FAHAMU KWA UNDANI KUHUSU VIDONGE VYA UZAZI WA MPANGO(au vidonge vya majira pamoja na Athari zake)
VIDONGE VYA UZAZI
• • • • •
FAHAMU KWA UNDANI KUHUSU VIDONGE VYA UZAZI WA MPANGO(au vidonge vya majira pamoja na Athari zake)
Vidonge vya uzazi wa mpango vimekuwa vikitumiwa na wanawake wengi katika maeneo tofauti tofauti,huku wengine wakiwa hata hawajui uhalisia wa vidonge hivi.
Kwa ufupi tu, kuna aina mbili za vidonge vya uzazi wa mpango, Hapa hatunzungumzii kuhusu P2 kwani hizi sio kwa ajili ya uzazi wa mpango bali ni dawa za dharura au emmergence contraceptive pills ambazo hutolewa kwa matukio maalumu kama mtu aliyebakwa, ambaye kafanya mapenzi kwa bahati mbaya siku za hatari bila kupanga kubeba mimba N.K, ila sio kama njia ya kudumu ya kupanga uzazi na zina madhara makubwa endapo zitatumika kama njia ya kupanga uzazi.
Aina hizo mbili ni pamoja na;
1. Kuna vidonge vya uzazi wa mpango vya rangi mbili kama unavyoona kwenye picha hapo chini ambavyo hujulikana kama Combined oral contraceptives pills(COC's) ikiwa na maana ya kuwa na mchanganyiko wa vichocheo aina mbili yaani progesterone pamoja na Estrigen.
Vidonge hivi humezwa kila siku kidonge kimoja kimoja bila kuacha kwa kufata mstari ambapo mwanamke hupewa paketi tatu kwa ajili ya kutumia kwa kipindi cha miezi 3. Vidonge hivi haruhusiwi kutumia mama anayenyonyesha kwani vinaathiri uzalishaji wa maziwa kwa mama.
2. Aina ya pili ni vidonge vya uzazi wa mpango vya rangi moja. Ambapo vidonge hivi kuwa na kichocheo cha aina moja tu ambacho kinajulikana kama Estrogen. Vidonge hivi ni sahihi kutumia mama mjamzito kwani haviathiri utengenezaji wa maziwa kwa ajili ya mtoto kunyonya.
KUMBUKA; Njia hii sio nzuri kama unapanga uzazi wa muda mrefu mfano miaka 2 au 3, kwani itakulazimu wewe mtumiaji kumeza vidonge kila siku kwa kipindi cha miaka 2 au 3 kitu ambacho sio salama kiafya.
MADHARA YA VIDONGE VYA UZAZI WA MPANGO NI PAMOJA NA;
- maumivu makali ya kichwa
- Kubadilika kwa mzunguko wako wa hedhi
- Kupata blid ya vitone vitone
- Huathiri utengenezaji wa maziwa ya mtoto endapo utatumia vya rangi mbili
N.K
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!