UKEKETAJI
• • • • •
MADHARA YA UKEKETAJI KWA MWANAMKE(Hii ni mojawapo ya mila potofu)
Hii ni mojawapo ya mila potofu ambayo ni hatari kwa afya ya mwanamke. Kitendo hiki huhusisha kukata au kupunguza baadhi ya sehemu katika utupu(uke) wa mwanamke ikiwemo kisimi,mashavu ya uke N.K
Ambapo jamii zinazofanya kitendo hiki zikiamini kwamba eti kinamsaidia mwanamke kutokuwa na tabia mbaya kama umalaya N.k na kuweza kutulia katika ndoa yake. Lahasha! hyo sio dawa.
MADHARA YA UKEKETAJI KWA MWANAMKE NI PAMOJA NA;
• Mwanamke kuvuja damu nyingi wakati wa ukeketaji na kupata shida ya kuishiwa na damu
• Mwanamke kuchanika vibaya wakati wa kujifungua na kupoteza damu nyingi zaidi
• Mwanamke kupata maumivu makali wakati wa kufanyiwa kitendo hiki
• Mwanamke kupoteza maisha wakati anafanyiwa ukeketaji au wakati anajifungua kutokana na kumwaga damu nyingi sana
• Mwanamke kuathirika kisaikolojia na kujiona yuko tofauti na wanawake wenzake hasa akiangalia maumbile yake
• Mwanamke kupatwa na magonjwa mengine kwa haraka kwani kwa asilimia kubwa kitendo hiki hakifanyiki katika mazingira ya Usafi
N.K
EPUKA UKATILI HUU KWANI HAUNA FAIDA YOYOTE KIAFYA,BADALA YAKE NI CHANZO CHA MADHARA MAKUBWA KIAFYA IKIWEMO PAMOJA NA KUPOTEZA MAISHA YA WATU.
KWA USHAURI ZAIDI AU ELIMU TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!