UPUNGUFU WA DAMU
• • • • • •
TATIZO LA UPUNGUFU WA DAMU KWA MAMA MJAMZITO
Katika hali ya kawaida kiwango cha kawaida cha damu kwa mama mjamzito hutakiwa kuwa juu ya kiwango cha chembe za damu yaani Haemoglobin 11 g/dl. Endapo kipo pungufu ya hapo,tunasema mama mjamzito yupo kwenye tatizo la upungufu wa damu mwilini.
Tafiti zinaonyesha kwamba Wastani wa kiwango cha kawaida cha damu kwa Mwanamke kipo chini kidogo ikilinganishwa na mwanaume,na wastani huu hutokana na changamoto mbali mbali anazozipata mwanamke kama vile; Blid ya kila mwezi au Period,Kujifungua ambapo damu nyingi hupotea N.K
Mama mjamzito akihudhuria kliniki,Moja ya vitu ambavyo huchunguzwa kwa ukaribu sana ni pamoja na wingi wake wa Damu, hii ni kutokana na kwamba,endapo mama atakuwa na kiwango kidogo cha damu atakuwa kwenye hatari zaidi wakati wa kujifungua kwani damu nyingi hupotea pia.
Lakini pia mama mjamzito akihhudhuria kliniki hupewa vidonge kwa ajili ya kuongeza damu maarufu kama FEFOL au FOLIC ACID, japo faida za vidonge hivi ni zaidi ya kuongeza damu,kwani pia huweza kusaidia katika uumbaji wa mtoto na kuzuia tatizo la kuzaa watoto wenye vichwa vikubwa pamoja na mgongo wazi.
VITU AMBAVYO HUWEZA KUSABABISHA TATIZO LA UPUNGUFU WA DAMU KWA MAMA MJAMZITO NI PAMOJA NA;
- Mama mjamzito kuwa na ugonjwa wa Malaria, ndyo maana pia moja ya dawa ambazo mjamzito hupewa hospitalini wakati wa mahudhurio ya kliniki ni pamoja na dawa za SP kwa ajili ya kumkinga mama mjamzito dhidi ya ugonjwa wa malaria.
- Mama mjamzito kushambuliwa na minyoo,ndyo maana pia moja ya dawa ambazo mama mjamzito hupewa akihudhuria kliniki ni pamoja na dawa za minyoo maarufu kama mebendazole.
- Lishe duni kwa mama mjamzito ambayo husababisha ukosefu wa madini ya chuma mwilini ambayo ndyo huhusika katika kutengeneza chembe chembe za damu.
- Mama mjamzito kuwa na ugonjwa wa Seli mundu au Sickle cell disease, tatizo hili huweza kusababisha upungufu mkubwa wa damu kwenye mwili wa mgonjwa, hata kupelekea mgonjwa kuwa na desturi ya kuchangiwa damu kila mara.
- Magonjwa ya mifupa ambayo huweza kuathiri utengenezaji wa damu kwa kupitia mifupa.
N.K
DALILI ZA UPUNGUFU WA DAMU MWILINI NI PAMOJA NA;
• Macho kubadilika rangi na kuwa na rangi kama nyeupe au njano
• Rangi ya viganja vya mikono kubadilika na kuwa kama nyeupe au njano
• Mwili kuishiwa na Nguvu
• Mgonjwa kupatwa na hali ya kupepesuka pamoja na kizunguzungu
• Lips za mdomo kubadilika rangi na kuwa nyeupe sio ule wekundu wa kawaida
N.K
•
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!