DALILI ZA UGONJWA WA KISUKARI(Maana ya kisukari na dalili )

 UGONJWA WA KISUKARI

• • • • • •

DALILI ZA UGONJWA WA KISUKARI(Maana ya kisukari Na dalili zake)


Ugonjwa wa kisukari ni ugonjwa ambao huhusisha kuwepo kwa kiwango kikubwa cha sukari kwenye damu au kuwa na kiwango kidogo sana cha sukari kwenye damu kuliko kawaida.


Hivo hapa tunapata aina mbili za kisukari;

(i) Kisukari cha kupanda au kwa kitaalam tunaita Hyperglycemia

(ii) Na kisukari cha kushuka au kwa kitaalam tunaita Hypoglycemia


(iii) Kwa kuongezea tu, kuna kisukari cha mimba ambacho hutokea wakati mama akiwa mjamzito tu.


KUMBUKA; Kiwango cha kawaida cha sukari kwenye damu huweza kuwa kati ya 4.0 mmol/L mpaka 5.4mmol/L Ukiwa na njaa ila baada ya kula huweza kupanda mpaka 7.8mmol/L.


CHANZO CHA UGONJWA WA SUKARI


Sababu za kuwa na ugonjwa wa sukari ni pamoja na Kushindwa kufanya kazi kwa Kichocheo cha Insulini katika mwili wako.


DALILI ZA UGONJWA WA SUKARI(HAPA NAZUNGUMZIA SUKARI YA KUPANDA) NI PAMOJA NA;


- Mgonjwa wa kisukari hukojoa sana mara kwa mara kuliko kawaida


- Kupata kiu kubwa ya maji mara kwa mara


- Kupata shida ya kuona ambapo kwa wengine hupata upofu wa macho kabsa


- Kuchoka haraka na Mwili kupata uchovu usio wa kawaida


- Uzito wa mwili kushuka kwa kasi sana hapa ndyo baadhi ya wagonjwa wa kisukari huanza kukonda sana hata kama walikuwa wanene


- Kuwa na shida ya vidonda kupona kwa haraka zaidi kama watu wengine, hasa vidonda vya miguuni hata wengine kufikia hatua ya kukatwa Miguu


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!