KUKAA SEHEMU MOJA KWA MDA MREFU
• • • • •
FAHAMU MADHARA YA KUKAA SEHEMU MOJA KWA MUDA MREFU
Kwa kawaida afya ya mwili hutegemea sana na mtindo wa maisha wa mtu au kama wengine wanavyopenda kusema Lifestyle. Hapa tunazungumzia vitu vingi ikiwemo chakula unachokula, kazi unayofanya, Mavazi unayovaa pamoja na mambo mengine ambayo huyafanya kila siku.
Kwa watu ambao wanafanya kazi mbali mbali za kukaa kwa muda mrefu mfano kazi za maofisini, madreva wa magari ya umbali mrefu, N.K , wapo kwenye hatari kubwa ya kupatwa na matatizo mbali mbali ya kiafya.
MADHARA YA KUKAA MUDA MREFU SEHEMU MOJA KIAFYA NI PAMOJA NA;
1. Unakuwa kwenye hatari ya kupatwa na magonjwa mbali mbali ya moyo kama vile moyo kuwa mkubwa pamoja na mishipa ya damu ndani ya moyo kuziba.
2. Unakuwa kwenye hatari ya kupatwa na matatizo ya shinikio la damu au Presha
3. Unakuwa kwenye hatari ya kupatwa na tatizo la uzito kupita kiasi pamoja na unene
4. Unakuwa kwenye hatari ya kupatwa na tatizo la Kisukari
5. Unakuwa kwenye hatari ya kupatwa na shida ya kuwa na kinga ya mwili ndogo thidi ya magonjwa mbali mbali
6. Unakuwa kwenye hatari ya mwili kukosa nguvu pamoja na kudhoofika kwa misuli mbali mbali ya mwili
7. Kupatwa na shida ya kuwa na Msongo wa mawazo huweza kumpata mtu ambaye anakaa sehemu moja kwa muda mrefu hususani yule ambaye hama cha kufanya
8. Kupata ulemavu wa viungo mbali mbali vya mwili ikiwemo pamoja na miguu
9. Unakuwa kwenye hatari ya kupatwa na matatizo ya miguu kuuma
10. Kupatwa na matatizo ya mifupa
11. Kupatwa na matatizo ya maumivu ya kiuno cha mara kwa mara
12. Kupatwa na tatizo la maumivu ya Mgongo wa mara kwa mara
USHAURI; Kwa wewe ambaye kazi zako ni za kukaa chini sehemu moja na kwa muda mrefu unashauriwa kutenga muda wa kufanya mazoezi mbali mbali ya mwili ili kuepusha kupatwa na matatizo mbali mbali kiafya
- Tenga muda wa mazoezi
- Tenga muda wa kufanya kazi zingine ambazo zitakufanya utoke sehemu moja kwenda nyingine
- Epuka matumizi ya pombe kupita kiasi
•
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!