Ticker

6/recent/ticker-posts

MADHARA YA KUTUMIA DAWA HOVIO PASIPO MAELEKEZO KUTOKA KWA WATAALAM WA AFYA(athari za tabia hii)



 DAWA

• • • •

MADHARA YA KUTUMIA DAWA HOVIO PASIPO MAELEKEZO KUTOKA KWA WATAALAM WA AFYA(athari za tabia hii)


Nmekuwa nikisisitiza katika makala zangu nyingi kuhusu matumizi ya dawa ambayo yanatokana na maelekezo kutoka kwa wataalam wa afya na sio kuamua tu mwenyewe kutumia dawa, kwani tabia hii huweza kukuletea madhara makubwa kwa afya yako.


Baadhi ya madhara ambayo huweza kutokea kwa kutumia dawa mwenyewe bila maelekezo kutoka kwa wataalam wa afya ni pamoja na;


- Kuzidhisha dose ya dawa,kitu ambacho huweza kukuletea madhara makubwa kama vile; kuharibu ini lako, figo, pamoja na viungo vingine vya mwili wako.


-  Kutumia dawa ambazo sio sahihi kulingana na tatizo lako, kitu ambacho huweza kukuletea madhara makubwa ikiwa ni pamoja na Kupoteza maisha kabsa kwani badala ya kutibu tatizo unaweza kuzidisha tatizo.


- Mimba kuharibika, hii hutokea sana kwa wanawake wengi wajawazito kwani kwa upande wa mjamzito dawa nyingi haziruhusiwi na zina madhara makubwa kwa mtoto aliyetumboni pamoja na mama mwenyewe. Hivo basi tabia ya kutumia dawa hovio huweza kusababisha mama mjamzito kutumia dawa ambazo ni hatari kwa ujauzito wake,kitu ambacho huweza kusababisha ujauzito wake kuharibika.


- Ulemavu wa maisha au kudumu, matumizi mengine ya dawa ambayo sio sahihi huweza kukusababishia hali ya kupooza,stroke, au ulemavu wa kudumu katika viungo mbali mbali vya mwil wako.


- Kutengeneza kitu kinaitwa body resistance, hali ambayo mwili unazoea dawa na dawa hiyo kutofanya kazi tena


N.K


NB; Ni vizuri kutumia dawa baada ya kupewa maelekezo ya kina kutoka kwa wataalam wa afya, na sio kupenda kunywa dawa mwenyewe. Epuka tabia hii kwani kinga ni bora kuliko tiba.



KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.






Post a Comment

0 Comments