TATIZO LA UKE KUJAMBA PAMOJA NA TIBA YAKE(chanzo cha tatizo hili ni nini?)
TATIZO LA UKE KUJAMBA PAMOJA NA TIBA YAKE(chanzo cha tatizo hili ni nini?)
Baada ya tafiti mbali mbali kufanyika imeonekana baadhi ya sababu mbali mbali huchangia shida ya uke kujamba,hasa wakati wa kufanya mapenzi, na sababu hizo ni kama;
- Kulegea kwa misuli ya uke,hivo kupelekea uke kuwa wazi mara nyingi na kuruhusu hewa kuingia na kujaa ukeni. Hivo kusababisha uke kujamba.
- Kuosha uke kwa maji ya moto mara kwa mara pia huchangia hali ya uke kujamba kwani huchangia misuli ya uke kulegea na kusababisha uke kuwa wazi na kusababisha hewa kujaa ukeni.
- Kulala hivo hivo mara tu baada ya kufanya mapenzi bila kujisafisha ukeni, hali hii huathiri joto la ndani ya uke na kupelekea shida mbali mbali kama hii ya uke kujamba.
Soma: Tatizo la Uke Kulegea,chanzo,dalili na Tiba yake
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
Tatizo la Uke kutoa hewa au Uke Kujamba ni tatizo ambalo kwa kitaalam hujulikana kama Vaginal flatulence,vaginal flatus, au queef,
Hali hii ni utoaji wa hewa iliyonaswa kutoka kwenye uke. Kujaa gesi kwenye uke ni jambo la kawaida kwa Wanawake wengi, Na Mara nyingi hutokea wakati wa kufanya Tendo la Ndoa au mazoezi. Kwa kiasi kikubwa, hali hii haina Athari yoyote kwenye afya ya Uzazi.
Dalili za Tatizo hili la Uke Kujamba au Uke kutoa Hewa
-Dalili kubwa ya Uke kutoa hewa ni Kujamba Ukeni,mithili ya Mtu ambaye amejamba kwa njia ya haja kubwa,
Hivo mtu mwenye hali hii huweza kusikia Sauti ya Kijambo Ukeni,kama unavyojamba kawaida.
-Tofauti na Kujamba Kwa kawaida,Kujamba Ukeni hakutoi harufu yoyote mbaya kwa Asilimia kubwa, labda kama una tatizo Lingine la Kiafya.
Hizi ni baadhi ya Dalili za Tatizo hili la Uke Kujamba au Uke kutoa Hewa.
Sababu Zingine za Uke Kutoa hewa au Uke kujamba
Hizi hapa ni baadhi ya Sababu hizo pamoja na Vitu ambavyo huongeza hatari ya Mwanamke kutoa hewa Ukeni;
• Aina za Staili ya Kujamiiana au Kuingiza Kitu kwenye Uke, Kitu kinapoingizwa kwenye uke, kinaweza kusababisha hewa kuingia ndani ya Uke.
• Pia Inawezekana gesi kuingia Ukeni wakati wa uchunguzi wa fupanyonga, wakati daktari anapoingiza au kuondoa kifaa kama speculum.
• Aina ya Mazoezi na jinsi unavyofanya Mazoezi vinaweza kusababisha hewa kunasa ndani ya uke.
Wanawake mara nyingi huripoti gesi Ukeni wakati wa shughuli fulani za kimwili, kama vile kufanya mazoezi aina ya yoga. n.k
• Ujauzito au Kukoma kwa Hedhi,
Baadhi ya wanawake huripoti matukio zaidi ya kujaa gesi ukeni wakati wa ujauzito au kukoma hedhi.
• Baada ya Kujifungua,
Wanawake wengi pia huripoti shida hii ya kujamba Ukeni au kutoa hewa Ukeni baada ya kujifungua kwa Njia ya Kawaida.
Kuzaa mtoto na hali zingine zinazoweka shinikizo kwenye tishu za fupanyonga zinaweza kusababisha hili.
• Muundo au Anatomia ya Sakafu ya Pelvic,
Sakafu ya fupanyonga ya kila mtu ni ya kipekee kidogo, na kwa baadhi ya Wanawake inaweza kuwa rahisi zaidi kuliko wengine kutoa hewa iliyonaswa.
• Pia mara chache tatizo la kujaa hewa kwenye uke huhusishwa na fistula ya ukeni,
Fistula ni tundu au mwanya usio wa kawaida unaounganisha uke na kiungo kingine, kama vile kibofu cha mkojo, koloni, au rektamu.
Ikiwa fistula imeunganishwa na koloni au rectum, inaweza kusababisha mkusanyiko wa kinyesi kutoka kwa njia ya uke.
Kuzaa, matibabu ya saratani, kuumia, na taratibu fulani za upasuaji zinaweza kusababisha kuundwa kwa fistula. Mwone daktari wako ikiwa kujamba kwako Ukeni au Hewa inayotoka ukeni ina harufu mbaya, au ukigundua inaambatana na kutokwa kwa maji yasiyo ya kawaida Ukeni.
Jinsi ya Kugundua tatizo la Uke kujamba(Diagnosis of Vaginal Flatulence)
Ingawa hakuna vipimo maalum au taratibu za kubainisha chanzo cha hewa kutoka kwa uke, daktari wako anaweza kufanya uchunguzi wa pelvic ili kudhibiti ikiwa kuna tatizo kubwa zaidi.
Hivo unaweza kufanyiwa na aina zingine za Vipimo kulingana na dalili ulizonazo kwa wakati huo.
Matibabu ya Tatizo hili la Uke Kujamba au Uke kutoa Hewa
Matibabu yake asilimia 100% hutegemea na chanzo husika, Hivo baada ya kugundua chanzo utapewa Tiba Sahihi.
Zipo dawa pamoja na Vitu vya Kufanya na Kuzingatia ili kukusaidia hali hii kuisha
NA KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
Hakikisha Unapata Msaada mapema ikiwa Tatizo hili la Uke Kujamba au Uke kutoa Hewa linaambatana na matatizo Kama haya;
- Kutoa harufu mbaya Ukeni
- Kutokwa na Usaha au uchafu mwingine Ukeni
- Kutokwa na kinyesi Ukeni
- Unapata maumivu ukeni
- Unahisi muwasho mkali
- Unaumia Ukeni,kwenye mashavu ya uke au wakati wa kujamiiana
- Unapata maambukizi ya mara kwa mara ya UTI au maambukizi Ukeni
Jinsi ya Kuzuia Tatizo hili la Uke Kujamba au Uke kutoa Hewa
Mara nyingi hakuna njia za moja kwa moja za kuzuia hali hii Lakini unaweza kuzingatia baadhi ya mambo;Epuka staili za Mapenzi ambazo hujaza hewa nyingi Ukeni n.k
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!