiba yake
MATIBABU YA FANGASI WA KICHWANI
- Fangasi wa kichwani hutibiwa kwa kutumia aina mbali mbali za dawa za fangasi ambapo zipo dawa za kupaka na endapo tatizo litakuwa sugu na la kujirudia rudia mgonjwa atapewa dawa za fangasi wa kichwani za kunywa.
- Dawa za fangasi ni pamoja na;
1. Clotrimazole cream
2. Fluconazole
3. Ketaconazole
4. Itraconazole (Nzuri sana kwa watoto wadogo)
5. Pamoja na Griseofulvin
KUMBUKA; matumizi ya dawa hovio pasipo maelekezo kutoka kwa wataalam wa afya ni hatari kwa afya yako,hivyo pata maelekezo na ushauri wa kutosha kutoka kwa wataalam wa afya kwanza,kabla ya kuanza kutumia dawa yoyote.
• Soma: Ugonjwa wa Lawalawa,chanzo,dalili na Tiba yake
•
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!