DALILI ZA MIMBA KUHARIBIKA PAMOJA NA CHANZO CHAKE(Tatizo kwa wanawake wengi)

 MIMBA KUHARIBIKA

• • • • •

DALILI ZA MIMBA KUHARIBIKA PAMOJA NA CHANZO CHAKE(Tatizo kwa wanawake wengi)



Mimba nyingi huhuribika kabla ya kufikia miezi mitatu(3) au tunasema huharibika katika miezi mitatu ya mwanzoni yaani kwa kitaalam First Trimester. je utajuaje kama ujauzito unatoka? Zipi ni dalili zake?


DALILI ZA MIMBA KUHARIBIKA NI PAMOJA;


- Mwanamke kupatwa na maumivu makali sana ya tumbo,wengine wanasema tumbo linakata.


- Kuanza kutokwa na damu ukeni wakati wewe ni mjamzito, Japo sio kila damu ikitoka basi wewe mimba yako inatoka, lahasha! kuna baadhi ya wanawake wachache ambao licha ya kuwa ni wajawazito hupata period ile miezi ya mwanzoni,na wengine hutokwa na vidamu damu kwa sababu ya mgandamizo wakati mtoto akijishikiza kwenye ukuta wa mji wa mimba kitendo ambacho hujulikana kama implantation.


- Mwanamke kupata maumivu makali ya kiuno


- Mwili kuchoka na kulegea


- Joto la mwili kupanda au Kuwa na Homa


SABABU ZA MIMBA KUHARIBIKA NI PAMOJA NA;


1. Mabadiliko ya vichocheo vya mwilini yaani hormone Imbalance


2. Magonjwa ambayo hutokana na kinga ya mwili, ambapo mwili hutengeneza antigen ambazo zinashambulia mwili wake wenyewe


3. Shida katika vinasababa vya mwanamke au tunasema Genetic factor


4. Mwanamke kuwa na shida ya uvimbe kwenye kizazi


5. Shida ambayo hutokana na maumbile ya mji wa mimba ulivyo kwa mwanamke mwenyewe


6. Mwanamke kuwa na tatizo la uzito mkubwa


7. Matumizi ya dawa hovio ambapo dawa zingine huweza kusababisha mimba kutoka


8. Unywaji wa pombe pamoja na uvutaji wa sigara wakati wa ujauzito


9. Mwanamke kupata ajali kwa kuanguka,kupigwa N.K


10. Matumizi ya vitu vyenye sumu,au sumu ya kimazingira


11. Matumizi ya vinywaji vyenye kiwango kikubwa cha Caffeine


N.K



KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!