KALENDA
• • • • •
KUTUMIA KALENDA KAMA NJIA YA UZAZI WA MPANGO(faida na hasara zake)
Matumizi ya kalenda kama njia ya uzazi wa mpango, njia hii ni nzuri sana na kila mmoja anaitamani kuitumia, japo wengine hawaifahamu kwa kina njia hii.
Matumizi ya kalenda kama njia ya uzazi wa mpango hutegemea mzunguko wako wa hedhi kwa asilimia mia moja. Hivo darasa kubwa linahusu kuujua vizuri mzunguko wako wa hedhi.
FAIDA ZA NJIA YA UZAZI WA MPANGO YA KALENDA NI PAMOJA NA;
1. Njia hii ni rahisi kutumia kama ukiiyelewa vizuri
2. Njia hii haihusishi kichocheo chochote hivo humuepusha mtumiaji na madhara mengi kama mvurugiko wa vichocheo vya mwili,hedhi kubadilika kabsa, N.K
3. Njia hii ni safi na salama kwa asilimia 100%
4. Ni harihisi kupata mtoto kwa muda unaotaka wewe tofauti na njia zingine ambazo hata baada ya kuacha kutumia uwezo wa kupata mimba huchukua muda mrefu kurudi Mfano; Sindano za uzazi wa mpango au maarufu kama Depo
HASARA ZA NJIA HII YA KALENDA NI PAMOJA NA;
- Njia hii haifai kwa mtu ambaye mzunguko wake wa hedhi ni wa kubadilika badilika yaani kwa kitaalam tunasema Irregular menstrual cycle.
- Upo kwenye hatari ya kubeba ujauzito mda wowote mzunguko ukibadilika pasipo wewe kujua. Vipo vitu mbali mbali ambavyo huweza kuchangia mzunguko wa hedhi kubadilika gafla kama vile;
(i). matumizi ya baadhi ya dawa zinazohusisha kuongeza au kupunguza vichocheo vyako vya mwili
(ii). Mabadiliko ya gafla ya kimazingira
(iii). Hali ya msongo wa mawazo kutokana na vitu mbali mbali kama vile kufiwa na mtu wako wa karibu, kupigwa N.K
-
NB; Hivo basi, mfano; kama mzunguko wako ni siku 28 na haubadiliki badiliki, unahitaji tu elimu ya kutosha jinsi ya kutumja njia hii, ila kama ubadilika badilika njia hii sio rafiki kwako.
Kumbuka kuna aina tatu ya mizunguko ya hedhi kwa kuzingatia muda ambayo ni;
(i). Kuna mzunguko mfupi yaani siku 21
(ii). Kuna mzunguko wa wastani yaani siku 28
(iii). Kuna mzunguko mrefu yaani siku 35
Lakini tunaweza kugawanya mizunguko ya hedhi kwa kuzingatia mabadiliko yake ambayo ni;
(i). Kuna mzunguko usio badilika badilika yaani REGULAR MENSTRUAL CYCLE
(ii). Na kuna mzunguko wa kubadilika badilika yaani IRREGULAR MENSTRUAL CYCLE
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!